Mwigulu Nchemba - wananchi hawana imani na uteuzi wako/Asha Rose Migiro-anaonekana katumwa

Hawa wateuliwa wameanza kujishtukia, leo katika gazeti la Nipashe nimesoma wameanza kukanusha.
Waliteuliwa juzi, wakaapishwa jana, leo wakaanza utetezi. Je umepima mtiririko ma matukio? Wameamua

Ukweli, kama watasaliti wateuzi wao, utabaki pale pale. 1. Migiro - kuhujumu mchakato wa Katiba Mpya ili, au muundo wa serikali mbili urudi, ikishindikana, muundo wa serikali tatu ukose theluthi mbili ya kura kwenye Bunge la Katiba. Kisha CCM kuendela kubaki madarakani. 2. Nchemba - kukusanya fedha kwa njia zozote zile kwa ajili ya CCM - kuwahonga wapiga kura. Time will tell. Ila, dalili ya mvua ......



Mmmmm.....uovu utawaumbua siku ya mwisho
 
Tatizo la dogo nchemba ni.utotooooo... Kujitamba yeye first class material ni matusi kwa wananchi wa iramba.....na wasomi wa tz. Sijapata ona kiongozi mwenye dharau kama huyu. Hajakomaa kisiasa, na nina waswas kama wizara itamkubali kwa kejeli zake. Akumbuke kuwa first class sio kipimo cha weredi na ufanisi wa kazi......kwanza hayupo katika kundi la wasomi...phds. Nina wasws kama atamudi huo utafiti wake anaojigamba anasoma.....
 
Wewe ina frustration na wivu wa kike tu.

Kwanini nisiwe na frustration wakati hazina inakwenda kuvunjwa? Kwanini nisiwe na ftrustration wakati urithi wa kizazi cha leo na kesho unaharibiwa.

Wengi tunategemea kulipa kodi na serikali kutoa huduma bora za jamii sio kulipa kodi halafu wachache waziibe. kweli hilo linachanganya. Hongera wewe uliyetulia.
 
Bado sijaamini kwamba Mwingulu na Malima ndio Manaibu wa Wizara ya Fedha.Huenda J.K.akatangaza Manaibu wiki ijayo.

Inabidi uamini ndugu yangu. Inauma sana hasa kwa watu wenye mapenzi mema na Tanzania. Watanzania tulichuma janga mwaka 2005 sasa lazima litutafune na vizazi vyetu.
 
Ni hivi mkuu, huwo mzaha wanaotaka kuufanya utawagharimu, kwasasa tulipofika hakuna mpuuzi yeyote yule mwenye cheo chochote kile atakayeweza kutumia eti mamlaka yake kuendelea kuwakandamiza watanzania, sikilizia operesheni#PAMOJA DAIMA (CHADEMA) then mtu aingie kichwa kichwa....

Huyu mama alipoondoka nchi Tanzania nadhani alikuwa hajaijua Chadema vizuri ndiyo maana akaingia mkenge... sasa tunaenda kimuonyesha nini maana ya nguvu ya umma na hicho wanachotaka kukifanya, sasa kama yeye alikuwa ni mtu wa kuambia tu nadhani anawajibu wa kuona kwasasa kazi ya operesheni hii kisha apeleke ripoti kwa boss wake kuwa uchakachuaji umeshindikana....

WATATUPUUZA LEO, WATATUHITAJI KESHO

Kamanda Kileo nimekusoma ila isitokee eti baadaye CHADEMA imeikaba ccm kooni halafu Kikwete analetwa Uswahili wa Mseto na Mazungumzo tuyamalize. Hawa jamaa(ccm) ni wahauni sijawahi kuona huwezi kumuweka Adam Kighoma Malima na Nchemba Wizara ya Fedha inayobeba uchumi wa nchi halafu bado eti mkaendelea kucheka nao hawa watu, Napendekeza chama kiimarishe pia intelijensia ya kufuatilia utendaji wa hawa jamaa na pia usalama kwenye Operation hii mpya uimarishwe Angani na Aridhini.
 
Wewe ina frustration na wivu wa kike tu.

hili ni jukwaa la GT, kama huna hoja bora ukukaa kimya na kusoma michango ya wenzio kuliko kuleta huu upumbafu wako ktk mambo ya msingi yanayogusa maisha yetu ya kila siku! pambafu sana ww na unaowatu
ikia.
 
Mungu akikukosesha akili bwana! Kwa mifumo ya sasa senti ya serikali itatoka je hazina kwenda chama cha siasa? yaani mnamaanisha wafanyakazi wa BOT, banks, hazina ni wanachama watiifu wa CCM. hivi kama mtu mwenye access na mtandao hana uwezo wa kung'amua hata hili? How about nyanya yangu kule kijijini)
 
Simply krap... ila unajitahidi kuota mchana!

Ni kwanini hili swala la kupoteza fedha za walipa kodi masikini ninyi haliwaumi? Hivi kweli inaingia akili kumwandaa msomi kama Asha Rose Mtengeti migiro kwenda kuharibu mchakato mzima wa katiba uliotumia mamilioni ya walipa kodi masikini?

Kweli ni busara kupeleka team hazina kwa ajili kutoa fedha za kampeni na kuacha watoto, waja wazito, wazee, kwa vijana wakifa kwa kukosa huduma za afya fedha zote uchaguzi?

kweli kuacha wataalamu wa maswala ya fedha waliobobea, na kutea wapiga debe wa wasiasa wasio na udhoefu zaidi ya kampeni chafu za kudhuru binadamu matusi, na kashfa za akila aina?

Haki haijawahi kupendwa, kweli haijawahi kukubalika, na nuru huwa hufunikwa ila mwisho wa siku tutakuwa mashajuu kwa kutetea kizazi chetu na kijacho.
 
Siku hizo ilikuwa sahihi. Siasa za chama kimoja hizo. Siasa za ushindani hazina tabia hiyo
Asante Mkuu, kumbe ndivyo ilivyo, basi kumbe hatuna sababu ya kushangaa teuzi mbalimbali maana kumbe mfumo wa vyama vingi Usalama wa Taifa hawahusiki kabisa. Looh, inasikitisha saana, sitoshangaa siku moja tukaona watu tusiowafahamu wakashika nyadhifa muhimu katika nchi. Kutohusisha Usalama wa Taifa katika teuzi hakika ni kujimaliza wenyewe, kumbe mfumo wa vyama vingi unalegezasana mambo muhimu. Asante kwa kunielewesha Mkuu.
 
baraza jipya ni mshahara wa unafiki wa watanzania, kila mara tunaacha kuspoti tatizo kinafikinafiki eti mawaziri, oho mfumo, ohooo basi fujo tupu, tunajifanya hatuoni kuwa tatizo ni raisi. tuache kuwa madebe matupu kulalamika tu. hili baraza la mawaziri ni dharau ya waziwazi isiyohitaji elimu ya chuo kikuu kuitambua. tutaacha kudharauliwa pindi tukiacha unafiki, ni wakati sasa wa kumkataa rais sio mtu mwingine, mwacheni pinda na wenzake kwani wao ni sehemu ndogo ya tatizo. Hatumwambii ukweli ameamua kututemea mate usoni.
 
Fue umesema kweli kuhusu Migiro, yule mama ni mtupu kabisa. Ametutia aibu kule UN, na sasa anakuja kucheza na damu za wanyonge. Tuone Mwisho utakuwa vipi?
 
Zamani baba yangu alipokuwa katika "System" alinisimulia kuwa teuzi zote za viongozi Mwalimu alikuwa anazifanya kupitia ushauri wa Usalama wa Taifa na alihakikisha kuwa anapata mtu anayeaminika walau mbele ya jamii, sasa sijui siku hizi kama bado hilo lipo ama ni teuzi zinafanywa na team inayoshilikisha Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu. Kama Usalama wa Taifa hawahusiki katika hili, basi ni hatari maana anaweza akaingia mtu asiye na sifa. Ama siku hizi teuzi zinafanyika kwa ushauri wa chama?

Usalama wa taifa unaouongelea wewe ni upi? Hivi bado unadhani kuna usalama wa taifa? Huo ni usalama wa viongozi wabadhilifu na ubadhilifu wao.
Tafadhali naomba uondoe hiyo dhana ya usalama wa taifa. Futa kabisa kichwani mwako.
 
mwigulu hawezi kubadilika kwa umri alofikia. kwanza ana mdomo mchafu yaani maneno yasiyo na hadhi ya mtu mzima licha ya unaibu waziri. yaani hana hekima
 
Mhe.Mwigulu Nchemba kamtukana mtanzania gani na kwa wakati gani jamani? Tuache fitina,tuwe wakweli.

Malumbano ya wanasiasa na siasa zao Msituhusishe watanzania kwa Ujumla wetu.

Mhe.Nchemba ni mtu makini na mweledi.Ni mwanasiasa mahiri na anayejua kuisimamia na kuitetea hoja yenye tija. Alichokuwa akikifanya Bungeni kama Mbunge,ni sahihi kabisaa...hana cha kumuonyesha eti ni Kiongozi asiyefaa,eti anamatusi,sijui maninii...Kwani Sugu mnavyoona anafaa na kustahili kuwepo Bungeni kama ndio hivyo?!

Mie ni Mtanzania,na sina upande wowote kiitikadi.Navutiwa na Uongozi wa baadhi ya Viongozi na kweli wapo ambao SIONI utendaji wao na SIJUI kama kweli wao wenyewe wanajiona ni VIONGOZI MZIGO katika Taifa hili.

Maoni yangu,ni bora tukawa na Serikali ya Kitaifa (isiyojali huyu anatoka chama gani,ila awe na sifa na uwezo), badala ya kuongeza mzigo tena mkubwa na usio na tija wa SERIKALI TATU.

"HAKIKA TUTAJUTA WATANZANIA WENZANGU".
 
Back
Top Bottom