Mwigulu Nchemba na Tuhuma za Ugaidi wa CHADEMA

maulaga

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
472
120
Magazeti ya UHURU na Mwananchi leo tarehe 14/9/2011 ya mebeba tuhuma nzito zilizotolewa na mweka hazina wa CCM Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mbunge wa moja ya jimbo mkoani Singida, kwamba CHADEMA wamepeleka vikundi vya kigaidi huko Igunga vikiwemo vikundi kutoka nje ya nchi.

Tuhuma hizo ni nzito na hazipaswi kupuuzwa. Je, Nchemba anataka kutuambia serikali na vyombo vya usalama ni butu kiasi hicho? Ameamua kuidharirisha serikali inayoongozwa na chama chake kwa nia ya kupata kuungwa mkono na wapiga kura wa Igunga?

Kama msomi alipaswa kujua athari ya kauri anazotoa ambazo kwa dhahiri zinaidharirisha serikali yake. Vinginevyo serikali itoe maelezo dhidi ya ugoigoi unaoelezwa na Nchemba dhidi yake.

Haiingii akilini chama cha siasa kiingize magaidi kutoka nje ya nchi wakae Igunga serikali isiwe na habari mpaka mweka hazina wa CCM atoe taarifa kwa vyombo vya habari.

Serikali hiyo inapaswa iondolewe madarakani kwa kushindwa kulinda usalama wa nchi.
 
Kila uchaguzi Tanzania una vituko vyake. Wenye nguvu hutumia nguvu zao kuumiza wanyonge. Misingi ya haki na utawala wa sheria haipo kabisa kwenye ardhi ya Tanzania. Tukio la kumwagiwa mtu tindikali halihitaji siasa linahitaji sheria, sasa kama mbunge ana ushahidi halafu anaendeleza uvuvuzela je mwendesha mkomkoteni afanyeje?? Kwa watu wanaothamini utu wa mwanadamu hawawezi kuendelea kupiga domo wakati wahalifu wana wajua si wakamatwe mbona mpaka leo ni kelele tu.

Kama mbunge au waziri ana weza kumchapa mtu vibao na polisi, wananchi wakaona ni sawa ( Ngeleja na mlinzi wa ATM0) Mudhihiri na Asha baraka) Mkuu wa wilaya na waalimu nk na hakuna sheria zilizofuatwa haitakuwa tabu kwa mwananchi kudhuriwa na wabunge kuendeleza siasa.

Serikali ya CCM imechoka kuwafanya watawala wake kutimiza wajibu wao ndio maana kila mmoja analalamika hata ajali ya meli ya Nungwi kila mtu anajifanya hajui, tubadilike tuanze kuchukua hatua. Kama Mweka hazina wa CCM na mbunge wa singida anawajua walomfanyia kitendo cha kinyama mwananchi yule awataje na wafikishwe mbele ya hseria.

CDM hawawezi kufanya unyama na kama kweli wangekuwa wao leo viongozi wote wa CDM wangekuwa jela kwa jinsi serikali ya CCM ninavyoijua, CCM wamemmwagia kijana wa watu tindikali ili wapate ground ya kisiasa huu ni unyama mkubwa sana na siasa hatarishi.
 
Magazeti ya UHURU na Mwananchi leo tarehe 14/9/2011 ya mebeba tuhuma nzito zilizotolewa na mweka hazina wa CCM Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mbunge wa moja ya jimbo mkoani Singida, kwamba CHADEMA wamepeleka vikundi vya kigaidi huko Igunga vikiwemo vikundi kutoka nje ya nchi.

Tuhuma hizo ni nzito na hazipaswi kupuuzwa. Je, Nchemba anataka kutuambia serikali na vyombo vya usalama ni butu kiasi hicho? Ameamua kuidharirisha serikali inayoongozwa na chama chake kwa nia ya kupata kuungwa mkono na wapiga kura wa Igunga?

Kama msomi alipaswa kujua athari ya kauri anazotoa ambazo kwa dhahiri zinaidharirisha serikali yake. Vinginevyo serikali itoe maelezo dhidi ya ugoigoi unaoelezwa na Nchemba dhidi yake.

Haiingii akilini chama cha siasa kiingize magaidi kutoka nje ya nchi wakae Igunga serikali isiwe na habari mpaka mweka hazina wa CCM atoe taarifa kwa vyombo vya habari.

Serikali hiyo inapaswa iondolewe madarakani kwa kushindwa kulinda usalama wa nchi.
Kuna watu wanaropoka maneno kabla hawajatathmini athali za maneno yao.......... Hao wote ni wale wale............. Hebu angali haya maneno.........
1. Wivu wa kike.............. Akaomba radhi ........na baadaye wivu wa kijinga
2. Vijisenti.......... akimaanisha bilioni.......... wakati wengine mlo wa dakika moja ijayo hana uhakika nao.................
3. Chama cha wachaga.................... Anasahau kuwa anahusisha ukabila kwenye siasa..................
4. Wanafikiri kwa makalio.................
5. Watanzania mna wivu wa kijinga kwa wawekezaji....................
6. .............etc...........etc
 
na yeye pia ni gaidi...alijuaje kuwa kuna magaidi kama yeye pia sio gaidi?? aache kuota mchana kweupe, ya tindikali imagoma sasa wanakuja na jingine.....................
 
Ntarahamwe wapo Tanzania tena kwenye kampeni za Igunga na usalama wa Taifa wapo Igunga. Kweli Tanzania sio nchi bali mtaa kwenye sayari.
 
Tumeishawazoea hawa magamba maji yakiwafika shingoni lazima waje na tuhuma, hasa za kighaidi. Kuna wakati IGP Mahita alionyesha visu vyenye rangi ya CUF siku moja kabla ya uchaguzi akidai vimeingizwa nchini kuvuruga uchaguzi wa Zanzibar, kumbe wamavitengeneza wenyewe...
Ishu sasa imejirudia tena, wamemsacrifice mwenzao kwa kummwagia tindikali ili wasingizie ni CDM.

CCM ndio magaidi hapa nchini linapokuja suala la ucnaguzi. Hapa ukiwauliza vyombo vya usalamo viko wapi nao watakuuliza vyombo vya usalama vilikuwa wapi hadi meli ya watu 610 ikabeba abiria 2,610? Utabaki kujiumauma wao wanachukua point kisingizio vyombo vyote vya serikali legelege ya awamu ya nne ni legelege...

Hawa jamaa ni wajanja mno, na huenda wao ndio wamewaleta hao vijana na kuwapa hela, Tshirts na Kofia za CDM, na hata Kadi feki kama za wale waliorudisha jumamosi. Linapokuja suala la ushindi ni lazima hawa jamaa magamba ni maghaidi kwelikweli. Ni suala la wanaIgunga kuwa makini na kuwapuuza.
 
Haya maneno yanaweza kuwa na ukweli tusiyapuuze!!

Pamoja na tofauti zetu za kisiasa naomba tufikiri kidogo. Kuna majasusi na Ntarahamwe Igunga wameingizwa na chama cha siasa tena cha upinzani, mbunge wa chama tawala anawajua ila vyombo vya usalama vya serikali ya chama tawala bado haijawakamata.

Kumbuka hawa kwanza wapo nchini kinyume cha sheria ni magaidi na wanataka kuvunja sheria kwa kuuwa au kudhuru wananchi, mbunge anafahamu hili wakati jeshi la polisi, usalama wa taifa, cid hawajui. Kweli tunanchi hapa? usalama wetu uko wapi? Kwa nini Nchemba asikabidhiwe idara ya usalama wa taifa na polisi????
 
Hawa watakuwa wamevukishiwa kupitia Arusha au moshi, itakuwa Lema ndio muhusika mkuu kwasababu anazijua vizuri njia za panya alizo kuwa akizitumia kwenye biashara ya wizi wa magari.

WanaCDM wamesha igeuza hii stori kuwa ni uzembe wa jeshi wakisahau tuhuma hiyo inawahusu wao kuleta majambazi nchini.
 
Utawala unao anguka huwa unakuwa na dalili za kuporomoka zinazoendana na vituko vya kijinga. Hivi huyu Mchamba kwa akili zake anataka kutuambia nini wananchi kuhusiana na usalama wetu.
Jeshi la polisi wangekuwa hawatumiwi na ccm walitakiwa wamkamate ili asaidie kutoa ushahidi.
 
Serikali hii, pamoja na udhaifu wake, inapaswa kuchukua hatua haraka. Nasikitishwa na jinsi jeshi la polisi na vyombo vya usalama vinavyokaa kimya bila kukemea uchochezi huu wa wazi unaofanywa na ccm.

Ni hatari sana kwa chama kuandaa vijana "GREEN GUARDS" eti wanawafundisha ukakamavu na moyo wa kujitolea na kulinda kura za ccm. Mwigulu amekiri jana katika press conference kuwapo kwa kundi hilo na kujaribu kuhalalisha mafunzo wanayowapa.

Tunajua kuwa vijana hawa wanaandaliwa kufanya fujo, na wamewahi kufanya fujo huko nyuma. Tunaelekea wapi?

Kwanini wawafundishe wakati wa uchaguzi pekee? Hii ni hatari, na ni dalili mbaya kwa taifa.
 
Magazeti ya UHURU na Mwananchi leo tarehe 14/9/2011 ya mebeba tuhuma nzito zilizotolewa na mweka hazina wa CCM Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mbunge wa moja ya jimbo mkoani Singida, kwamba CHADEMA wamepeleka vikundi vya kigaidi huko Igunga vikiwemo vikundi kutoka nje ya nchi.

Tuhuma hizo ni nzito na hazipaswi kupuuzwa. Je, Nchemba anataka kutuambia serikali na vyombo vya usalama ni butu kiasi hicho? Ameamua kuidharirisha serikali inayoongozwa na chama chake kwa nia ya kupata kuungwa mkono na wapiga kura wa Igunga?

Kama msomi alipaswa kujua athari ya kauri anazotoa ambazo kwa dhahiri zinaidharirisha serikali yake. Vinginevyo serikali itoe maelezo dhidi ya ugoigoi unaoelezwa na Nchemba dhidi yake.

Haiingii akilini chama cha siasa kiingize magaidi kutoka nje ya nchi wakae Igunga serikali isiwe na habari mpaka mweka hazina wa CCM atoe taarifa kwa vyombo vya habari.

Serikali hiyo inapaswa iondolewe madarakani kwa kushindwa kulinda usalama wa nchi.

Hii si habari mpya kusikika toka kwa wanamagamba wanapokuwa wamebanwa kila kona.

Kwa mnaokumbuka vizuri, uchaguzi mdogo wa tarime baada ya kifo cha Chacha Wangwe, wanamagamba walilipuka na tuhuma kama hizi. Walidai kwamba chadema imeingiza nchini vijana wa Mungiki kutoka Kenya. Pamoja na propaganda hiyo mwisho wake mgombea udiwani wa tarime mjini Peter zakaria ndiye alikamatwa na polisi akiwa amejaza silaha kwenye gari yake akizivusha kuja tarime toka kenya.

Kwahiyo kwa mwenendo huu nina kila sababu ya kuamini kwamba magamba watakuwa wamepeleka "magaidi" huko igunga kwahiyo wanajaribu kuweka mazingira ya kuwatumia kufanya kila aina ya uhalifu huku wakiisingizia chadema ili wapate nafasi ya kuchakachua. Bahati mbaya sana kwao mwaka huu igunga hawachakachui, mshindi ni yule atakayekuwa amechaguliwa na wanaigunga wenyewe, hakuna mteule wa NEC wala nini!!
 
CCM wako tayari kupoteza huai wa mtu ili uwemtaji wao!rejea uchaguzi mkuu walivyomuonga aliyekuwa mme wa Josephine amshitaki Slaa kuwa kampokonya mke wakati walikuwa wameachana kabla na Wananchi walipolipuuza hilo wakaunda njama kumuua yule jamaa ionekane Slaa kaua mtu aliyemshitaki!jamaa kaandaliwa gari kubwa likamgonga akiwa ktk gari lake dogo Mungu mkubwa kapona ila gari halikutamanika!watashindwa kummwagia mtu tindikali aliyekuwa anawabandikia mabango ili waseme chadema?CCM ni chama pekee kilicho na jeshi lake blueguard sijui kama sheria za nchi zinaruhusu ama vipi!
 
Haya maneno yanaweza kuwa na ukweli tusiyapuuze!!
<br />
<br />
unajuwa kama ungekuwa na akil timam uwez kukurupuka kuchangia ktk thread.jiulize tangu lini mgen akawa na nguvu kuliko mwenyej kama ao vijana ni wagen wakamatwe na waojiwe! Na hiyo kambi ya cdm iko wapi wanapopatiwa mafunzo hao vijana,ila magamba wao tangu long time wana vijana.intelejensia wanafanya kaz gani.mbinu za magamba ni zakigaidi sana
 
Kuna watu wanaropoka maneno kabla hawajatathmini athali za maneno yao.......... Hao wote ni wale wale............. Hebu angali haya maneno.........
1. Wivu wa kike.............. Akaomba radhi ........na baadaye wivu wa kijinga
2. Vijisenti.......... akimaanisha bilioni.......... wakati wengine mlo wa dakika moja ijayo hana uhakika nao.................
3. Chama cha wachaga.................... Anasahau kuwa anahusisha ukabila kwenye siasa..................
4. Wanafikiri kwa makalio.................
5. Watanzania mna wivu wa kijinga kwa wawekezaji....................
6. .............etc...........etc
Kaka matusi tumeyazoea, umesahau hii " Hat mkila majani ndege ya rais lazima inunuliwe, mnataka rais wetu abebwe na punda?"
 
magazeti ya uhuru na mwananchi leo tarehe 14/9/2011 ya mebeba tuhuma nzito zilizotolewa na mweka hazina wa ccm mwigulu nchemba ambaye pia ni mbunge wa moja ya jimbo mkoani singida, kwamba chadema wamepeleka vikundi vya kigaidi huko igunga vikiwemo vikundi kutoka nje ya nchi.

Tuhuma hizo ni nzito na hazipaswi kupuuzwa. Je, nchemba anataka kutuambia serikali na vyombo vya usalama ni butu kiasi hicho? Ameamua kuidharirisha serikali inayoongozwa na chama chake kwa nia ya kupata kuungwa mkono na wapiga kura wa igunga?

Kama msomi alipaswa kujua athari ya kauri anazotoa ambazo kwa dhahiri zinaidharirisha serikali yake. Vinginevyo serikali itoe maelezo dhidi ya ugoigoi unaoelezwa na nchemba dhidi yake.

Haiingii akilini chama cha siasa kiingize magaidi kutoka nje ya nchi wakae igunga serikali isiwe na habari mpaka mweka hazina wa ccm atoe taarifa kwa vyombo vya habari.

Serikali hiyo inapaswa iondolewe madarakani kwa kushindwa kulinda usalama wa nchi.

gazeti la mwananchi tarehe 13.09.2011, limeriport kwa head "chadema chaigeuzia kibao ccm". Content yake inadai kuwa chadema wanaituhumu ccm kwa ".......kuandaa kambi za vijana mahususi kwa ajili ya kufanya vitendo vya kijasusi ikiwemo kuwamwagia tindikali wafuasi wa vyama vingine".

Pia chadema wanadai kuwa, ".....ccm wamekodisha kikundi cha vijana 20 wa kutoka tarime mara ili kuwakata mapanga......."

nashindwa niamini lipi na nisiamini lipi.

Kweli human being are political animals............
 
Hawa watakuwa wamevukishiwa kupitia Arusha au moshi, itakuwa Lema ndio muhusika mkuu kwasababu anazijua vizuri njia za panya alizo kuwa akizitumia kwenye biashara ya wizi wa magari.

WanaCDM wamesha igeuza hii stori kuwa ni uzembe wa jeshi wakisahau tuhuma hiyo inawahusu wao kuleta majambazi nchini.
Wewe unacheza na Interahamwe 800 si kitu kidogo ni jeshi kubwa tena liingie kwa mji mdogo kama Igunga lazima Jeshi letu litaarifiwe na Mwigulu atusaidie.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom