acha matata
Senior Member
- Jan 5, 2011
- 165
- 39
Nikiri kuwa mimi ni mwana-ccm niliyehama chama kwakutupa kadi kapuni baada ya kuona chama kimetekwa na mafisadi. Wapo wengi sana wanamna hiyo ninaowajua.
Pia nikiri kuwa mimi ni miongoni mwa watu waliotokea kumchukia Mwiguru Nchemba alipojitoa ufahamu na kusemekana kupanga mipango ovu juu ya vyama pinzani vya ccm hasa hasa CHADEMA.
Kwasiku za karibuni, Mwiguru amekuwa akijipambanua kwahoja nzito na zenye mashiko kwa umma. Hata hivyo, nimekuwa nikiendelea kuwa na mashaka.
Leo nikisikiliza hotuba yake na kuilinganisha na ya Lowasa, Nchemba ameendelea kuwa na hoja za mashiko kama kweli zikitekelezwa. Hoja kama za 1. Makao makuu kuhamia Dodoma; 2. Mbinu za kuinua viwanda vya ndani 3. Mbinu za kuongeza ajira; 4. Kurekebisha mifumo ya ajira kwenye utumishi ya umma;
Walio wengi wetu tulimsikia jana Mh. Ngoyae Lowasa; ambaye inasemekana watanzania wengi matumaini yao yako kwake (!!??). Binafsi sikupata ramani kamili na njia mbadala atakazotumia kuufikisha umma wa watanzania Kwenye nchi ya uchumi wa kati. Angalau nimeiona kwa Mwigulu Nchemba.
Napenda kujifunza kutoka kwa wenzangu.
Nawasilisha