Mwigulu Nchemba na Elibariki Kingu, hata undugu kwenu kwa Lissu umekufa?

Nadhani hata Nyarandu sijui kama atapona katika hili, labda kwa sababu yeye ni mbunge tu
 
Inasikitisha sana kuona hawa ndugu zangu wawili ambao kimsingi wote wawili ni wabunge ambao majimbo yao ni ya mkoa wa Singida, Tukimwacha ndugu yetu Lazaro Nyalandu lakini hawa watu wawili hatujawasikia hata mmoja kati yao walao akikanyaga Nairobi au akisikika kuwapa hata ndugu wa mgonjwa pole.Basi hata wangeonesha ile roho ya huruma na upendo kwa ndugu yao.

Itikadi ya kisiasa tu ndio inatufikisha huku? Hakika inasikitisha sana, sisi WANASINGIDA tumefedheheshwa sana na ukimya wa hawa ndugu zetu,tumechukia sana na tumegundua kua sio watu wazuri hata kidogo na hili sio jambo la kawaida kutokea.

Pamoja na Lissu kua na madaifu yake kama binadamu wrngine au kufanya kile ambacho ninyi mlikua hamkipendi, lakini kwa hali ya kiutu na ubinadamu hatukupaswa kufikia huku! Mmetuacha na maswali mengi sana vinywani sisi kama WANASINGIDA. Mlipaswa kua wabunge wa kwanza na mstari wa mbele kuhakikisha kua mwenzenu anasaidiwa kwa suala la matibabu.

Kama mkuu wa mkoa tu yuko msitari wa mbele kuhimiza wananchi kumwombea na kumchangia ndugu yetu Lissu, Je,ninyi ambao mlikua mkiiingia mlango mmoja wa bunge na pengine hata kula chakula meza moja mmeshindwaje kuambatana nae kwenye suala la matibabu? Hivi kwa hili mtajiteteaje jamani?

Ndugu yangu Mwigulu Nchemba ukiweka kofia yako ya uwaziri wewe ni mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi ndani ya mkoa wa Singida, nimekutaja wewe kwa sababu kwanza ni umaarufu halafu pia kiongozi ndani ya serikali, kwakweli juu ya hili umetuangusha sana ndugu yangu. Elibariki Kingu ni mbunge wa jimbo la Singida Magharibi linalopakana na jimbo la Lissu, nae ameshindwaje kua karibu kwenye suala la matibabu ya mgonjwa?

Sisi WANASINGIDA hua ni wamoja kwenye masuala ya kijamii tukiweka itikadi zetu pembeni, sasa hawa ndugu zetu imekuwaje tena? Niseme tu wazi sisi tumeichukulia kama ni suala la chuki tu labda kuwe na jambo lingine lililowazuia wabunge hawa kuonesha upendo kwa ndugu yao.

Wachamungu siku zote honekana kwa kitendo tuu!
Sema ww,usisemee nafsi za wenzako
 
Kinachowasuta hata ni matukio na matamko yao dhidi ya Lissu na Chadema,tunajifunza kuwa kupambane kwa hoja na kisiasa sio kutumia dola kuqngamizana
 
Na kibaya zaidi Nchemba ndiye Waziri Wa mambo ya ndani ya Nchi haya mambo n yeye mwenye dhamana ya kudili nayo ila daaa kimyaaaaaa
 
Afadhali hata Mwiguru yuko Wilaya nyingine lkn Kingu na Lissu wanatoka wilaya moja na wote ni wajumbe wa baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi....hivi vyama kweli vimetufikisha pabaya..
 
tusiwahukumu tusije hukumiwa.Nina imani wanampenda sana ndugu yao kuliko hata sisi wengine.Kumbuka damu nzito kuliko maji.Ndugu hufukuzana huku wakionyeshana mashimo barabarani.
 
Elibariki Kingu,,anajipendekeza kweli kwa Bashite,,nadhani anataka uwaziri flani..
Labda pia kwa kuwa Mwigulu na Elibariki ni wanyiramba,,damu sio maji.
 
Inasikitisha sana kuona hawa ndugu zangu wawili ambao kimsingi wote wawili ni wabunge ambao majimbo yao ni ya mkoa wa Singida, Tukimwacha ndugu yetu Lazaro Nyalandu lakini hawa watu wawili hatujawasikia hata mmoja kati yao walao akikanyaga Nairobi au akisikika kuwapa hata ndugu wa mgonjwa pole.Basi hata wangeonesha ile roho ya huruma na upendo kwa ndugu yao.

Itikadi ya kisiasa tu ndio inatufikisha huku? Hakika inasikitisha sana, sisi WANASINGIDA tumefedheheshwa sana na ukimya wa hawa ndugu zetu,tumechukia sana na tumegundua kua sio watu wazuri hata kidogo na hili sio jambo la kawaida kutokea.

Pamoja na Lissu kua na madaifu yake kama binadamu wrngine au kufanya kile ambacho ninyi mlikua hamkipendi, lakini kwa hali ya kiutu na ubinadamu hatukupaswa kufikia huku! Mmetuacha na maswali mengi sana vinywani sisi kama WANASINGIDA. Mlipaswa kua wabunge wa kwanza na mstari wa mbele kuhakikisha kua mwenzenu anasaidiwa kwa suala la matibabu.

Kama mkuu wa mkoa tu yuko msitari wa mbele kuhimiza wananchi kumwombea na kumchangia ndugu yetu Lissu, Je,ninyi ambao mlikua mkiiingia mlango mmoja wa bunge na pengine hata kula chakula meza moja mmeshindwaje kuambatana nae kwenye suala la matibabu? Hivi kwa hili mtajiteteaje jamani?
Nadhani kuna nguvu fulani imemzuia Mwigulu maana siku ile akitoa kauli baada ya tukio la kupigwa risasi Lisu nilimuona Nchemba katika hali ya huzuni kubwa juu ya tukio lile sijawahi kumuona akiwa vile usoni hata siku moja tangu nimjue huyu bwana.
Kwa hisia zangu huyu jamaa atakuwa anasaidia matibabu ya Lisu kimtindo hawezi kuwa amenyamaza tu.

Ndugu yangu Mwigulu Nchemba ukiweka kofia yako ya uwaziri wewe ni mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi ndani ya mkoa wa Singida, nimekutaja wewe kwa sababu kwanza ni umaarufu halafu pia kiongozi ndani ya serikali, kwakweli juu ya hili umetuangusha sana ndugu yangu. Elibariki Kingu ni mbunge wa jimbo la Singida Magharibi linalopakana na jimbo la Lissu, nae ameshindwaje kua karibu kwenye suala la matibabu ya mgonjwa?

Sisi WANASINGIDA hua ni wamoja kwenye masuala ya kijamii tukiweka itikadi zetu pembeni, sasa hawa ndugu zetu imekuwaje tena? Niseme tu wazi sisi tumeichukulia kama ni suala la chuki tu labda kuwe na jambo lingine lililowazuia wabunge hawa kuonesha upendo kwa ndugu yao.

Wachamungu siku zote honekana kwa kitendo tuu!
 
Kama ni siasa hizi ninazo ziona tunazoenda nazo za ndugu, marafiki na jamii moja kuonana ni maadui bora tukabidhi nchi hao jamaa wenye magwanda watusaidie kidogo kuiendesha hadi hapo tutakapo jua siasa nini. Siasa gani hiyo ambayo baba na mwana wasiongei au baba aue mwanae na jirani ashindwe kumjulia hali jirani yake. Niombe tufike sehemu hawa viongozi wanao tuambia tufanye siasa za namna hii tuwambie "NO".
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom