Mwingine aua kwa risasi naye kuuawa na wananchi kwa ugomvi wa ardhi huko Kahama

Hoho

JF-Expert Member
Apr 9, 2012
321
225
Migogoro ya kugombea ardhi imeendelea kusababisha vifo baada kikomgwe mweye umri wa miaka 87 mkazi wa kijiji cha Kahama wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga kumiuua kwa kumpiga na risasi ya kichwa mkazi mmoja wa kijiji hicho kutokana na ugomvi wa mashamba.

Hata hivyo kikomgwe huyo aliyetajwa kwa jina la Charles Makune (87) naye aliuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira waliofika katika eneo la tukio kwa lengo la kutaka kuamua ugomvi wa watu hao wawili.

Mauaji hayo yametokea ikiwa ni siku chache baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Mwanza Clement Mabina kuuawa na wananchi wenye hasira kutokana ugomvi wa kugombea ardhi.

Kandanda wa polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evaristi Mangala amemtaja aliyeuawa kwa kupigwa risasi na kikongwe huyo kuwa ni Mihangwa Mloziku (40) maarufu kwa jina la mambe, mkazi wa kijiji cha kuhanga na kwamba tukio hilo lilitokea Desemba 15, mwaka huu saa moja asubuhi kijijini hapo.

Afafanua zaidi kamanda Mangala alisema siku hiyo ya tukio Maziku akiwa nyumbani kwake alivamiwa na Makunde ambapo walirushiana maneno kutokana na ugomvi wa ardhi.

Alisema kutokana na kutokuelewana huko Makune aliondoka na kurusi nyumbani kwake ambako alikwenda kuchukua bunduki yake aina ya shortgun alioyo kuwa akimiliki kihalali na kwenda nayo nyumbani kwa Maziku na kisha kumpiga risasi kichwani na kufa papo hapo.

Kamanda Mangala aliendelea kufafanua kuwa baada ya wananchi kusikia mlio wa risasi walikwenda katika eneo la tukio ambapo katika harakati za kutaka kumkamata Makune baadhi yao waliamua kumpiga na kitu kizito kichwani hali iliyosababisha apoteze fahamu na kukimbizwa katika hosipitali ya serikali wilayani Kahama.

Katika kurupushani za kutaka kumkamata Mzee huyo baadhi ya wananchi ambao hawakufahamika mara moja waliamua kumahambulia kwa kumpinga na kitu kizito kichwani hili iliyo sababisha apoteze fahamu na kukimbizwa hospitali ya wilaya ambako alifariki juzi mchana na wakati akipatiwa matibabu.
 

mrelbattawy

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
564
195
rekebisha lugha yk mtoa mada kamanda unaandika kandanda au ndio kibongo kiswail cha tabu tabu.,,
 

Naytsory

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
2,176
2,000
Watauawa sana serikali isipovitazama kwa makini vyombo vya utoaji haki, hasa mahakama.
 

funza

JF-Expert Member
Sep 5, 2013
7,475
2,000
Watauawa sana serikali isipovitazama kwa makini vyombo vya utoaji haki, hasa mahakama.

Ucheleweshaji wa kesi na maamuzi ya utata ktk Kutoa Haki ni chanzo cha Haya Majanga .mahakama wangefanya kazi mpaka weekend Pia siku za kazi Mahakama zianze kazi saa moja asubuhi hadi saa 11 jioni angalau itasaidia kupunguza mlundikano wa kesi na kuharakisha Haki za watu
 

double diff

Member
Nov 17, 2013
12
0
kurudi(kurusi), kamanda(kandanda) duh we noma sana

Ila kama amemuua mwenzie kwa kumpiga risasi naye akauawa bac poa!
 

ngungwangungwa

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
573
500
rekebisha lugha yk mtoa mada kamanda unaandika kandanda au ndio kibongo kiswail cha tabu tabu.,,
Hayo ni makosa ya kawaida kutokea unapochapa. Lakini wewe umeharibu zaidi Lugha kwa kuandika'yk'badala yako. Na kiswahili umeandika 'Kiswail'.
 

Mapi

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
6,853
1,250
bulletproof zigawiwe bure kwa kila mwananchi. Naomba kuwasilisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom