Taarifa za ujenzi wa hizo zahanati zitolewe ili iwe ushuduma uwepo na walioko kule wathibitishe kujenga kwa hiyo miradi na siyo kutoa taarifa za jumla jumla inakuwa kama bosheni tu.

Wakati ule Umi akiwa waziri wa afya alisema wamejenga vituo vya afya vingi lakini watu wamekuwa wakijuuliza vimejengwa wapi? Maeneo gani Mbona havionekani?
 
Safi sana Mwigulu Nchemba na Rais Mama Samia Suluhu Hassan. Salute Kwenu Sisi wafanyakazi Tangu Uhuru Tunakatwa Kodi tuu na Atuna Pa Kukwepa...Mshahara Ukija Tayari ushakatwa Kodi juu jwa juu!

Afadhali mmekuwa Wabunifu MUNGU awabariki upande ambao sio wafanyakazi wanaumia Kawaida ya Msumeno ni kukata huku na Huku,Sio wengine walikuwa wanafurahia Jasho Letu,
Imagine Nakatwa kodi for 18yrs now!

Tena Direct Paye hapo bado sijanunua Bidhaa,
Acha wote tuchangie Maendeleo!
Ila kwenye Miamala Ondoeni hizo Tozo!
Imekalia sana Watu wa Chini tozo za Miamala na Kuwaumiza mnooo!ni Massive destruction.

Pili Kwenye Luku Pia Nawapa Kongole 12,000kwa Mwaka Safi haina Shida kama Ninejenga Nyumba ga 35,000,000
Kulipa Buku kika Mwezi Sio Issue.
MUNGU awabariki kwa mawazo mapya haya!
Tozo miamala ondoeni.
Haya Mengine tuko Pamoja Wafanyakazi Tunaendelea Kuchangia kodi na hawa wsngine nao wachangie,
Haina Shida tutakutana kwenye bidhaa pia tutanunua!
 
Mwigulu Nchemba ana kiburi kweli kauli zake utadhani analeta ligi na wananchi.
Mwigulu huyu ndiye yule aliyetoa lugha ya dharau wakati akisoma tozo wakati wa bajeti, alisema kwa jeuri eti anatuonea huruma watanzania kwa jinsi tutakavyo kamuliwa! Raha ya kutawala bila ya kutegemea kura.
 
Nakubaliana hapo kwenye leadership style sio lazima zifanane na there is no single approach of winning trust.

Isitoshe Magufuli zilipendwa ata iweje na Samia is entitled to steer the ship on her terms
Hoja yako nzuri kuna ya kuchukua na kuna ya kufikirisha.

Mama mi namwona tu kama caretaker president hadi 2025 tu. Baada ya hapo atulie zake astaafu kwa heshima awaachie wenye energy, wenye charisma, watu wanaoweza kucommunicate na kushawishi. Hapo tupo pamoja, lakini pia ieleweke hakuwahi kujiandaa kuwa president, ni president wa circumstances tu.

Ila kwangu naona katika kipindi hiki cha mpito tuna wajibu wa kusaidia jahazi lisizame kwa kumsaidia mambo yaende. Falsafa ya tozo haina shida hata kidogo. Shida ije kwenye coordination za hizo tozo na matumizi ya hizo tozo. Kwa mfano what the hell are ewura doing kwenye muamala wa tanesco? Mimi kwanza nina ishu na maagency kibao ya serikali yaliyopo tu kinyonyaji. Yanachojua ni kwenda mtaani kunyonya hela za watu tu, tija za uwepo wake haupo kabisa.

Kuhusu hierarchy of needs za watu wetu mimi naona sometimes huwa tunaentertain na kuhurumia upuuzi bila sababu zozote za msingi. Watu wa nchi si kwamba ni maskini in a real sense. Ni just wapuuzi na baadhi ya upuuzi ni kutokana na tamaduni za asili zinazowafanya waonekane maskini kumbe siyo maskini.

Chukulia mfano mmasai na ng'ombe zake 300 lakini hataki kumpeleka mtoto shule. Huyo ni maskini? Huyo anashindwa kuchangia ujenzi wa shule kupitia kodi au tozo? Sometimes serikali inabidi kutumia brutal force, top down algorithms ili kufanya huduma za msingi zipatikane hata kama watu hawaperceive hizo huduma kama basic needs. Leo hii kuna shule kibao umasaini na zote zimelazimika kuwa boarding ili kubypass culture ya kimasai isiyokuwa favourable kwa mtoto kwenda shule na isiyofavour wanafunzi wa kutwa.

Nafikiri pia in your mind unawahurumia akina mama na wazee na watu wengi tu ambao kiukweli ni ndugu zetu wa vijijini na hata mjini ambao ni maskini kweli kweli. Yes, kama ni maskini kweli kweli hawezi kufikiwa na hiyo miamala (maana hata simu hana, haweki vocha, hawezi kupokea mpesa wala airtel money, na hawezi kutuma pia, nyumba haina umeme wala maji mtiririko vitakavyohitaji afanye transactions kupata hizo huduma).

How do you help such people? Ni kuwapelekea miundo mbinu wezeshi kama barabara za lami vijijini, maji tiririka vijijini na umeme vijijini, na shule vijijini na huduma za afya vijijini). Uwepo wa hizo huduma kote kote ndio ukombozi wa kweli wa mtu maskini. Kama Mwigulu alivyosema katika hayo mambo ya msingi hatutakuwa na debate. Debate iwe je kama tutatozana kufika huko ni vibaya? Na kama tutatozana njia gani bora? Njia za zamani za kuwaroza watu wachache doesn't seem to work. Kuna wakati police traffic waligeuka kufanya kazi ya TRA wakapewa hadi lengo la kutimiza kila mwaka na mlipiga mayowe, hata mimi niliyapiga maana si kazi ya police kutafutiza faini.

Katika kufikia hayo malengo mujarabu mzigo usipokuwa distributed kwa wananchi wote utawaelemea watu wachache. Na si afya nchi kujengwa na watu wachache, hilo tulikwepe kwa namna zote.
 
Mwenye ufahamu wa kiasi cha pesa kinachotumwa/kupokelewa kwa mwezi kwenye mtandao ya simu atuwekee hapa ili tuujue ukweli au uongo wa Madelu kuweza kutukamua 48bn. ndani ya siku 45
 
Inaweza kua kweli ila bado tozo hizo zitabaki kua za dhuluma, kuna mianya mingi ya kukusanya mabilioni yakodi halali ila uzembe wa serikali unasababisha wananchi wakamuliwe.

Mfano mdogo kodi tunayopaswa kulipa baada ya manunuzi ya bidhaa inapotea kwa sababu wafanyabaishara hawapendi kutoa rrisit, hapa serikali ingekuwa na wafanyabaishara kuwaeleza kwa kua hawapendi kutoa risiti basi kodi hiyo wawe wanailipa moja kwa moja wao ili wasiikoseshe serikali mapato.
 
Mzee wa fiksi!Inept.

Period.
Acv3MT.jpg
 
Ukifanya simple mathematics, utabaini hicho kiasi ni kidogo au huenda nyingine zinajenga mansion binafsi. Tuwe wazalendo, Tulipe kodi.
 
Hamna kitu hapo idadi za watumia mtandao wa simu means SMS,internet, kutuma /kutoa pesa ,kupiga simu kwa dk 1tu kwa mfano piga idadi ya watu million 30+(watumiaji wa internet tu kwa mujibu wa Tcra) piga Mara kwa idadi ndogo ya hela ya Tsh 500/1000 utapata Jibu hio ni kwa sekunde ,piga sasa Mara dk in sh ngapi ,uje kwa mara Massa njoo kwa siku ,wiki then kwa mwezi hiyo hela ni ndogo sana.
 
Hamna kitu hapo idadi za watumia mtandao wa simu means SMS,internet, kutuma /kutoa pesa ,kupiga simu kwa dk 1tu kwa mfano piga idadi ya watu million 30+(watumiaji wa internet tu kwa mujibu wa Tcra) piga Mara kwa idadi ndogo ya hela ya Tsh 500/1000 utapata Jibu hio ni kwa sekunde ,piga sasa Mara dk in sh ngapi ,uje kwa mara Massa njoo kwa siku ,wiki then kwa mwezi hiyo hela ni ndogo sana.
Duh mkuu hii inahusiana na miamala tu mbona umeupiga mwing mpaka umepaisha?
 
Wananchi wanalaumiwa kwa kushangilia watu fulani fulani wakitwaliwa na iziraili lakini saa nyingine naona ni sawa tu wananchi kushangilia mauti yao kama yule ambaye iziraili alimpangia ratiba yake ya roho kutwaliwa iwe March.
 
Sio kweli basi hayo makampuni yangekua na hela za hatari wao walikua na fungu la kujenga hizo zahanati na shule kutegemea hizo Tozo ndio zutarudisha hiyo pesa...wanatuona makoro sana hawa..
 
Sio kweli basi hayo makampuni yangekua na hela za hatari wao walikua na fungu la kujenga hizo zahanati na shule kutegemea hizo Tozo ndio zutarudisha hiyo pesa...wanatuona makoro sana hawa..
Pesa zinazotumwa kupitia kwenye mitandao ya simu hazifiki bn12 kwa mwezi. Sasa tozo ambayo haizidi 2% inawezaje kuzidi kiasi kilichotumwa?
 
Naona serikali imeridhika na tozo na imesahau traditional revenue toka kwenye biashara mijini, Ukienda dukani unaelezwa tukupe risiti ya kusafiria au tukupe ya TRA tumerudi kule kule. Mambo yote tozo cheap to collect while they are in the offices. TRA amkeni tumerudi kule kule kuweni macho mngekusanya more and more especially sasa hivi biashara zimechangamka kidogo.
 
Back
Top Bottom