Mwigulu tena ndio usiongope kabisaa katika suala la elimu kwamba ccm imewekeza ni uwongo mkuuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwigulu tena ndio usiongope kabisaa katika suala la elimu kwamba ccm imewekeza ni uwongo mkuuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwigamba son, Jun 18, 2012.

 1. Mwigamba son

  Mwigamba son Member

  #1
  Jun 18, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  sisi yatima tuliofiwa na mzazi/wazazi/watoto maskini ccm imetufungia fursa ya kupata elimu ya juu kwa kutunyima mikopo ya elimu ya juu kwa kigezo cha mature age na equivalent ina niuma sana nina first class diploma in accountancy mzumbe walinipa admission ya kuendelea na degree lakin bodi ya mkopo ya ccm ikasema hakuna mkopo kwa equivalent wala mature age kwa sasa niko mtaani sina ajira natamani kuongeza elimu lakini tumaini hilo limefutwa hivyo naendelea kumtegemea mama yangu ambaye ni mjane.

  Sasa nikuuulize swali Mwigulu na ccm yako je ccm haijavunja katiba kwa kuwabagua watanzania katika suala la elimu .kutoka ndani ya moyo wako una fikiri elimu ya juu tanzania inatolewa kwa kufuata misingi ya usawa? Hiyo OC uliyoipamba kwamba imefanya makubwa kwenye elimu ni yapi mbona umaskini wetu umezidi. na fursa za elimu zimetoweka ukilinganisha na kipindi cha Mkapa?

  Kwa maana nyingine jibu unalo hivyo kidole ulichonyoosha juu ya chadema kilikuwa ni kimoja huku ukisahau kuwa vinne vilivyobaki vilikurudia wewe na ccm yako. Watanzania tumesoma na tuna akili timamu siku zenu watawala zimekwisha. Nitakuwa mpumbavu mimi mwenye diploma kama nahitaji elimu ya juu halafu niwasifu ccm. kwa lipi labda Mkapa peke yake ambaye kwenye utawala wake elimu ya juu ilikuwa bure.

  Mwigulu HAKI HUINUA TAIFA BALI DHAMBI NI AIBU YA WATU WOTE hivyo acha wapinzani watutafutie haki ili na sisi wanyonge tusome elimu ya juu tukiwa na equivalent zetu na mature age zetu . ee Mungu wape hekima na uadilifu wapinzani na uwezo wa kukubalika mashambani na mijini pia ili 2015 waiokoe Tanzania yenye neema Amina...
   
 2. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kijana huyu Mwigulu a.k.a mfumaniwaji hana tofauti na Lusinde ndio maana wanaenda wote, kwa kiongozi mwandamizi wa chama tawala asingetupa hotuba ya bajeti ya upinzani hata ingekuwa rubbish kiasi gani aana hiyo ni document iliyotumia fedha za walipa kodi.
  Si busara kabisa aliyotumia huku akishangiliwa, suala la serikali kukosolewa na upinzani ndivyo ilivyo kwenye mabunge yote duniani. Wapinzani huisema serikali ili ijitazame inapokosea iende sawa, Mwigulu ametia aibu kwa chama chake na LUKUVI hakumuona kama alivyofanya kwa Lissu wala Mabumba naye alikula pini. Aibu kwao CCM.
   
Loading...