Mwijaku akutwa na kesi ya kujibu shtaka la kusambaza picha za utupu kinyume cha sheria

Mtapenda

JF-Expert Member
Sep 20, 2011
1,115
2,055
Mtangazaji wa Clouds, Mwemba Burton maarufu Mwijaku amekutwa na kesi ya kujibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Ni baada ya Serikali kufunga ushahidi wao wa mashahidi watano na vielelezo vinne walivyoviwasilisha wakati wa ushahidi.

Mwijaku anakabiliwa na shtaka moja la kusambaza picha za utupu kinyume cha sheria.

Pia, soma; Mwijaku afikishwa Kisutu na kushtakiwa kusambaza picha za utupu. Ashindwa kutimiza masharti ya dhamana

mwijaku.jpg
===

My take
Ndio maana jamaa anajitahidi sana kujipendekeza kwa mama Samia ilia apate huruma...
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemkuta na kesi ya kujibu Mtangazaji wa Clouds FM, Mwemba Burton maarufu Mwijaku katika shtaka la kusambaza picha za utupu kinyume cha Sheria linalomkabili
-
Mwijaku anashutumiwa kusambaza picha za utupu za Msanii wa Bongo Movie, Menina Alegria kati ya Septemba 17, 2019 na Oktoba 2019
 
na kujipendekeza kote kwa ccm na kwa mama ila serikali hipo pale pale .
fundisho kwa ccm na chawa
 
Back
Top Bottom