Mwigulu unatuaibisha products za Mlimani...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwigulu unatuaibisha products za Mlimani...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Oti Kate, Jun 21, 2012.

 1. Oti Kate

  Oti Kate Member

  #1
  Jun 21, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wana JF

  Kwa kweli huyu mwigulu anatuaibisha sana sisi wote ambao tumesoma chuo kikuu sehemu ya mlimani. Niliposikia kwa mara ya kwanza akijisifu kuwa yeye ni mchumi wa daraja la kwanza kutokea mlimani then BoT, nilisema ayamkini kijana
  ameteleza ulimi, so sikutegemea kusikia tena akijinasibu kwa maneno hayo!

  Cha ajabu jana akiwa TBC katika mdahalo, alirudia maneno hayo tena na zaidi. Sasa wewe Mheshimiwa (wa kuiba wake za watu) wach huo utoto, hayo mambo ya kijisifia elimu na uwezo wako, hebu waachie watoto wa std. 7 na form one, wewe angalia nini wana-Iramba magharibi wamekutuma au wamekosa kule jimboni ili uwawakilishie kwa wahusika hapo mjengoni.

  Kama kila mtu angeamua kujisifu hapo bungeni kuhusu shule yake, nadhani muda wa bunge la bajeti usingetosha......kumbuka kuna maprofesa humo humo ndani ya CCM ingawa Mchungaji Msingwa alituthibitishia kuwa wanafikiri kama watoto wa darasa la pili, lakini kumbuka wameenda shule.

  Hebu wacha huo utoto, fanya kilichokupeleka bungeni........................unatuabisha wenzako tuliopitia mlimani, tutaonekana kichwa maji kaka wewe!
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hivi kuna product ya Mlimani iliyopo CCM? Hao ni wale ma-papet tu. Leo bajeti yetu inalingana na ya Ruanda, halafu graduate uko CCM? Huu ni usaliti kwa waTanganyika.
   
 3. B

  Babuu Rogger JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 898
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 60
  Huyu jamaa kwa kweli nimemshangaa sana, anakuwa kama mtoto mdogo kabisa, hata kama wameambiwa waiteteee bajeti kwa namna yoyote. Na hakuna mahali aliponikera kama alipoitupa bajeti ya kambi ya upinzani. Yeye asome alama za nyakati na aendelee kuwalamba miguu wakubwa zake ila ipo siku ataumbuka.
   
 4. calculator

  calculator JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Angekuwa ni CHADEMA mwenzenu mngejiunga wote kumpa shavu. Kwani TUNDU LISU kila siku anapojisifia hamuoni wala hamskii??? Na wewe umepata wapi legitimacy ya kuwasemea waliopita UDSM? Kwa hoja hii uliyoijenga hapa, nashawishika kuamini wewe ulikuwa mtunza bustani hapo UDSM. Unaboa sana
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,571
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Watu kama kina Mwigulu nchemba kule usukumani wanaajiriwa kama wachunga ng'ombe.kazi yao ni kupeleka ng'ombe Lubaga maana yake ni kupeleka ng'ombe porini ambako kuna marisho ya kutosha.Nchemba analijua hilo.
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 180
  Sasa na ako kadegree kake kama angesoma Harvard na kufanya kazi IMF AU WORLD BANK naona angeamulu bunge zima walale chini apite juu yao!
  He is so myopic I never imagined msomi angeweza tamka maneno hayo!
  Nchi ina matatizo makubwa ya msingi kama kuongezeka kwa deni,inflation,reliance on sigara and beer for increased revenue,
  Sasa serikali wametenga 35% ya dvt expenditure based on donor money sasa wakisema kubalini ucameroun otherwise hatuwapi ela si miradi itakwama.
  Sasa Mwigulu badala ya kupigani iyo ela itokane na fedha za ndani anashupalia yeye nii first class economist!
  Sisi wa darasa la 2004 umetudhalilisha!
   
 7. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2012
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,585
  Likes Received: 605
  Trophy Points: 280
  Guys hivi anavyosema mchumi daraja la kwanza ina maana first class au ni cheo cha huko BOT alikokuwa. ninavyojua kama umeajiliwa especialy serikalini kuna aina hiyo ya vyeo, kama ni mchumi toka chuo na kadegree kako basi unaanza na dalaja la pili, then baadaye unapandishwa kuwa mchumi daraja la kwanza, then unakuwa mchumi mwandamizi mpaka mwandamizi mkuu kama sikosei. huyu jamaa sidhani kama alipata kweli first class mbona kama hajui chochote ni kama mzee DHAIFU tu
   
 8. Challenger

  Challenger Member

  #8
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 5, 2007
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilimuangalia na kumsikiliza Mwigulu - Mwisho nikahitimisha kuwa zile hoja ni SIASA tu!!
   
 9. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #9
  Jun 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Umenifurahisha ulivyoiandika "waTanganyika"
   
 10. N

  Nyambu Member

  #10
  Jun 21, 2012
  Joined: May 5, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwigulu ni kichaa hana akili kbs,anaongea km yuko ukumbi wa taharabu anarusha bajet wananyamaza ila wa chadema angerusha wangeomba mwongozo,akili yao sawa na mropokaji Rusinde,ccm wamewekeza kwa waimba taharabu,
   
 11. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tena atakuwa awawazalilisha zaidi watu wa UD ambao bado wapo NyinyiEM
   
 12. calculator

  calculator JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
   
 13. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #13
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,666
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Kuna Watu walitembelewa na M4C wakaamua kuwanunulia wananchi wao Vazi la mwisho baada ya safari ya Hapa duniani!! Badala ya kununua Hata Madawa kwenye Hospitali za Serekali!! Mimi nashauri kwa watu Kama Mwigulu Inatakiwa M4C ipige Kambi kidogo kwenye Jimbo lake na pia aanze Kuona kama safari ya siasa Katika maisha Yake imefika ukingoni / Kikomo!! Ni hatari sana kwa mbunge wa jimbo kushindwa kuwatetea wananchi waliomtuma na kuanza propaganda Mufilisi!!
   
 14. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #14
  Jun 21, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 9,860
  Likes Received: 3,167
  Trophy Points: 280
  mbona na mimi nina first class gpa ya uhasibu na wenzangu kama kumi hivi!it's no big deal!nchemba alikuwa mchumi daraja la kwanza na sidhani kama ni gpa
   
 15. calculator

  calculator JF-Expert Member

  #15
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mtakaa sana. M4C kwenu hukohuko. Mnaumwa na nini nyie chadema lakini??
   
 16. U

  Udaa JF-Expert Member

  #16
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 727
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu kuanzisha thread nyingi zinazohusiana na (chemba)tunakosea,kz yake chema ni kupitisha uchafu.SASA KUNA ASIYEJUA?
   
 17. U

  Udaa JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 727
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu kuanzisha thread nyingi zinazohusiana na (chemba)tunakosea,kz ya chemba ni kupitisha uchafu tu.SASA KUNA ASIYEJUA?
   
 18. g

  gongolamboto JF-Expert Member

  #18
  Jun 21, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Unajua kuna kitu kinaitwa elimu na kuna kitu kinaitwa IQ. Unaweza kuwa na elimu kubwa lakini IQ yako ndoooooogo kabisa. Ndiyo maana huyo anayejiita mchumi daraja la kwanza anafananishwa na mtoto wa darasa la pili kwa sababu IQ yake ni sawa na mtoto wa darasa la pili
   
 19. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #19
  Jun 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 973
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 60

  Wewe ni miongoni mwa wale walamba miguu ya wakubwa ili mdondoshewe chochote,inawezekana Mwigulu alikua na hoja ila jinsi alivyokua akijisifia elimu yake ilitosha kwa mtu mwenye akili timamu kumdharau.Wapo ma prof wengi tu wala wajisifii elimu yao,haya ya kujisifia elimu inafanywa na wanafunzi wa kidato cha nne.
   
 20. The Planner

  The Planner JF-Expert Member

  #20
  Jun 21, 2012
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 344
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Naanza na nakuu hii," Ni bora ukae kimya watu wakadhani wewe ni mjinga kuliko kuongea na kudhihirisha fikra zao"
  Alianza Nape, Wassira, Lusinde sasa Nchemba kweli siasa inafanya tuprove uwezo wa watu kufikiri
   
Loading...