Mwigulu nchemba: Nemeuza vx v8 yangu kununua motor za maji (jamaa kweli tatizo)

Hakika mh. Mwigulu amekuwa mfano wa kuigwa baada ya kusema bungeni kuwa ilimlazimu kuuza gari yake aina ya vx v8 na kununua pampu ya maji kwa ajili ya wananchi wa jimbo lake.

Ameyasema hayo wakati wa kuchangia bajeti ya maji.
Hebu tujiulize ni wabunge wangapi wenye moyo wa kuuza magari yao na kuhudumia wananchi wao.

Hakika ni wachache tena sana na kwa hili mwigulu unastahili pongezi. Wana iramba tumepata jembe.!!!!!!!!!!!!!

hapo kwenye nyekundu alimesema aliuza gari yake VX V8 kwa ajili ya kununua Pampu ya Maji, nilipo bold kwa blue anasema alinunuaa Pampu ya maji ina maana pampu ya maji ni sawa na hilo V8 lake mbona jamaa muongo?
 
Mwigulu mnafiki kama kweli anauchungu na maisha ya mtanzania kwa nini asipeleke hoja bungeni kupinga serikari kununua ma v8 ili pesa ziende kwenye miradi mhimu ya wananchi, akiwekea mfano uamuzi wake.?
 
Wakauze Ma Vx V8 yote ya wizara na maofisi mbvalimbali ili kununua hizo pampu na T-Scan machines wanazolilia madokta kila kukicha.

"Liwalo na Liwe" wakati anaapishwa kuwa PM alikataa katakata kutumia hizo Vx kwa kubana matumizi, but cha ajabu eti akadai "labda apewe mwingine"
.
 
FJM,
Hivi mzee Ndesamburo anavyojenga visima kwa pesa yake binafsi unaweza kweli kusema ni upuuzi?

Mzee Ndesamburo aliunga mkono wale wale waliotaka serikali itenge fedha za miradi ya maendeleo kama inayoelekezwa kwenye mpango wa Maendeleo wa miaka 5. Soma vizuri nilichoandika, lakini pia rejea mjadala wa bunge wakati wa bajeti ya serikali. Specifiacally rejea mchango wa Mwigulu kuhusu serikali kutakiwa kutenga fedha 35% kila mwaka.

Huko tuendako, ningependa kuona sheria inapitishwa bungeni kukataza wabunge kutumia fedha zao kufadhili miradi kwenye majimbo ya uchaguzi. That's institutional corruption. Hela za miradi zipo, tena nyingi sana. Lakini kwa sababu wabunge wamejikita kwenye mipasho serikali inafanya inavyotaka na ndio maana wamenunua magari yenye thaman ya Tsh 5 trillion! Na hapo ni magari peke yake, nenda kwenye posho, safari, vitafunwa, sherehe za kitaifa, mwenge wa uhuru (!), maua maofisini, Computer (hazina), furnitures etc.

Kama wabunge wangekuwa makini tatizo la maji lisingekuwepo kabisa Tanzania. Just imagine Tsh 5 zingefanya nini? Hapo kwa Kagame wakubwa wanatembelea magari ya kawaida kabisa, lakini hapa bongo wakubwa bado wanaishi kama Hollywood stars.
 
Mwigulu anapenda sana sifa!!!! Kauli yake inatia shaka, hebu atueleze VX hilo alilouza je ni lile alilokopeshwa baada ya kupata ubunge? Je amemaliza kulilipia mkopo?
 
Hakika mh. Mwigulu amekuwa mfano wa kuigwa baada ya kusema bungeni kuwa ilimlazimu kuuza gari yake aina ya vx v8 na kununua pampu ya maji kwa ajili ya wananchi wa jimbo lake.

Ameyasema hayo wakati wa kuchangia bajeti ya maji.
Hebu tujiulize ni wabunge wangapi wenye moyo wa kuuza magari yao na kuhudumia wananchi wao.

Hakika ni wachache tena sana na kwa hili mwigulu unastahili pongezi. Wana iramba tumepata jembe.!!!!!!!!!!!!!

Nchemba ??????????????????? Mr masifa saeting allowance je?????????????????????.ngojeni hili jembe linamagego
 
Akauze na masaburi, si anadai serikali yake ni sikivu ikafanye hiyo kazi au pesa amepewa mkulu akajisafishe.
 
Nchemba anasema ameuza vx v8 lake kununua motor za maji kwenye vijiji kama kumi hivi! Then anasema leo

'sijapandisha jazba maana naongea mambo ya msingi'. Kisha anamkumbusha spika kuwa 'siku saba' zimepita kwa

ule ushahidi wa Mnyika!

Kumbe,

1. Kama Vx V8 moja linanunua motor kwa zaidi ya vijiji kumi, je yakiuzwa mia?

2. Kumbe Mwigulu kwa akili zake huwa anaamua kupandisha jabza akiwa anaongea mambo yasiyo ya msingi.

Hii ndio akili ya CCM!

katika siku nimecheka leo nimecheka sana dah!
 
Back
Top Bottom