maulaga
JF-Expert Member
- Feb 22, 2009
- 472
- 120
Magazeti ya UHURU na Mwananchi leo tarehe 14/9/2011 ya mebeba tuhuma nzito zilizotolewa na mweka hazina wa CCM Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mbunge wa moja ya jimbo mkoani Singida, kwamba CHADEMA wamepeleka vikundi vya kigaidi huko Igunga vikiwemo vikundi kutoka nje ya nchi.
Tuhuma hizo ni nzito na hazipaswi kupuuzwa. Je, Nchemba anataka kutuambia serikali na vyombo vya usalama ni butu kiasi hicho? Ameamua kuidharirisha serikali inayoongozwa na chama chake kwa nia ya kupata kuungwa mkono na wapiga kura wa Igunga?
Kama msomi alipaswa kujua athari ya kauri anazotoa ambazo kwa dhahiri zinaidharirisha serikali yake. Vinginevyo serikali itoe maelezo dhidi ya ugoigoi unaoelezwa na Nchemba dhidi yake.
Haiingii akilini chama cha siasa kiingize magaidi kutoka nje ya nchi wakae Igunga serikali isiwe na habari mpaka mweka hazina wa CCM atoe taarifa kwa vyombo vya habari.
Serikali hiyo inapaswa iondolewe madarakani kwa kushindwa kulinda usalama wa nchi.