Mwili wa Gaddafi, Mwanae wazikwa sehemu ya siri Jangwani

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Hatimaye Gaddafi Azikwa Jangwani Eneo la Siri

6021146.jpg

Gaddafi alivyokamatwa
Tuesday, October 25, 2011 10:06 AM
Aliyekuwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi amezikwa leo alfajiri jangwani katika eneo ambalo halijulikani ili kuepuka wafuasi wake kuligeuza kaburi lake sehemu ya makumbusho.
Baada ya mwili wa Gaddafi kuanza kuharibika kutokana na kuwekwa wazi kwenye stoo ya baridi ya kuhifadhia nyama, hatimaye Gaddafi amepumzishwa kwenye nyumba yake ya milele ambayo NTC wameichagua kuwa iwe kwenye jangwa nene.

Muda mfupi baada ya Gaddafi kukamatwa na kuuliwa mjini Sirte mwili wake uliwekwa kwenye stoo ya baridi mjini Misrata na kuachwa wazi ili watu waishuhudie.

Mwili wa Gaddafi na mwanae ulitolewa toka kwenye stoo ya nyama mjini Misrata usiku wa kuamkia leo na kupelekwa kwenye maeneo ya jagwani ambako ulizikwa kwa siri.

Mazishi ya Gaddafi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 69 yaliongozwa na mashehe.

Wakati huo huo, mwenyekiti wa NTC, Mustafa Abdul Jalil amelazimika kuyarudisha mdomoni maneno yake na kujaribu kuwatoa hofu mataifa ya magharibi baada ya kutangaza kuwa Libya sasa itaongozwa kwa mujibu wa sharia za kiislamu.

Siku moja baada ya kutoa kauli hiyo, Ufaransa na umoja wa ulaya ulimuonya Jalili kuzilinda haki za binadamu.

"Tunapenda kuzitoa hofu jumuiya za kimataifa kuwa sisi Walibya ni waislamu na ni waislamu wa siasa za kati", alisema Jalili.

Jalili yupo kwenye wakati mgumu wa kuchagua wapi aipeleke Libya kwani kundi la waislamu wanaotaka sharia za kiislamu ndilo lililotoa mchango mkubwa zaidi katika kumng'oa Gaddafi.

Wakati huo huo, Mtoto wa Gaddafi, Saif al-Islam amefanikiwa kutoroka Libya hivi sasa akitajwa kuwa yuko kwenye mpaka wa Niger na Algeria.

Saif al-Islam akiongea na televisheni ya El Rai ya Syria ameahidi kulipiza kisasi cha kuuliwa kwa baba yake na ataviendeleza vita vilivyoachwa na baba yake.

Saif alisema kuwa yuko hai na bado yuko nchini Libya na yuko tayari kuendelea kupambana hadi mwisho.

"Nitaendelea kupambana hadi mwisho, nitaviendeleza vita dhidi ya waasi", alisema Saif.
 
Kila siku gaddafi gaddafi, kama vipi mfufueni "kila nafsi itaonja mauti" hakuna binadamu, sifa muhimu ya binadamu ni kufa. Sema tu ni kutangulizana, mwacheni baba wa watu apumzike huku tulio hai tukisubiri zamu zetu.
 
unamwonea huruma wakati kaishi maisha yake yote kama yupo peponi, kitanda cha dhahabu, bastola ya dhahabu, samani za ndani dhahabu tupu-- mtu mwenye mabillion ya dola alifikiria atazikwa nazo -- kifo ndiyo kikomo chao watu wanaojilimbikizia mihela kibao ya wizi wa mali za umma -- hata ukiwa na majumba ya kifahari mpaka london nadi Hollywood lakini fagio la chuma lazima likupate tu. tena wamemuua kistaarabu wangeanza kukata kiungo kimoja kimoja hadi afe. kaacha kila kitu duniani, ulikuja uchi unarudi hivo hivyo.
 
watajua wenyewe hata wangeamua kumchoma wamle nyama ingekua poa tu, wameshadhalilisha maiti yk vya kutosha lkn iko siku watayalilia mema aliyowatendea .
 
Ni muhimu kukumbuka mema aliyofanya.
lkn ni muhimu sana viongozi wengine kijifunza kutoka kwa gaddafi.
 
Ntashangazwa sana kama hawa waasi wataweza kuitawala Libya.


My broda JIMUSHI I SAPPORT YOU Killing of Gadafi cannot be the end of the problem in Libya, a man that manage the resources of his country well. How can we compare it with our country where the resources are just shared within 50 out of 40,000,000 people, no jobs no power bad roads, corruption etc.
Libya with the population of just 6,000,000 killed their leader whom did not allow the west to control him.
 
unamwonea huruma wakati kaishi maisha yake yote kama yupo peponi, kitanda cha dhahabu, bastola ya dhahabu, samani za ndani dhahabu tupu-- mtu mwenye mabillion ya dola alifikiria atazikwa nazo -- kifo ndiyo kikomo chao watu wanaojilimbikizia mihela kibao ya wizi wa mali za umma -- hata ukiwa na majumba ya kifahari mpaka london nadi Hollywood lakini fagio la chuma lazima likupate tu. tena wamemuua kistaarabu wangeanza kukata kiungo kimoja kimoja hadi afe. kaacha kila kitu duniani, ulikuja uchi unarudi hivo hivyo.
acha propaganda za magamba humu kuna dhahabu libya jamaa kaishi kwenye mahema miaka yote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom