Mwigulu Nchemba timiza wajibu wako ndani ya chama...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwigulu Nchemba timiza wajibu wako ndani ya chama...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tanzaniaist, Aug 31, 2012.

 1. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wanaJF...!

  Leo ni Rai moja tu, kumwambia mh.Mwigulu Lameck Nchemba mbunge wa Iramba Magharibi na Katibu wa Fedha CCM (chama tawala) kufanya majukumu,kazi na wajibu wake ndani ya CCM..! sisi wote tunajua kazi ya Mbunge ni nini na vile vile kazi ya Ukatibu wa fedha ni majukumu gani...!

  Unapokuwa kiongozi mahali popote lazima uwe na VISION,PLAN na STRATEGIES..,kama mbunge mipango yako ni kuwakilisha wananchi bungeni,kusimamia,kushauri na kuhoji mipango ya serikali katika kutimiza wajibu wake kwa wananchi..,na vile vile kuwa sauti ya wananchi unaowakilisha..,kama mbunge Mh.Mwigulu Nchemba amekuwa akijitahidi sana katika kazi zake za kibunge...!

  Tukija katika Nafasi yake nyingine kama katibu wa fedha ndani ya CCM, naona hapa huyu mheshimiwa amesahau majukumu yake..,nilitegemea siku alipoteuliwa kushika nafasi hiyo angewaeleza wanachama wa CCM ni nini hasa mipango yake katika kufanikisha chama kiwe na fedha za kutosha,kiwekeze vizuri katika rasilimali zake,kupunguza gharama za uendeshaji,kuwaongeza makada motisha za posho...,na mipango yake baadaye katika kukiendeleza chama Kiuchumi na kifedha...,

  Sisi wengi tulikuwa mashuhuda baaada ya uchaguzi mkuu 2010, CCM walikuwa na hali mbaya Kifedha na hili linatokana hasa na mipango mibovu ya mapato na matumizi na kutegemea RUZUKU..,CCM ni chama ambacho kina rasilimali nyingi tu..,majengo,ardhi..na tatizo kubwa sana CCM ni FEDHA ndio maana chama kimevamiwa na MAFISADI wanaomwaga hela chafu ili kupata kinga na mwisho wake CHADEMA wanapata cha kuwasema kwenye majukwaa...!

  Tangia uchaguliwe kuwa katibu wa Fedha Mh.Mwigulu sijaona utendaji wako kwenye hili baadala yake ni kwenda Igunga na Arumeru kwenye kampeni..,
  1.Nilitegemea ungefanya ziara ya kukagua rasilimali za CCM na kuona chama kitaweza kufaidika nazo vipi, au mipango ipi ifanyike chama kiweze kuongeza kipato zaidi kupitia rasilimali zake
  2.Nilitegemea ungewatembelea makada na makatibu kwenye mashina ya CCM kuona kwamba chama kitaweza kuwasaidia vipi kujiajiri kwenye ujasiriamali kuliko kutegema RUZUKU kutoka makao makuu,
  3.Nilitegemea ungekuwa mtu wa kwanza kutoa ushauri wa jinsi gani chama kipunguze matumizi hasa kwenye mikutano mbali mbali ambayo imekuwa ni mzigo mkubwa kwa chama mkizingatia wenzenu CHADEMA wamebuni mbinu mbadala ya kuchangisha wananchi kupunguza gharama..!
  4.Nilitegemea utupe Mchakato wako wa kukikuza chama zaidi kiuchumi na kifedha, na kutafuta wahisani zaidi kukisaidia chama kuliko kutegemea ruzuku

  Kwani kazi kubwa ya katibu wa fedha,ama mkurugenzi yeyote wa fedha duniani..,ni kuhakikisha taasisi inaongeza pato,inapunguza gharama,inapunguza utegemezi,inahudumia vizuri rasilimali zake na inakuwa na mipango mizuri ya fedha hapo baadaye..,siku zote Budget, income statement,statement of financial position,cashflow, hivi ndivyo vipimo muhimu za kazi mkurugenzi,katibu na meneja wa fedha yeyote duniani..,na sio ushabiki wa kisiasa na chadema

  Ndugu zangu ni aibu kuona chama tawala kikishindwa hata kulipa kodi kwenye baadhi ya mapango yake..,juzi tuliona ofisi ya CCM Ilala ikitimuliwa kwenye ofisi ya NHC kisa kodi,..na sio hapo tu ni Aibu paka sasa hv CHAMA tawala kutegema RUZUKU wakati kikiwa na rasilimali za kutosha kila mkoa..,kingeweza kutumia rasilimali hizo kuongeza mzunguko wa fedha kwa kuchukua mikopo benki na kuwekeza ili kuongeza pato la chama.

  Niwapongeze tu CCM kwa lile jengo la UVCCM ambalo ni juhudi za Mh. Edward Lowassa, sasa Mwigulu Vision yako ni nini...? kama katibu wa fedha....?

  Umeacha wajibu wako na kukimbili kwenye ushabiki wa kisiasa usio kuwa na tija kwa chama, kama kumvika mbwa bendera.., mimi siamini hizo ni kazi za katibu wa fedha..,kila siku kutukanana na Chadema mimi siamini hizo ni kazi za katibu wa fedha...,mimi naaamini CCM kila mtu ana wajibu na majukumu yake! lakini MH. naona umesahau wajibu wako ndani ya CHAMA...!

  Hilo zimwi la CHADEMA waachie wenzako Nape,Mukama na Lusinde...,ww fanya kazi yako kuhahakikisha Chama kinakuwa vizuri kiuchumi na Kifedha...,kwani pia ni sifa nzuri ya chama kuweza kuvutia wanachama zaidi na pia kukihakikishia chama kushika tena Dola
   
 2. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  yuko busy kwenda mbio na M4C wacha acheze samba zago
   
 3. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mwehu wa uchumi unamfundisha kuzingatia majukumu yake ha ha ha! unajambia mtoni wewe!
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Upumbavu mtupu, nendeni Moshi mkahesabiwe maana mmekuwa aido hapa town, huwezi kuandika usengerema wote huu halafu zote vepa.
   
 5. Masaningala

  Masaningala JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 539
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Huyo hata ubunge umemshinda. Ni mzigo na majuto kwa wanajimbo la Iramba Magharibi.
   
 6. K

  Kibagata JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 773
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  message sent, and derivered to mwigulu
   
 7. M

  Molemo JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Yuko busy kuvalisha mbwa bendera za CDM na kutengeneza Tshirts zinazopotosha maana ya M4C.Namtakia kila la kheri.
   
Loading...