Mwigulu Nchemba ni mtoto wa mkulima kweli! Kwanini aipende CCM hivi?

Historia ya Mwigulu haina tofauti na Watanzania wengi katika legacy ya Mwalimu Nyerere ilikuwa ina wezekana mtu from no where na kuingia kwenye systeam lakini kwa sasa ni ngumu sana.
 
Usanii mtupu! Amepigia picha hapo kudanganya watu! Yes hapo yawezakuwa hapo ndo origin yake,cha kuangalia hapa ni kwamba yeye kama Mwigulu kafikaje hapo alipo? Katokea BOT na pale ndo EPA ilitokea! Jamaa anataka kutudanganya hakuwa na pesa ni usanii tu,jamaa alikuwa na cash ya kutosha kabisa na wala asitutanie!
 
Duh wameweka kakipande kale aliwachachafya wapinzani na ''bajeti mbadala'' bungeni. ha ha haaaaa
 
sijaona mantiki ya hali ya maisha na kwa mfuasi wa chama fulani.
 
Mwigulu anasema CHADEMA inaeneza siasa za chuki! Hivi huyu jamaa anaakiri kweli? Anataka CHADEMA ifike jimboni kwake waanze kusifia CCM jamaa hamnazo,eti CHADEMA inachonganisha wananchi kwa kusema CCM ni wezi! Kwani hapa kipya ni kipi na nani asiejua hilo?

Nakuwa na wasiwasi kamj huyu mwanasiasa wetu kaiva! Ushauri wa bure kwa Nchemba ni kuwa magamba wap4e kazi kwa spidi ya rocket ili watz wawakubali na si kulalamika tu km wanavofanya sasa!
 
Mwalimu wa Mwigulu anakumbukumbu kweli story aliyosimulia Mwigulu naye kasimulia hiyo hiyo. dah mwalimu kiboko
 
*Kuzaliwa na mkulima(maskini) hakukufanyi na wewe kuwa mkulima(maskini).
Ni kwenye ufalme tu ambako mtoto mzaliwa ana uhakika naye kuja kuwa mfalme pia.

*Watu wanaotumia logic hii kama Pinda na Mwigulu ni wanasiasa wanaotafuta cheap popularity katika siasa yaani watu wawaonee huruma au wawaamini kuwa wao ni waaminifu.

*Bahati mbaya kuna watanzania wengi wanaamini mtu kuwa maskini basi ni kielelezo cha kuwa mwaminifu which is not true.

Swali kuu ni: Is Mwiguru peasant?
 
Kuweni waungwana, upinzani si kupinga yote yanayofanywa na mpinzani wako.
Hicho kipindi kina mambo mengi yanayoweza kumu-inspire mtu mbali ya kuona usisiem na uchadema.
Acheni unafiki(mnajijua).
 
Kama utachunguza vizuri utagundua kuwa Mwigulu sio mwanasiasa mzuri.
Kivipi? Zile sifa kuu za kuwa mwanasiasa mzuri hana, kwa mfano
1/Uwezo wa kujenga hoja

2/Mwonekano wa kisiasa(Political Icon)

3/Nguvu ya Ushawishi(Convincing power)
 
- Ok Muumini wa CCM anatakiwa kuwa wa namna gani na na wa chama chenu Chadema namna ipi? Hebu funguka hapo kwanza hapo tuwekane sawa!!

Le Mutuz!

anatakiwa awe kama wewe uliepata zero form four afu saizi una degree.
Anatakiwa awe kama wewe unaeishi kwa baba na kula na kulala bure huku ukiwa na miaka 54
 
kuna siku za nyuma kuna thread ilikuwa inaelezea ufisadi wa nchemba tokea alipokuwa mazengo na hata kuchukua mke wa mtu kule tabora naomba atukumbushe tulinganishe na tuliyosikia leo
 
Jamaa nilimsikiliza sana, kwa uweli siasa hazimfai Mwigulu, ila katika watu tunaowaita Wafurumiti /wapiganaji, kajitahidi, manake mazingiza yale, dah anastahili sifa, manake alijitahidi sana darasani, kuliko waleo waliokuwa na fursa na access ya elimu!
 
Ana akili za ovyo mno na hata ukimuuliza kwanini ng'ombe wa babake wamekondeana vile pamoja na yeye kusoma shule. Wala hana majibu ya kwanini hali ya maisha ya ndugu zake pale jimboni ni duni vile hata baada ya ccm kuwepo madarakani. Kumbe hajaelimika. Mtangazaji alijaribu sana kumpa maswali ya kumjenga , lakini imegoma kwani watu wale ni maskini kupindukia. Kumbe kiswahili alianza kukifahamu na kuzungumza alipoingia shuleni, mmmmmmmmmmmmmm, poleee.
 
Back
Top Bottom