Mwigulu Nchemba ni vyema akajikita kwenye kuboresha magereza na haki za wafungwa!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
187,488
2,000
Mwigulu Nchemba anapwaya na hata majukumu yake hayaelewi.

Kauli zake ni kama mcee haonyeshi utashi, uzoefu au maarifa ya kuisimamia wizara nyeti kama hii.

Huko Kibiti anasoma siasa wakati kuna kero za msingi za kutatuliwa. Kifupi hana mkakati.

Kazi ambayo angejikita nayo maana hizo nyingine hawezi ni kupigania kuboresha haki za wafungwa ambazo zinaporwa kila kukicha.

Rumande ziwe na vyoo vya kuflash na ukomo wa idadi kwa kila chumba, lishe bora na viwepo vitanda vya kulala na mwanga wa kutosha.

Wafungwa wawe na vitanda kila mmoja, lishe bora, vyoo vya kuflash, kila chumba wasizidi wafungwa 12.

Vifungo vya nje na faini badala ya vifungo kupunguza msongamano kwenye jela.

Nchi isiyoheshimu haki za wafungwa haiwezi kuendelea.

Hayo anaweza kufanikisha na kujipangusa maeneo mengi aliyoonyesha udhaifu

Vinginevyo just resign and go home because you are useless!
 

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,857
2,000
Mwigulu anapwaya sana katika hiyo nafasi. Sikujua kama jamaa uwezo wake ni mdogo kiasi hiki
 

Nginana

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
835
1,000
Kama wiki tatu zilizopita kuna mwandishi wa BBC Swahili alitembelea hayo maeneo ya Kibiti/Rufiji na katika ripoti yake alisema chanzo hasa cha mauaji ni migogoro ya ardhi.

Tangu miaka ya 70 Mamlaka ya Bonde la mto Rufiji (Rubada) ilikuwa inaratibu ugawaji wa ardhi kwenye hayo maeneo kwa 'wawekezaji".

Baada ya kupitishwa kwa sheria ya ardhi ya vijiji, jukumu la udhibitii wa ardhi lilihamia kwa serikali za vijiji na Rubada ikabaki kuwa kama taasisi ya madalali tu wa ardhi ya bonde la mto Rufiji.

Kutokana na rushwa na kutokuzingatiwa kwa sheria, kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za ugawaji wa ardhi kwa 'wawekezaji' inazofanywa na viongozi wa vijiji.

Mathalan, kwa mujibu wa sheria, eneo la ardhi ya kijiji lililotengwa kwa ajili ya wawekezaji halipaswi kuzidi asilimia 25 ya eneo lote la kijiji. Lakini cha kushangaza ni kwamba katika maeneo ya Kibiti na Rufiji kuna vijiji 'vimeuza' kifisadi zaidi ya 75% ya maeneo yao kwa 'wawekezaji'.

Kwa vile idadi ya watu inaongezeka kwa kasi ni dhahiri kuwa haya ni mazingira yanayokaribisha shari. Na ndicho kinachotokea.

Hili ni suala ambalo Mwingulu analifahamu fika ila kwa vile yeye ni mwanasiasa anayeendesha siasa kwa misingi ya malumbano yasiyo na tija pamoja na vijembe, hatafanya lolote na mauaji ya wananchi yataendelea.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom