Mwili wa Michael Jackson kufukuliwa kwa ajili ya uchunguzi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
mj-660x400.jpg



Kwa mujibu wa mtandao wa Radar Online unaripoti kuwa mwili wa Mfalme wa Pop Marehemu Michael Jackson unaweza kufukuliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi kufuatia tuhuma za ulawiti zilizotolewa na wavulana tofauti hivi karibuni.
Screen-Shot-2019-02-07-at-12.44.12-PM.png

Kupitia makala ya ‘Leaving Neverland’ imebaini kuwa Mfalme huyo wa Pop aliwahi kuwalawiti wavulana zaidi ya 30 wakiwa na umri mdogo huku waathirika 11 tayari wamejitokeza na kukiri unyanyasaji huo na kusema kuwa MJ alifanya kitendo hicho wakiwa na umri kati ya miaka 7 mpaka 14.
Inaripotiwa kuwa mmoja wa mashuhuda aliuambia mtandao huo kuwa MJ alikuwa akiwaliti watoto wengi kutokana na wao kwenda kumtembelea nyumbani kwake na alikua akifanya hivyo hasa kwa walemavu pamoja na wagonjwa waliokuwa wakisumbuliwa na magonjwa mbalimbali.
Screen-Shot-2019-02-07-at-12.44.43-PM.png

Kutokana na tuhuma hizo mwili wa Marehemu MJ utafukuliwa kwaajili ya vipimo vya DNA kwenye mabaki ya sehemu za mwili wake ili kuthibitisha ukweli unaosemwa. Mwaka 1993 MJ aliwahi kufunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya mvulana mwenye umri wa miaka 13.
 
Situnaambiwa huko ndio kuna haki inatendeka? Wamwache aendelee kupata mshahara wa matendo yake kwa kadri alivyoishi iwe ni raha au shida.

Wakifukua mwili wake na kubaini kweli alifanya hivyo vitendo, watamfungulia mashtaka au wanachukua hatua gani?
 
Sasa huu ni utoto wa kiwango cha juu, kwanini wasianze kuwapima hao watoto akili zao kwanza kama wana utimamu?

Yaani hii ni plan ambayo imewekwa ili kumchafulia jina MJ pamoja na familia yake. Hata wakipima wakikosa walichokua wakidhani watatoa majibu ya uongo ili wamchafulie jina kwenye familia yake

Sent using unknown device
 
Situnaambiwa huko ndio kuna haki inatendeka? Wamwache aendelee kupata mshahara wa matendo yake kwa kadri alivyoishi iwe ni raha au shida.

Wakifukua mwili wake na kubaini kweli alifanya hivyo vitendo, watamfungulia mashtaka au wanachukua hatua gani?
Sometimez hawa watu hamnazo.
 
Back
Top Bottom