Mwigulu unaambiwa Wanafunzi 5000 waloingia Kidato cha Kwanza Hawajui Kusoma/Kuandika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwigulu unaambiwa Wanafunzi 5000 waloingia Kidato cha Kwanza Hawajui Kusoma/Kuandika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Penguine, Jul 6, 2012.

 1. P

  Penguine JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 29, 2009
  Messages: 1,226
  Likes Received: 390
  Trophy Points: 180
  Nilisikiliza kwa karibu sana marumbano ya wabunge wetu Bungeni kuhusu mijadala ya bajeti ya Serikali. Wapo walioneena kwamba hakuna uwiano wa moja kwa moja kati ya maudhui ya bajeti hiyo na Mpango wa Taifa wa maendeleo. kwa maana hiyo maudhui ya Bajeti hayafanani na Dira ya Maendeleo ya Taifa na Strategic Plans za Taifa.

  Lakini wapo Waliojadili kwamba maudhui ya bajeti hiyo hayaoneshi kutatua matatizo ya Walimu ndiyo maana ktk maeneo kadhaa, baadhi ya waalimu wamekuwa wakifanya biashara zao kazini ili kujiongezea "mboga juu ya ugali wenye kachumbari peke yake mezani" (hii ni tafsiri yangu binafsi)

  Kisomi, MWIGULU angeamua kuwa mtafiti juu ya Ukweli wa yaliyomo kwenye aya ya pili hapo juu angeamua kutafiti UKWELI WA WAPINZANI KWAMBA WALIMU WANAFANYA BIASHARA MASHULENI. Katika utafiti huo, pamoja na viashiria vingine, angeweza kupima ongezeko la watoto wanaojua kusoma na kuandika. hii ni kwa sababu kujua kusoma na kuandika ni matokeo ya kuwajibika kwa mwalimu na umakini wa mwanafunzi.

  Sasa kama tafiti zilizotangulia Mjadala huu wa Bajeti zinaonesha kwamba ZAIDI YA WATOTO 5000 wameingia kidato cha kwanza katika mwaka 2012 wakiwa hawajui kusoma na kuandika, NAJIULIZA, Mwigulu Mchemba atalipinga vipi Angalizo la Kambi ya Upinzani Bungeni juu ya Walimu kuamua kufanya biashara zao shuleni.....ikiwa na maana kwamba kudorora ktk ufundishaji ili waeze kujiongezea kipato kupitia biashara zao kwani kazi ya kufundisha haiwakomboi?
   
Loading...