Mwigulu: Nimeelekeza vyombo vinavyohusika kuchukua hatua kwa watu wanaozusha taarifa za magonjwa au vifo

Waziri wa Mifugo sorry ..
Usitupangie maisha yetu na familia zetu
Corona ipo watu wanakufa unatuletea kiherehere cha kujipendekeza
Haijafika nyumbani mwako ndio maana
Hizi Amri dharau kebehi siku parapanda ikilia nyumbani mwako utakaponyamaza kimya utakuwa na jambo la kumsimulia aliyekutuma kweli?!
 
Unafki tu.

Sheria rundo zinakanyagwa, katiba inachezewa na kugeuzwageuzwa na wenzake... Hayo hayaoni ila anakuja kukimbizana mitandaoni sababu tu wanaguswa wao.

Ndimi mbili mbili.

Hii mambo bhana... Mungu tu atunusuru.
 
Kwani kuna mtu anaweza kuzuia kifo ambacho Mungu kapanga?,
Baada ya corona kwisha aubkupungua vifo vitaendelea tu.
Tatizo ni waongo na wale wanaofulahia vifo kwa kujifanya wanatangaza taarifa za uongo bila uhakika.
 
Ukisha kuwa kiongozi hakuna private ni lazima watu waambiwe hali zao sababu wewe ni kiongozi.

Sasa ndugu waziri kuzima hizi zote kelele maana zingine sio za kweli ila watu wanaamini tu kwa sababu hata serikali wanaongoza katika kuongea uwongo watu hawaamini mnachosema hata kama ni kweli ukisha kuwa muongo hata ukija kusema ukweli watu ngumu kuamini.

Njia pekee ya hili ni serikali kuongea ukweli kuhusu hali za viongozi na mambo mengine yote ujenge imani na watu ili wawe wanasikiliza serikali tu sababu taarifa zao za uhakika. Maalim Seif kama sio chama chake kusema wazi Corona hakuna mtu angejuwa. Katibu mkuu kiongozi unakuja kutangaziwa kifo tu, kuweni wazi sababu sio dhambi wala aibu mtu kuumwa.

Tofauti ya mimi na wewe mimi nikumwa watakaonijuwa family na friends tu lakini wewe wote wanakujuwa sababu ni kiongozi. acheni mambo ya kizamani ya siri siku hizi kila mtu mwandishi habari social media lazima mjiongeze mwende na mabadiliko watu hawasubiri kusoma kesho gazeti la Uhuru.
 
Mbowe na wenzake walizomewa sana waliposema na kutoa ushauri wa kuokoa watu dhidi ya janga hili, matokeo yake walibezwa na kutungiwa kila aina ya majina mabaya. Leo hii tunaona umma unavyoteketea halafu tunaambiwa tunyamaze?
 
Muelekeze nguvu hizo kutenda mambo yanayoisaidia jamii kuwa na afya njema ili kupunguza tetesi na matangazo yanayoanzia neno TANZIA.
 
Mwigulu Nchemba acha ujinga wako na tamaa zako za kimadaraka, kujipendekeza kwako ndio kaburi.

Mpaka huyu mdudu agonge hodi nyumbani mwako ndio tuanze kutangaziana?

Acha uduanzi!
 
Back
Top Bottom