Mwigulu Nchemba: "Napendekeza kupunguza adhabu kwa makosa ya pikipiki na bajaji lengo ni kuweka adhabu kwa kuzingatia uwezo wa kulipa"

Hahahahaaa mkuu, hao jamaa niliowa-tag sijafanya hivyo kuwa kupenda ila nimelazimika kwa maana walinikejeli sana siku nilipoandika humu kuwa tozo zinapaswa kuendana na uzito wa kosa.

Kosa la bajaj sio sawa na la mwenye lorry.
Wakati ni hakimu wa haki
 
Nadhani lengo la faini sio mtu kulipa au kushindwa kulipa, lengo lake ni kuzuia mtu asifanye au kurudia kosa. Kuweka faini ndogo wakati mwingine inawaweza kuhamasisha mtu kufanya makosa kirahisi akijua uwezo wa kulipa anao.
 
Uzito wa kosa...mfano bajaj kapita taa nyekundu na mimi na Vitz nimepita taa nyekundu, kosa si lile lile? Inakuwaje huyu alipe 10,000 na yule 30,000?! Bodaboda na bajaj pamoja na faini 30,000 ndio wavunja sheria wakuu sasa kuwapunguzia hadi 10,000 si ndio watatumaliza?!!
Hata mm nimelishangaa hili
 
Ndio maana tunabambikiziwa ili kutunisha mapato
Kuna police traffic mmoja aliwahi kunipiga fine 60,000/= eti nina makosa mawili. Hivi kwa hizi gari seconda hand za Japan, unaweza usiwe na kosa? Magari yenyewe mabovu yanaweza kuwa na makosa hata 20, lakini busara lazima itumike na alipaswa kuandika kosa moja tu 30,000/= baaas.
 
Ngoja wataalamu wa falsafa ya adhabu jinai waje kutujuza, kuongeza au kupunguza adhabu ni kipi kinapunguza matokeo ya uhalifu? Hapa serikali imeangalia hoja ya kiuchumi (uhimili wa fine) affordability peke yak
Hapo serekali imesha liangalia hilo jambo kisawasawa, maana bila shaka sasa serekali itaona pesa za boda boda
 
Kuna police traffic mmoja aliwahi kunipiga fine 60,000/= eti nina makosa mawili. Hivi kwa hizi gari seconda hand za Japan, unaweza usiwe na kosa? Magari yenyewe mabovu yanaweza kuwa na makosa hata 20, lakini busara lazima itumike na alipaswa kuandika kosa moja tu 30,000/= baaas.
Tukio lilitokea wapi?Ila pole sana
 
Back
Top Bottom