Mwijaku afikishwa Kisutu na kushtakiwa kusambaza picha za utupu. Ashindwa kutimiza masharti ya dhamana

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,369
217,430
Mwijaku.JPG

Mwijaku ambaye ni miongoni mwa watia nia waliojitokeza kuomba ubunge kwa tiketi ya CCM, amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkaazi Kisutu kwa kusambaza picha za utupu kwenye mtandao wa Whatsapp.

Inadaiwa alitenda kosa hilo kati ya Septemba 15 na Oktoba 10 mwaka 2019 .

------
Aliyekuwa mtia nia wa Ubunge Jimbo la Kawe na Mtangazaji wa Clouds, Mwemba Brighton maarufu Mwijaku (35) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kusambaza picha za utupu.

Mwijaku alisomewa mashtaka hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate.

Mwijaku ambaye alikana mashitaka hayo, amekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ambayo ni kuwa na wadhamini wawili kutoka ama Bongo Movie au tasnia ya muziki wenye barua zilizothibitishwa na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na kusaini kila mmoja Sh 500,000.
 
wajumbe sio watu wazuri sanaaa...walichomoa betri/jina lake mapemaaaa👋
 
Back
Top Bottom