Mwigulu Nchemba: Uchumi wa Tanzania umekua licha ya mlipuko wa COVID-19. Deni la Serikali ni himilivu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema licha ya mlipuko wa COVID19, Tanzania ni miongoni mwa Nchi chache zilizokuwa na ukuaji wa Uchumi chanya kwa mwaka 2020.

Amesema Pato la Taifa la Tanzania lilikua kwa 4.8% na sekta zilizochangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji ni Ujenzi, Habari na Mawasiliano, Uchukuzi na Uhifadhi wa Mizigo, Huduma zinazohusiana na Utawala, Madini na mawe, Afya na huduma za Jamii

DENI LA SERIKALI LIMEFIKIA TRILIONI 60.9, NI HIMILIVU

Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema hadi Aprili 2021, Deni la Serikali lilikuwa Trilioni 60.9 ambapo kati ya kiasi hicho, Deni la Nje ni Trilioni 43.7 na la Ndani ni Trilioni 17.3. Deni linatokana na kupokelewa Fedha za Mikopo kwa ajili ya kugharamia Miradi ya Maendeleo

Imeelezwa, Deni ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vinavyokubalika Kimataifa

PIA, SOMA=> Bungeni, Dodoma: Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba kusoma bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha 2021/22

 
R.I.P Magufuli

Ulikataa lock down kwa watanzania licha ya chadema kukimbia bunge na kwenda kukaa lockdown.
 
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema licha ya mlipuko wa COVID19, Tanzania ni miongoni mwa Nchi chache zilizokuwa na ukuaji wa Uchumi chanya kwa mwaka 2020

Amesema Pato la Taifa la Tanzania lilikua kwa 4.8% na sekta zilizochangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji ni Ujenzi, Habari na Mawasiliano, Uchukuzi na Uhifadhi wa Mizigo, Huduma zinazohusiana na Utawala, Madini na mawe, Afya na huduma za Jamii
Anaikumbuka sababu aliyoitoa Rais juu ya kutopandisha "salare" siku ya mei mosi.. kuna Watu bado wapo na mentality za siasa za ulaghailaghai tu
 
Kuwa na mtazamo tofauti siyo kwamba ndo ni mpinzani mkuu, sema tunaangalia hali za watanzania kwa ujumla je kinachosemwa kinaendana na uhalisia wa maisha yetu?
R.I.P Magufuli

Ulikataa lock down kwa watanzania licha ya chadema kukimbia bunge na kwenda kukaa lockdown.
Sasa uchumi umekua.
 
Mbona mnashindwa kumuelewa? You are thinking emotionally!

Amesema ni moja kati ya nchi chache zilizokuwa na ukuaji uchumi chanya 2020. Au kwenye hiyo 4.8% mmeona alama ya negative?

Na ni kweli nchi nyingi duniani uchumi ulikuwa unasoma negative something.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchumi wa kwenye karatasi na Watu wachache walioko kwenye hatamu kwanini usikue

Ila Uchumi uchumi halisi umedorora saana
 
Siasa safi, uwazi na uwajibikaji kwa viongozi ndiyo tatizo la nchi hii. Ushabiki wa kisiasa pia ni sumu kwa maendeleo yetu.
 
Back
Top Bottom