Mwigulu, ni kweli kulipai na kukusanya kodi ni heshima kwa nchi lakin kuombaomba ni aibu kwa nchi

BALAKI

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
371
0
Ktk kikao cha bunge kilichomalizika hivi karibun waliskika wasemaji wengi wazalendo na wasema kweli kadhalika na wale ambao wanaowadanganya watz ni wazalendo na wakweli. Akichangia juu ya kodi ya simu Mwigulu alidai kuwa ni sahihi kuwekewa kodi hiyo kwa kisngizio cha kuboresha huduma za umeme na maji vijijin.
Akaenda mbele zaidi na kusema kulipa kodi ni heshima kwa nchi jambo ambalo lilinistua kwa sababu kama kulipa na kukusanya kodi ni heshima kwa nchi iweje leo nchi ijipatie heshima kwa kuwa ombaomba tena kiongozi wa nchi akitembeza kibaba kaskazin mpaka kusin, magharibi mpaka mashariki ya dunia huku akiandamana na jopo lake ''officials'' linaloifilisi kodi ya mtz kwa gharama kubwa za malazi na chakula.
Huku viongozi wa serikali kama bw Muhongo akiliambia taifa ujinga wa viongozi wetu akiwemo yy mwenyewe kuwa migodi ya tanzanite yenye wawekezaji zaid ya 500 wanaoilipa kodi ni kama 10 walilipa kodi ya sh 30mil kwa miaka 5. Hii ni kukiri kuwa serikali haikusanyi kodi halafu yenyewe inajilalamikia na kujishangaa. Lipi jepesi na la heshima ndg zangu watz, kukusanya kodi ama kutumia hata hicho kidogo kuzurura na kibaba cha msaada kwa hao mabepari wenye conditions nying kwa misaada yao?
Hapa ndipo ambapo siwez toa sifa kwa viongoz wangu wa ccm, kwa kipi wanachofanya ktk hili la kukusanya kodi? mnatuchefua wananchi kwa kauli za kipumbavu wakat wenyewe ndo wasimamizi na watendaji
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom