Mwili wa Agnes Gerald 'Masogange' waagwa leo katika viwanja vya Leaders

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wasanii mbalimbali na wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wamejitokeza leo katika Viwanja vya Leaders, jijini hapa, kwa ajili ya kumuaga msanii anayepamba video za wasanii ‘video queen’ Agnes Gerald, maarufu Masogange.

Mwili wa Masogange umewasili viwanjani hapa saa 11:24 asubuhi hii.

Msanii wa filamu na rafiki wa karibu wa marehemu, Irene Uwoya alibeba msalaba wakati mwili huo ukiingia Leaders.

Wasanii wengine walioonekana viwanjani hapo ni Mrisho Mpoto, Jackline Wolper, Chege, Timbulo, Kajala na Aunt Ezekiel. Wengine ni ‘video queen’ Tunda, msanii wa filamu, Rammy Ghalis.

Mshereheshaji katika shughuli hiyo leo ni MC Pilipili.

Masogange anatarajia kuzikwa kijijini kwao Utengule, Mbeya kesho

IMG_20180422_123722.jpg
IMG-20180422-WA0028.jpg
IMG_20180422_130115.jpg
IMG_20180422_130119.jpg

Soma hapa pia; TANZIA: Agnes Gerald ‘Masogange’ afariki dunia Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge, Dar
 
RIP aggy..
It's too sad, umeondoka mapema mno huku malengo yako mengi hujatimiza!
Ila nakupa hongera kwa kumjali nzazi wako kumjengea nyumba. Ambayo ni ndoto ya kila mwanamke kuwajengea wazazi wake...
RIP + Hongera...
Kufa katika Kristo ni Faida...!
 
Hao kina mama wanahuzunisha walahi!
Ehh Maulana Mola wangu tusaidie!
 
Wasanii mbalimbali na wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wamejitokeza leo katika Viwanja vya Leaders, jijini hapa, kwa ajili ya kumuaga msanii anayepamba video za wasanii ‘video queen’ Agnes Gerald, maarufu Masogange.

Mwili wa Masogange umewasili viwanjani hapa saa 11:24 asubuhi hii.

Msanii wa filamu na rafiki wa karibu wa marehemu, Irene Uwoya alibeba msalaba wakati mwili huo ukiingia Leaders...
Hapo kwenye RED unamaanisha saa 11 alfajiri?...
RIP Agness...
 
Utengule Usangu, unaingilia Igurusi, barabara ya Iringa - Mbeya, unafika kijiji cha Usangu then unaenda sasa kijiji cha Utengule, kwenye bonde la Usangu maarufu kwa kilimo cha Mpunga, ufugaji wa mbuzi na Ng'ombe, wakazi wake wengi wao wenyeji wa Mbeya, wasangu, wasafwa, wanyaki na wasukuma waliohamia na kuweka makazi yao katika hili bonde wakilima mpunga na mahindi na kufuga, nimepata kuishi kwa muda katika hili bonde.

Sikujua kama Masogange ni mzaliwa kutoka katika hiki kijiji.

Rest in Piece Agnes Masogange.
 
Masogange anatokea Utengule ya Mbalizi, Njia ya kuelekea Mkwajuni Chunya.
 
Utengule Usangu, unaingilia Igurusi, barabara ya Iringa - Mbeya, unafika kijiji cha Usangu then unaenda sasa kijiji cha Utengule, kwenye bonde la Usangu maarufu kwa kilimo cha Mpunga, ufugaji wa mbuzi na Ng'ombe, wakazi wake wengi wao wenyeji wa Mbeya, wasangu, wasafwa, wanyaki na wasukuma waliohamia na kuweka makazi yao katika hili bonde wakilima mpunga na mahindi na kufuga, nimepata kuishi kwa muda katika hili bonde.

Sikujua kama Masogange ni mzaliwa kutoka katika hiki kijiji.

Rest in Piece Agnes Masogange.
Umekosea Mkuu...ni utengule usongwe kata ya mbalizi mbeya vijijini. Wenyeji wa huko ni wasafwa.. Wakulima wa mahindi, maharage, kahawa. viazi aina zote na pia ni wafugaji wazuri tu.MAREHEMU NI MSAFWA ORIGINAL KUTOKA KWA WAZAZI WOTE.
 
30590336_162637241088121_8896675469743620096_n.jpg
MATUKIO KWA PICHA : Tukio la kuagwa mwili wa Video Vixen, Agnes Masogange viwanja vya Leaders...hamisamobetto... esha.s.buheti na Wengineo wamefika kuaga Mwili wa Marehemu
30602917_1959309021051254_7085383865761529856_n.jpg

MATUKIO KWA PICHA : Tukio la kuagwa mwili wa Video Vixen, Agnes Masogange viwanja vya Leaders.....@mrishompoto ...@chegechigunda na Mkewe wajitokeza kuaga mwili wa marehemu .
30592714_1758982970849346_1364875714007924736_n.jpg

Pichani ni baadhi ya wasanii wa Tanzania na Moja ya hao ni Wasanii Wa BongoFleva. Diamond Akiwa na Mpinzani Wake Mkuu. Alikiba na Pembeni Harmonize.
30087114_816019718608922_2666580838572883968_n.jpg

Baadhi ya wasanii waliojitokeza [HASHTAG]#LeadersClubKinondoni[/HASHTAG] kumsindikiza kipenzi chetu Agness Masogange.
 
Back
Top Bottom