Mwigulu: Wananchi wanaenda kupata fedha nyingi, watazoea makato

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,009
9,874
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema wananchi wasiwaze kuhusu gharama za miamala ya simu kwa kuwa mzunguko wa fedha utaongezeka

Akiongea katika kipindi cha Aridhio, TBC amesema gharama za miamala hazina maana kwa kuwa watakuwa wanapata fedha zaidi katika kipindi hichi

Amesema serikali imejipanga kulipa madeni ili wananchi wawe na fedha

Kwani kila mwananchi anaidai serikali? huu uongo wake hautoshi, angesema serikali imejiandaa kugawa fedha kama pipi mitaani ningeuelewa huo uongo wake, naona sasa ameamua kubuni kila aina ya jibu kila anapoulizwa hilo swali.
 
Hawa watu wamelewa madaraka na wamebaki kukebehi watu. Wanaona kila mtu asiyekuwa kiongozi ni mjinga na unaweza kumdanganya kadiri unavyotaka. Kwa nini wasisubiri kwanza wananchi wapate hizo fedha ili waanze makato? Upole na woga wa watanzania umefanya viongozi wafanye wanavyotaka!
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema wananchi wasiwaze kuhusu gharama za miamala ya simu kwa kuwa mzunguko wa fedha utaongezeka

Akiongea katika kipindi cha Aridhio, TBC amesema gharama za miamala hazina maana kwa kuwa watakuwa wanapata fedha zaidi katika kipindi hichi

Amesema serikali imejipanga kulipa madeni ili wananchi wawe na fedha

IMG_20210715_213635_704.jpg

Mwigulu must go!
 
Huyu mtu aache kufuru. Amezoea kupata fedha nyingi bila jasho. Amesahau wengine hutoka jasho. Hela kuzunguka zilizokua zinaliwa walituambia ni zile za serikali kufisidiwa. Madilu anatuambia wanaenda ruhusu ufisadi ili hela zizunguke?
 
Yani waziri mwigulu haaminiki Tena kwa kauli zake huyu ndiye aliyewahi kutuambia uongo eti magufuli yupo ikulu anachspa kazi kumbe rais wetu ni marehem tayar,aliwadanganya watanzania.

Nadhani baadhi ya viongozi wa serikali wanatumia ukimya was watanzania na uoga wa watanzania kufanya maamuzi ya ajabu Kama advantage
 
Back
Top Bottom