Mwili wa mfanyakazi wa NMB wapatikana baharini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Marehemu Kilungulia ni mmoja wa wafanyakazi 11 wa Benki ya NMB, waliokuwa ndani ya boti ambayo waliikodisha kutoka Klabu ya Boti ndogo za kuogelea ya jijini Tanga (Yatch Club) kwa ajili ya kwenda kufanya utalii katika kisiwa kidogo cha kihistoria na utalii cha Toteni. aliyekufa . Boti hiyo ilipinduka baada ya kupigwa na wimbi.

Wafanyakazi hao wa Benki ya NMB Tawi la Korogwe walikuwa katika sherehe ya Siku ya Familia ya NMB (NMB Family Day).

Ajali hiyo ilitokea Jumapili saa 12:30 jioni, ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, ambapo watu 10 waliokuwa ndani ya boti hiyo walinusurika kifo baada ya kuokolewa na mmoja alikuwa hajapatikana.

Mwili wa Kilungulia ulipatikana Jumatatu mchana akiwa tayari amefariki dunia.

Kwa mujibu wa Wakala wa Meli Mkoa wa Tanga (TASAC), Christopher Mlelwa, wafanyakazi hao walikuwa katika kusherekea Siku ya Familia ya NMB na boti hiyo waliikodisha kutoka katika klabu ya Tanga Yatch Club.

Mmoja wa wafanyakazi wa NMB Tawi la Korogwe, ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa Kilungulia unafanyika kuupeleka nyumbani kwao Lushoto kwa ajili ya mazishi.

Mmoja wa wavuvi katika Bahari ya Hindi eneo la mwambao wa pwani ya Tanga, Yasin Jumanne (36) alisema kuwa kipindi hiki ni kipindi cha upepo mkali, hivyo wanaotumia vyombo vya majini wanatakiwa kuwa makini.

Picha

MWILI wa aliyekuwa mfanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Korogwe, Patrick Kilungulia (53), umeopolewa katika Bahari ya Hindi maeneo ya Jiji la Tanga.
 
Ajali haina kinga lakini nadhani walipaswa kushauriwa na Wakodishaji/Authorities kwamba huu muda walioteuwa kufanya tour yao haukuwa mzuri
Sijajua kama mtu yoyote akiamua kuingia baharini tuu anaingia bila kuangalia uwezo wake wa kukimudu chombo na chombo chenyewe uwezo wake wa kuhimili tafrani
Sijui niseme tumuachie Mungu itakuwa sawa
 
Hakuwa na Life jacket?RIP
Naomba mnifundishe; Life jacket huwa lina uhai ndani yake au?? Kwa sababu weye ni wa pili humu unaulizia hicho kitu. Wadhani ukiisha kulivaa weye huwezi kufa?? Mauti yako ilishaandikwa siku saa na mahali pa kukutana nayo.
 
Back
Top Bottom