Mwili wa George Lutuhi siku 7 Mochwari hospitali ya kibena Njombe madaktari waomba ndugu kujitokeza kuutambua

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
1544181420835.jpeg

Serikali Mkoani Njombe Imewataka Watanzania Kujenga Mazoea ya Kutembea na Nyaraka Zote Muhimu za Utambulisho Wao Pindi Wanapokuwa Safarini Ili Kurahisisha Mawasiliano Wakati Linapotokea Jambo Lolote Linalohitaji Mawasiliano ya Dharura.

Wito Huo Umetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii Kutoka Hospitali ya Rufaa Ya Kibena Mkoani Njombe Bwana Samson Sollo Wakati Akizungumza na Vyombo Vya Habari Juu Ya Mkazi wa Mmoja wa Songea Aliyefahamika Kwa Majina ya George Lutuhi Ambaye Amefariki Akiwa Anapatiwa Matibabu na Hakuna Ndugu Aliyejitokeza Hadi Sasa.


“nauomba umma kuweza kutusaidia kuweza kuwapata ndugu wa marehemu GEORGE LUTUMO,amabye ni mkazi wa songea alikuwa ni mvuvi alikuwa akisafiri kuelekea Mtera mkoani Iringa siku ya tarehe moja mnamo saa moja na nusu asubuhi tuliweza kumpokea hapa hospitalini kutoka katika gesti aliyokuwa amepumzika na tumeweza kumuhumia lakini kwa bahati mbaya aliweza kupoteza maisha na tuliweza kutafuta taarifa zake hatukuweza kufanikiwa”alisema afisa afya

Bwana Sollo Amesema Marehemu Baada ya Kuugua Alifikishwa Hospitalini Hapo na wasamalia Disemba Mosi ya Mwaka Huu Akitokea Katika Nyumba ya Kulala Wageni ya Iditima Iliyopo Mjini Njombe Eneo Alilofikia Kabla ya Kuelekea Mtera Huko Mkoani Iringa Kwenye Shughuli za Uvuvi.

Aidha Afisa Ustawi Huyo Amesema Taarifa za Awali Walizipata Katika Nyumba Hiyo ya Wageni Alikofikia Kabla ya Umauti Kumkuta Lakini Kwa Bahati Mbaya Hakukutwa na Simu,Taarifa Zozote Wala Nyaraka Muhimu za Utambulisho Jambo Ambalo Limewalazimu Kutumia Vyombo Vya Habari Kutoa Taarifa Hiyo.

Alfred Melele ni Daktari Katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Njombe ya Kibena Ambaye Anasema Marehemu Anakadiriwa Kuwa na Umri wa Miaka 29 Hadi 30 na Alifariki Majira ya Mchana Siku Hiyo Hiyo ya Disemba Mosi.

“tulipima vipimo vyote kwenye Damu,sukari pia ilikuwa kawaida kipimo cha malaria kipimo cha virusi lakini marehemu alikuwa anatoa harufu mdomoni kama alikuwa amekunywa pombe sana na kuonekana kama alikuwa anatumia vidonge vya Parasetum inawezekana alikuwa anaumwa mda mrefu kwa hiyo alikuwa anatumia dawa na akatumia vinywaji vikampelekea kuto kujitambua na kuwa na hali mbaya”alisema daktari Melele

Dokta Melele Anasema Kwa Mujibu wa Taratibu Ndugu Wasipopatikana Katika Kipindi Cha Siku 14 Kuchukua Mwili Huo Basi Serikali Italazimika Kuuzika.

Mr.mtaani/mc.amiri

1544181507679.jpeg
 

Attachments

  • 1544181462202.jpeg
    1544181462202.jpeg
    190.1 KB · Views: 60
  • REPORT AMIRI KILAGALILA.mp3
    2.8 MB · Views: 16
  • SAUTI NDEFU YA MAELEZO.mp3
    4 MB · Views: 18
Back
Top Bottom