Mwingine aagwa TISS, wa Ubalozi apewa Ukurugenzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwingine aagwa TISS, wa Ubalozi apewa Ukurugenzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 4, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nimeamka nikiwa na matumaini makubwa ya mwaka mpya na mojawapo ya mambo ambayo ka'nzi' kamenibrief ni mabadiliko ya ndani ambayo yametokea Idara yetu ya Usalama wa Taifa mabadiliko ambayo kama ilivyotarajiwa yanaendeleza kufahamianization. Mmoja wa wakurungezi amestaafu na kuagwa rasmi huko Mbweni, Bagamoyo.

  Mojawapo ya mambo ambayo tutayadokeza zaidi mwaka huu ni ulazima wa mabadiliko ya Idara ya usalama wa taifa kama nilivyodokeza kwenye Unleashed-Vol.1 Licha ya manung'uniko ya hapa na pale dhidi ya RO ndani ya idara hiyo bado mgawanyo wa maslahi unazidi kujaa na hasa tunapoelekea uchaguzi mkuu.

  Mmojawapo ya vyanzo vya kuaminika vinadokeza nia na kusudio la idara hiyo na wapambe wake kuhakikisha kuwa vyovyote itakavyokuwa hakuna challenge ya maana ambayo Rais JK ataipata toka ndani ya CCM kwani taarifa zimeshakusanywa za kutosha dhidi ya wale wote wanaotaka nafasi hiyo kupitia CCM na "mafaili" yao yatavutwa pale ambapo watajionesha wanakusudia kweli kweli kumpa changamoto JK.

  Natumaini Enigma na wenzake wakimaliza ripoti yao ya Silaha Haramu tutapata update ya uhakika ya nini kinaendelea ndani ya idara hii.

  Kwa mara nyingine, tunatoa shukrani kwa niaba ya taifa kwa mzee wetu wa TISS aliyestaafu kwa kulitumikia taifa kwa muda wote huu na kama ada na sheria Jina lake haliwezi kutajwa kumlinda yeye na familia yake. Huyo aliyeingia toka Ubalozini ameshazua manung'uniko kwani wapo ndani ya Idara watu wanaolalamika kurukwa tena vyeo hivyo kama ilivyotokea alipoteuliwa RO mwenyewe..
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Tunamtakia mapumziko mema.Kama ilivyo kwa wastaafu wengi, si busara kuamua kuchoka mapema na kuishi kwa lawama kwamba hakuna anayejali michango yenu.Ni vema kijipanga wakaendelea kutoa michango zaidi ya kutuwezesha watanzania wote kujitambua na kuona umuhimu wa kuwa na identity isiyoyumba come rain come sun.Yes bado wanaweza kabisa kutuonyesha mwanga wa wapi tunatakiwa kwenda kwa kutumia uzoefu wenu.
  Mungu akubariki na mapumziko mema kijiweni
   
 3. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu unaniachaga hoi kweli unapotuletea taarifa za TISS mara Mkurugenzi huyu kafa kazikwa tabata,mara Mkurugenzi huyu kastaafu kateuliwa mpya,mara...halafu mwisho unaweka ki excuse kwa mujibu wa sheria majina kwapani
  Sasa lengo lako nini hasa na ipi faida kwa wasiowajua hao waheshimiwa?
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Lengo ni kuwa wajue kuwa mchango wao unakumbukwa. Na ya kwamba wasilitumikie taifa wakifikiri kuwa hawawi appreciated. Ni gharama kubwa sana ya wao kuilipa. Ingekuwa ni wanasiasa wangeitisha vyombo vya habari au kupiga kelele Bungeni, hawa wenzetu hawana jukwaa hilo.
   
 5. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu naona ni wewe tu hapa JF ndiyo unakumbuka mchango wa hao watu(wenzako?) na ku appreciate manake ndiye unayetuletea taarifa zao hapa.Binafsi siwezi kukumbuka na ku appreciate mchango wa mtu kama simjui na sijui amelifanyia nini taifa kisa eti ni secret agent.Nitajuaje,labda ndiyo walewale vibaraka wa mafisadi?
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu hawa jamaa wa TISS wangekuwa na mahala pa kulalamika basi kusingekuwa na mtu Ikulu au ofisi ya PM. NI sawa na wewe unamwambia mtoto andika 1+1=2 yeye kila siku anaandika 1+1=96KPR, unaweza kuchukia sana na kuona kuwa unafanya kazi bure.

  Kama wangekuwa wanamwaga hadharani uozo wa wanasiasa wetu nadhani leo tungewakamata wote na kuwacharaza bakora. Pamoja na kuwa TISS kuna watu ovyo sana, majority ni watu makini wanaoangushwa na wanasiasa.

  Mchango wao ni mkubwa sana na tunauona, japokuwa hawapigi porojo kwenye vyombo vya habari kama wanasiasa. So let him pumzika, na kama ameamua kuingia kwenye public life asaidie tu kuwapa meno TISS. Sasa hivi TISS wanaonekana hopeless kwa sababu ya ujinga wa baadhi ya wanasiasa. Lakini the fact remains kuwa ni watu makini.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  mzee siyo sisi tu karibu nchi zote duniani kamwe hazitaji maagenti wake; kumbuka hapa hatuwazungumzii political appointee kama kina RO tunazungumzia watu ambao wamewezesha kesi za mauaji ya Albino kuletwa mahakamani baada ya Polisi kushindwa (niliwadokeza mwishoni mwa 2008 juu ya hilo), wakati mwingine mnasikia njama za uchaguzi zafichuliwa mtadhania zinatoka hewani, au baadhi ya mambo ambayo hata mlikuwa hamyajui yanatokea ni kwa ajili ya hawa watu ambao mshahara wao ni kiduchu cha watu wa BoT!
   
 8. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tisa ni kwamba watu hawa siku ya hukumu nao watasimama mbele ya Pilato kutoa yao maovu waliyoifanyia jamii,Kwani wana mengi sirini juu ya uovu na uozo wa viongozi dhidi ya umma wa watanzania.

  Kweli kama wanastahili sifa basi mambo yasingeachwa yaende shaghabagala kama hivi yalivyo.Wanasiasa mchango wao ni wa mpito tu ,Lakini jukumu kubwa la hawa mawakala wa usalama ni kuhakikisha mabo yote yako shwari(Stability and consistence).Lakini wapi bwana.

  Tunalewa nao tunabaka nao,na kuvizia nyumba kwa maana ya wake za watu tena huko majuu.Maendeleo ya Taifa Kiusalama kwao ni ndoto za Alinacha.
   
 9. M

  Mzee Kibiongo JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi niwatakie mapumziko mema (ya kustaafu) baada ya kupiga mzigo kwa time ndefu. Ni vizuri wamafahamu kuwa time yao imefika na hawakutaka kurudisha nyuma umri wao ili waendelee kula mema ya nchi ilhali wamechoka.

  Sasa hebu sikilizeni hili la huyo mkulu wa taasisi moja ya fedha ya umma hapa nchini ambaye alistaafu tangu 1997 kwa mujibu wa sheria lakini mwaka huo huo akapewa mkataba wa miaka mitatu ya kufanya kazi. Aliendelea na mikataba hadi tarehe 26/11/2009 mkataba wake wa mwisho ulipofikia tamati. Cha ajabu bado yuko ofisini hataki kuondoka, hana barua ya kumuweka kazini, wakuu wake wako kimya - yaani Wizara ya Fedha, Benki Kuu na Bodi yao ya Wakurugenzi, wote kimya!!!!!!!!!

  Sasa sikiliza vimbwanga anavyofanya huyu mkulu, kahakikisha anahamisha wale wote waliokuwa hawakubaliani na maamuzi yake ya kibabe na kuwapeleka mikoani bila kujali nyadhifa zao eti anafungua kanda. Hata madereva kawahamisha bila vitendea kazi (magari) ili mradi waondoke jijini (kwanza taasisi yenyewe haina mpango wa kununua magari mwaka huu, hii ni kwa mujibu wa bajeti iliyopitishwa na bodi yao tarehe 28/12/09). Kisa ? Eti yuko pia USALAMA WA TAIFA, hivyo hakuna wa kumgusa. Hivi, maamuzi makubwa anayofanya bila barua ya ajira/mkataba si ni batili. Wanajamvi naomba mnijuze kama ni halali jambo hili.

  Huyu mkulu sasa ana umri wa karibu miaka 70 na amechoka kweli kazi kusinzia tu ofisini. Jamani wakubwa wa nchi hii mwokoeni aende akapumzike, atafia ofisini. Tunataka kuona safari hii kama serikali na vyombo vyake vina meno ya kumng'ata bwana huyu ili haki itendeke.

  Iweje mtu anakaa ofisini ilhali hana mkataba !!!!! Marupurupu yake ya kustaafu keshalipwa, halafu mshahara wa mwezi Desemba kalipwa, sasa hatujui ni kwa mkataba upi. Mkuu wa kitengo cha Fedha cha taasisi hiyo kwa kuwa ni kibaraka wake naye kaidhinisha malipo kisirisiri lakini kwa kuwa malipo huwa yanapitia mikono mingi, siri imefichuka.

  Wanasebule, hebu fuatilieni jambo hili ili tuliweke wazi na huyo anayempa jeuri naye ajulikane ili hatua sahihi zichukuliwe dhidi yao wote. Hivi nchi hii haina watu wa kuweza kuendesha taasisi hiyo ila yeye tu ?????? Haya Mzee Kibiongo yangu macho ila sitaacha kupiga kelele hadi hapo nitakapoona uhalali wa jambo hili. Fuatilieni tu katika taasisi za umma za fedha nchini. Mkishindwa ndipo nitawatajia jina. Lakini najua Wanasebule hamuwezi kushindwa kuitambua taasisi hiyo na mkulu wake.

  Hadi baadaye.
   
 10. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  MKJJ,
  Sasa kama ndio hivyo na kwa siasa za bongo hapo si wazi kabisa uongozi unakuwa wa makundi na kujijengea maaadui, na nchi haito kaaa iwe na mustakabadhi hata siku mmoja kama Moja ya kiini cha nchi kinaweka watu wake ili itawale vyema, sasa si ndio Dictatorial Leadership style jamani?

  Tatizo letu kubwa ni kuwa nchi yaongozwa na group la jamii ya watu wachache kwa manufaa yao na sio ya watanzania wote, na ku reshuffle hilo group sijui kufanyike kitu gani.

  Ivi do people now kuwa usalama wa taifa ni kiungo muhimu sana ndani nchi yoyote ile na ndicho chaweza leta machafuko au usalama ndani ya nchi??sasa kikiingiliwa na mambo ya upendeleo fulani tumekwisha

   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Tumesikia mara kwa mara mawaziri wetu wakisema hawawezi kuwashughulikia mafisadi, ma sure kama TISS wangekuwa na meno ujinga huu tusingekuwa tunauzungumzia sasa, tungekuwa tunaona tatizo linaondolewa hata kabla ya kuingiza kansa kwenye jamii. Jamaa wanahitaji meno.

  wametufunilia facts nyingi sana kuhusu ufisadi lakini baadhi ya wabunge wetu wametuangusha, wengine wamenunuliwa na sisi wanachi badi hatujaorganised vizuri kuwashikisha adabu mafisadi, jamaa wanahitaji meno zaidi.
   
 12. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #12
  Jan 5, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Oh TISS!!! Iko kwa maslahi ya nani?? Simple-- Rulling party!!!!! To protect the interest of the one in power!!! Kumbe hiki ni chombo cha watanzania wote kwa usalama wa watanzania?? Mbona watanzania wanafanyiwa mambo mengi ya kifisadi na tunaambiwa eti uchunguzi bado bado bado mpaka lini?? Kama ni kweli walishughulikia suala la albino basi na uozo mwingine washughulikie.

  Kama kweli wanafanya kazi tusingekuwa na baadhi ya viongozi wazembe na mafisadi kiasi hiki. Wamelala hao!!
   
 13. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145  kumbe na wewe kama Augustine Lyatonga Mrema? wenzenu wewe na nani? Au mnajuana? teh teh teh -
   
 14. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Oooh mi sikufikiria hivyo......nilidhani aliposema ''Wenzetu'' alimaanisha.....watanzania wenzetu .....simple like that! hata na hivyo wacha nisiusemee moyo wake!
   
 15. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #15
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Etii ehh
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ni kweli idara inahitaji mabadiliko makubwa sana ya kisheria, kimuundo na kimfumo. Sasa hivi imegawanyika ndani kwa ndani kiasi kwamba ni vigumu kweli kutekeleza majukumu fulani fulani; matokeo yake ndiyo hayo tunayaona. Lakini mgawanyiko huu umetokana na wanasiasa zaidi kuliko maajenti wenyewe kwani hatuna mfumo mzuri wa kubadilisha na kusimamia idara ndio maana wale wanaoondoka sasa hivi wanaondoka wakiwa na manung'uniko kwa sababu kisheria hawawezi kuzungumzia mambo ya ndani ya idara ndani na hivyo manung'uniko yao hayasikiki isipokuwa kwa kupitia outlet kama hii.

  Ndio maana baadhi ya mabadiliko tutakayoyasimamia mwaka huu wa agenda 2010 ni mabadiliko ya hii idara ili iwe kweli moyo wa kijasusi wa taifa. Kutokana na kudunda dunda kwake kwa kwiki ndio tunawaona mafisadi wakionekana kupeta.
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Jan 5, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Kazi ipo..mdharau mwiba guu huota tende! Ninawaomba mwaka huu waupatilizie mbali mtandao wa aina yoyote hata kama formation yake inaanzia ofisi kubwa kubwa.Miaka hii mitano imethibitisha tunalipia gharama kubwa ya mitandao isiyo na kichwa wala mguu.Kama ilivyo kwa wawekezaji tunaowang'ang'aniza kila siku waje, mtandao umejaa matapeli kibao
   
Loading...