Mwili wa marehemu Sir Andy Chande wachomwa moto

Wasomba

JF-Expert Member
Dec 19, 2016
389
533
Wakuu nipo njiani kuelekea Masaki katika kushuhudia kuagwa na atimaye mazishi ya aliyekuwa kiingozi wa Freemasonry Afrika Mashariki sir Andry Chande aliyefariki siku chache zilizopita jijini Nairobi.

Kufuatana na mila na desturi za kwao (kibaniani) mwili wa sir Andry Chande utachomwa moto na hatimaye mabaki yake kutupa kwenye bahari ya hindi na baadhi kwenye mto mtakatifu( the holy river) huko India.
Tunategemee viongozi wengi wa serikali kuhudhuria kwa kuwa sir Andry Chande alikuwa mchango mkubwa sana katika taifa hili.

Pia viongozi wengi wa Freemasonry kutoka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo.

Pale nitakapoweza kuingia na kuwapatia kapicha nitaingia na pale nitakaposhindwa kuingia kutoka na mila na desturi za Masonic kunizuia nitawatarifu kuwa nimeshindwa.

Update no 2.

Wakuu nimeshafika jirani na hapo. Kamkweche kangu nimekapaki huko mbali maana ni aibu. Nipo mita chache natupia jicho. Natafuta namna ya kujichanganya. Magari yanayoingia hapa ni kufuru kubwa. Kuna walinzi wengi. Mazingira tulivu. Watu na heshima zao, karibia wote wamevalia suti nyeusi nawaona wakishuka kwa mbali. Natamani nirudi nyumbani nikabadilishe ili niendane na muktadha.

Update 3
Wakuu kwa juhudi zangu binafsi nimefanikiwa kuingia kwenye makazi haya. Utulivu ni wa hali ya juu. Kila sehemu imeandikwa no photographing. Walinzi wengi mno. Kuna Watu wengi maarufu nawaona hapa. Ni hawa hawa tulionao mitaani na kuwatajataja kuwa ni wanachama wa club hii. Nitafanya kila namna niwaletee picha. Haiwezekani nisipigie picha hapa. Naomba muwe na subira. Subira yavuta heri. Kwa sasa nitatulia bila kuandika kidogo ili niendane na mazingira kabla sijatafuta namna ya kupiga picha.
Update no 4
Kuna mtu mmoja yuko hapa anapiga picha hovyohovyo tena bila wasiwasi. Hata mimi kaniphotoa. Amevaa pete kubwa mkononi ye nembo ya freemason naaam hata tai yake pia ina nembo ile ya bikali.
Napata SMS nyingi sana Wakuu kwenye inbox yangu. Tafadhalini sitaweza kuzijibu wala kutuma chochote. Kila kitu nitaweka hapa.

Update no 5

Nimefanikiwa kupiga baadhi ya picha. Nitawawekea hapa hapa baada ya kutoka mahali hapa. Vitu vingi wamefanya ndani. Mambo yaliyoendelea hapa nje niliyoweza kuchukua picha kwa Siri nitawawekea.
Update no 6

Wakuu Shughuli ya mazishi ndiyo inaendelea. Moto unawekwa kwenye kuni. Kuna vitu wanavipakapaka kwenye mwili. Hakika hizi sasa ni tamaduni za kibaniani.

Update no 7

Zoezi la limekamilika. Hakika ni moto kweli. Kuna fremason mmoja yupo kwa mbali kidogo nataka nimfate ili nipate maelezo kidogo ya hii kitu. Yule anaingilika. kijana mdogo wa kiafrika. Anaonyesha yuko under 25.


Maswali yangu kwa kijana:

Baada ya mazungumzo mafupi namuuliza maswali.
Mazishi haya ni ya kifrimasoni au ya kihindi?
Jibu: Fremason siyo dini bali ni imani. Hivyo mazishi ya mwanachama hufanyika kufuatana na dini yake. Mwanachama wa fremason hsruhusiwi kuwa na imani mbili tofauti na ya kifemason

Fremasoni inamsaidia nini mwanachama wake?
Jibu : Endless friendship, endless support and endless contact

When did you meet?

Answ: Monday and Friday evening

A freemason friend went further by telling that they are the people who control this World.
He told me that they influence a lot of things through medias. They also have big influence in politics though they don't practice politics in the lodge.

Bwana mdogo aliniambia kuwa kwa fremasons Vitu vitatu ndiyo muhimu na hupewa kipaumbele
I. Fremasonary -Ni muhimu kuonyesha utii na kwa fremason
2.Family-Ni lazima mtu apende na awe responsible kwa familia yake.

3. Work. Awe mchapa kazi .

Picha zaidi zitawajia.

Stay tuned with Omega.
 

Attachments

  • b0e1ba9a624e991e937d741e2f04c931.jpg
    b0e1ba9a624e991e937d741e2f04c931.jpg
    16.2 KB · Views: 509
Fanya ufanyavyo upate picha za mamasoni na viongozi walio karibu nao ikiwemo yule msanii kama nae yumo. Angalia kama mtekaji mkuu nae yumo umfotoe. Na wengineo waliotuaminishaga ni mamasoni.

Itasaidia kutofautisha wachawi wauza madawa na mamasoni wa ukwee. Maana hakuna masoni wa kweli atakosa kuaga bosi wao mkuu.
 
Fanya ufanyavyo upate picha za mamasoni na viongozi walio karibu nao ikiwemo yule msanii kama nae yumo. Angalia kama mtekaji mkuu nae yumo umfotoe. Na wengineo waliotuaminishaga ni mamasoni.

Itasaidia kutofautisha wachawi wauza madawa na mamasoni wa ukwee. Maana hakuna masoni wa kweli atakosa kuaga bosi wao mkuu.
Pamoja mkuu . Heshima nyingi sana.Hasa ndicho kilichonileta.
 
Wakuu nipo njiani kuelekea Masaki katika kushuhudia kuagwa na atimaye mazishi ya aliyekuwa kiingozi wa Freemasonry Afrika Mashariki sir Andry Chande aliyefariki siku chache, zilizopita jijini Nairobi.

Kufuatana na mira na desturi za kwao mwili wa sir Andry Chande utachomwa moto na hatimaye kuzika mavumbi yake.
Tunategemee viongozi Wendi wa serikali kuhudhuria Kia kuwa sir Andry Chande anao mchango mkubwa sana katika taifa hili.

Pia viongozi wengi wa Freemasonry kutoka nchi mbalimbali duniani wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo.

Pale nitakapoweka kuingia na kuwapatia kapicha nitaingia na pale nitakaposhindwa kuingia kutoka na mira na desturi za Masonic nitawatarifu kuwa nimeshindwa.

Taarifa zote nitakazozitoa zitaambatana na picha.

Stay tuned and wait to hear from me.
Vipi vyakula nataka niibuke
 
Umekumbuka kuvaa suti?? Kama hujavaa basi kuna uwezekano mdogo sana wa kuruhusiwa.... Naomba nisiulizwe kwanini
 
Back
Top Bottom