Mwili kuchoka sana na maumivu makali ya mgongo

Good Neighbour

JF-Expert Member
Jul 12, 2017
887
1,000
Habari Wakuu,
kwa zaidi ya mwezi sasa nimekuwa nikipata tatizo la
1.mwili kuchoka sana kusiko kwa kawaida
2.maumivu makali ya mgongo

Hapo zamani nlikuwa mtu wa kufanya mazoezi,nliacha mazoezi sababu ya kuskia mavumivu kwenye miguu hasa nikiwa nakimbia.Nikiwa katika kutembea nakuwa sawa kabisa/Very Normal,ila baada ya kukimbia umbali mkubwa kama 7-10Km kwa siku 3/4 kuendelea basi miguu huanza kuniuma na kupelekea kuacha mazoezi

Nikiri kuwa nina weight kubwa kuliko BMI yangu (iko kwenye overweight).Lakini tatizo hili la mgongo kuuma sana na mwili kuchoka mno limeanza zaidi ya mwezi sasa Na katika kipindi hiki sijaongezeka uzito
Urefu 177cm
uzito 93Kg
Naomba msaada/ushauri zaidi wa kiafya
 

kijana13

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
1,553
2,000
Usiache mazoezi yawe sehemu yako ya maisha changamoto za miguu au misuli kuuma Ni kawaida Sana kwa kila mkimbiaji na u anaweza tatua Hilo...endelea na mazoezi plus kula vyakula vya kupunguza uzito..nenda hospital pia kacheck kiwango chako Cha sukari

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom