Mwigulu: Nimeelekeza vyombo vinavyohusika kuchukua hatua kwa watu wanaozusha taarifa za magonjwa au vifo

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
565
1,000
Taifa lipo kwenye Msiba wa viongozi wetu ambao wametangulia mbele za haki kwa Mapenzi yake Mungu, Kumetokea tabia mbaya ya kuzushiana, (Na fulani anaumwa, na fulani naye anaumwa.

Mara nasikia fulani amekufa na fulani naye amekufa), Huku ni kukosa UTU, ni kuathiri maisha Binafsi ya mtu, Familia yake na kusababisha TAHARUKI kwenye Jamii.

Kifungu cha 16 cha Sheria ya Mitandao kinazuia watu kutoa taarifa za uongo. Nimeelekeza vyombo vyote husika kuchukua hatua bila kusubiri mtu binafsi akalalamike.

Nani amekupa kazi ya kufuatilia afya za wengine na kuwa msemaji wa hali zao?

TUACHE TABIA HII MARA MOJA.

Mwigulu Nchemba
Waziri katiba na sheria
 

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
2,878
2,000
Na ninyi mlioibadilisha corona jina na kuiita nimonia kali/changamoto za upumuaji mchukuliwe hatua gani?

Plz Mr Nchemba achaneni na vitu visivyo na msingi hangaikieni maisha ya watanzania kwani hii korona inaziacha familia nyingi na wakati mgumu.Kina mama wamekuwa wajane na watoto wamekuwa yatima kwasababu ya huu ugonjwa.

Zielekeze hasira zako kwenye mikakati yakuhakikisha tunaishanda korona kuliko huu mpango wako wakulipa kisasi kwa niaba ya viongozi wanaoshukiwa kuwa na korona.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom