Mwingiliano TBS,TFDA kikwazo kwa wajasiriamali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwingiliano TBS,TFDA kikwazo kwa wajasiriamali

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by sulphadoxine, Jul 8, 2011.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MWINGILIANO wa utendaji kati ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) unachangia kukwamisha jitihada za wajasiriamali wadogo, katika kukuza uchumi wao na taifa kwa jumla.

  Akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro juzi, Mkuu wa Mradi wa usindikaji wa amatunda na mbogamboga kwa wajasiriamali wadogo wa Tanzania na Rwanda, Profesa Bendantunguka Tiisekwa,alisema mwingiliano huo ni tatizo katika maendeleo ya wajasiriamali.

  "Unaweza kukuta TBS inafanya ukaguzi katika viwanda na kutoa ushauri lakini baadaye wanakuja TFDA na kutia ushauri wao ambao wakati mwingine unakinzana na ule wa TBS,"alisema Profesa Tiisekwa.

  Alisema ni vema serikali ikatazama upya utendaji wa mashirika hayo ili kuondoa mwingiliano na hivyo kuwawezesha wajasiriamali wadogo kufanya shughuli zao kwa uhuru .

  Profesa Tiisekwa ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), alisema mbali na tatizo la mwingiliano wa mamlaka hizo mbili, pia kuna matatizo ya kisera na sheria zinazosimamia masuala ya chakula.

  Kuhusu mradi wa usindikaji matunda na mbogamboga kibiashara, mkuu huyo wa mradi alisema utasaidia kuinua vipato vya wajasiriamali.

  Alisema mradi huo unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu, una gharimu zaidi Sh 888 milioni na unalenga kuwafundisha wajasirimali wadogo namna ya kuendesha shughuli zao kwa ufanisi.
   
 2. g

  gonsalva mswaga Member

  #2
  Feb 5, 2013
  Joined: Oct 23, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mmmmmmhhhhhhhhhhhhhh kazi ipo hapo
   
 3. k

  kibaravumba JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2013
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 3,659
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Unajua TFDA kuna watu wanoko na wanakubana kwa sheria za kukopi Marekani bila kujali mazingira yetu na hasa ya mjasilia mali mdogo anayeanza!Hii kwa wafanyabishara wakubwa huwa haiwapi shida kwani wana uwezo wa kutoa rushwa kubwa kubwa!mfano tu ni baadhi ya viwanda vya dawa hapa nchini ni tabu tupu!kuna wakati niliuziwa dawa aina ya Malafin b/n 120002 zimetengenezwa may 2012 na zina exp Apr 2014 nilishindwa kuzitumia kwani zilkuwa na rangi ya ugolo kama vile zimelowa na chai au kahawa.Nilitoa ripoti lakini jamaa walichukulia poa tu!Angekuwa mjasiliamali mdogo ungeona waandishi wa habari wa kila chombo wameitwa kushuhudia watanzania wanavyovunja sheria!
   
 4. i

  iMind JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2013
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 1,907
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  TFDA ilitakiwa kuwa department ya TBS badala ya kuwa mamlaka. The same as RITA na NIDA. Kumekuwa na wimbi la uanzishwaji wa mamlaka na agencies katika serikali hii.
   
 5. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2013
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,105
  Likes Received: 1,492
  Trophy Points: 280
  TBS inahusika na viwango vya bidhaa TFDA inahusika na ubora wa chakula na madawa na kuna tume ya ushindani ambayo inahusika na bidhaa bandia ama bidhaa feki kila chombo kina majukumu yake kama umeuziwa bidhaa feki waone tume ya ushindani kama chakula au madawa yamepitisha muda waone TFDA
   
 6. k

  kibaravumba JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2013
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 3,659
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Asante kwa taarifa.Hii tume ya upinzani ina ofisi huku mikoani?Mbona hatujawahi kuona gata siku moja wakifanya kama tuwaonavyo huko Dar?Ama hata mawasiliano yao tu,kama hawana ofisi yatasaidia hasa kwa sie tulio mikoani.
   
 7. Mkoroshokigoli

  Mkoroshokigoli JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2013
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 14,419
  Likes Received: 2,519
  Trophy Points: 280
  unashauri nini sasa?kwamba TFDA wasiendelee na shughuli zao tule vyakula vibaya au?imagine wasingekuwepo TFDA hali ingekuwaje?au unashauri kwakua wafanyabiashara wadogo hata wakitengeneza dawa au vyakula visivyokidhi haja waruhusiwe maana ni wadogo?
  wadau me nahis TFDA wanajitahidi na waungwe mkono,maana nchi zinazotuzunguuka hazina maabara za kisasa kama za TFDA,hivi sasa wana maabara zilizoidhinishwa na WHO jambo ambalo SI TBS WALA MKEMIA MKUU HAWANA,wafanya biashara wana hila jaman wanaweza hata kutulisha kinyesi wao wapate faida,
  kama kuna mapungufu basi yafanyiwe kazi,TBS NAO WAJIPANGE BIDHAA ZISIZO NA UBORA ZISIINGIE
   
 8. Mkoroshokigoli

  Mkoroshokigoli JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2013
  Joined: Dec 20, 2012
  Messages: 14,419
  Likes Received: 2,519
  Trophy Points: 280
  mdau umedadavua vizuri sana,TFDA sidhan kama wana mtimanyongo na mtu maana nijuavyo mie kama sample imepelekwa na ikatolewa majibu endapo mwenye sample atahisi kuna walakini basi inapelekwa S.A kwa gharama za TFDA na iwapo majibu yatakuja yaleyale kama ya TFDA basi mwenye sample atalipia gharama zote,na ishawah kutokea hivyo na watu wakawajibika kulipia sample zao
   
 9. s

  snps Member

  #9
  Feb 9, 2013
  Joined: Jan 29, 2013
  Messages: 59
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  TBS wanajitahidi tuwaunge mkono lakini, TBS siasa tuu... wanapima kwa macho hakuna lolote... vifaa wanapigia picha tuuu lakini havifanyi kazi.. wanasiasa wakipitishwa na kuonyeshwa na kwa kuwa hawajui kitu wanakubaliana tuu. TBS wabadilike wafanye kazi za kweli.. msimu wa kuleta siasa umepita fanyeni kazi.
   
 10. k

  kibaravumba JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2013
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 3,659
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  TFDA wanatakiwa kuwa washauri elekezi(sina uhakika na kiswahili hiki mtanisahihisha) badala ya kuwa wakosoaji tu hasa wa bidhaa za ndani za wajasiliamali wadogo.Kwani hata wafanya bishara wakubwa duniani mf Colgate alianza kutengeneza dawa na kuiuza ki machinga na kadiri alivyoendelea alizidi kufanya vizuri hadi leo hii kuwa kampuni la kimataifa.Is kweli kuwa TFDA wanazuia bidhaa kwa vile tu ni feki,wakati mwingine wana wanaweza kuita hata bidhaa nzuri kabisa kuwa haifai kisa haijalipiwa kodi wanazotoza!mf ni mafuta ya Samona ambayo sasa yanauzwa waliwahi kuyapiga marufuku hata yasitangazwe,baada ya jamaa kuwatoa sasa ni halali!Unadhani mtu anayeanza kutengeneza atakuwa na mtaji wa kutosha kuanza kulipia kabla hata hajapata soko?Wanatakiwa kujua kuwa sisi hatuishi marekani kwa hiyo nitakapofunga mkate niliotengeza kwenye mifuko isiyo na lebo wapotezee tu hadi kamtaji katakapokuwa!
   
Loading...