Mwijage azomewa na wabunge kutoka Zanzibar

Ketoka

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,087
1,913
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage leo Ijumaa Septemba 7, 2018 amejikuta katika wakati mgumu bungeni mjini hapa baada ya kuzomewa na wabunge kutoka Zanzibar.

Alikumbwa na mkasa huo wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua sababu za Serikali kuendelea kuzuia sukari ya kiwanda cha Mahonda kuuzwa Tanzania Bara.

Katika swali lake, Jaku amesema haiingii akilini kuona bidhaa kutoka Zanzibar kuwa ngumu kuingia katika soko la Tanzania Bara, wakati zile za Tanzania Bara zinaingia kirahisi Zanzibar.

Katika majibu yake, Mwijage amesema katika kipindi cha uongozi wake hawezi kuruhusu sukari kutoka kiwanda cha Mahonda kuletwa Tanzania Bara kwa maelezo kuwa bado kuna vitu vya kuhoji ndani ya kiwanda hicho.

Kauli hiyo ilizua mvutano mkali bungeni na wabunge wa Zanzibar walianza kupiga kelele kwa sauti za juu wakipinga majibu hayo.

“Mheshimiwa mwenyekiti naomba nikuelekeze wewe majibu yangu na wabunge wanaotaka kunisikiliza, lakini wale wasiotaka waache waendelee kupiga kelele tu,” amesema Mwijage.

“Mimi ninasimamia kuwa kiwanda cha Mahonda kinazalisha tani 4,000 wakati mahitaji ya wananchi wa Zanzibar ni tani 20,000, je hiyo wanayotaka kuuza huku wanaitoa wapi? Siko tayari kukubali hata wakizomea.”

Kuhusu sukari iliyorundikana kwenye viwanda, Mwijage amesema vyombo vya dola viko kazini na tayari wamegundua ndani ya uchunguzi huo kuna jinai hivyo kuna watu ambao watashughulikiwa.
 
Huyu ni waziri wa pili kwa kuwa na NUKSI , namba 1 ni Mwakyembe
 
Kweli kabisa Kwasababu hata mimi mpaka sasa sijaelewa kazi ya huyu jamaa
 
“Mheshimiwa mwenyekiti naomba nikuelekeze wewe majibu yangu na wabunge wanaotaka kunisikiliza, lakini wale wasiotaka waache waendelee kupiga kelele tu,” amesema Mwijage.

“Mimi ninasimamia kuwa kiwanda cha Mahonda kinazalisha tani 4,000 wakati mahitaji ya wananchi wa Zanzibar ni tani 20,000, je hiyo wanayotaka kuuza huku wanaitoa wapi? Siko tayari kukubali hata wakizomea.”

Kuhusu sukari iliyorundikana kwenye viwanda, Mwijage amesema vyombo vya dola viko kazini na tayari wamegundua ndani ya uchunguzi huo kuna jinai hivyo kuna watu ambao watashughulikiwa.

Hawa jamaa wajanja sana, bila umakini hapa tutaweka kwenye kekundu, na hapa wanatafuta mbinu ya kukifunga kamba kisiwa wakivutie mbali kule, jiulizeni mfuatano wa matukio ya hivi sasa, mara petition UN, mara kesi ya uhalali wa Muungano, mara tukikatiwa umeme tutawasha vibatari nk
 
Huyu ni waziri wa pili kwa kuwa na NUKSI , namba 1 ni Mwakyembe

kuna shemu nilisoma naye mwaijaje. Tokea chuo alikuwa ni mpiga makelele yasiyo na tija. kuna hasara gani ya sukari ya znz kuingia ktk soko la tanganyika? Ni suala dogo kwa ajili ya 'good spirit of the union' na serikali ya makufuli ingeiruhusu bidhaa hiyo kuingia ktk soko la T/ Bara.

Znz kwa muda mwingi imekuwa ikitumia bidhaa nyingi tukutoka T/ bara , sasa leo serikali ya znz iamue kuweka marufuku ya bidhaa za T/ bara zisiingie znz , siitakuwa hasara kubwa kwa pande mbili za muungano?

miaka ya nyuma wakti wigo wa biashara ulipokuwa haujapanuka sana, znz walikuwa wakipata mahitaji ya vyakuka kutoka nje ya Tz na hususan India na nchi nyengine za mashariki ya mbali. Sioni anavyofanya Mwaijage kuwa sawa?Nafkr angetafakari zaidi.
 
They want to eat their cake and have it. Wanataka kuula (kufaidi utamu wa) uhai wa muungano; ili usife?
 
Kama wanazalisha tani 4,000 na mahitaji ni tani 20,000, wanatoa wapi ya kuuza bara au wanazalisha 4,000 ila kimuujiza wana tani 60,000?
Jibu ni rahisi. Gharama za umeme ni kubwa,uzalishaji ni gharama. Nikiuza Zenj, bei ndogo sipati faida kama kuuza Tanganyiks. So, naagiza ya bei che Muskst,nauza nyumbani na ya nyumbani nauza nje kiwanda kiendelee nilipe mkopo! Right?
 
Back
Top Bottom