Mwigulu Nchemba: Msihofie Mikopo, riba yake ni ndogo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,357
8,069
Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba akiwa Dar es salaam leo ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuwa Mdau Mkuu wa Maendeleo ya Tanzania kwa kutoa mikopo nafuu na misaada mbalimbali inayotumika kutekeleza miradi inayochochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Watu ambapo mpaka sasa, Benki hiyo, imetoa dola za Marekani Bilioni 7.8.

Waziri Mwigulu @mwigulunchemba amewatoa hofu Watanzania kuhusu mikopo ambayo Serikali inakopa kwa ajili ya kuharakisha maendeleo yao ambapo amesema asilimia 73 ya mikopo hiyo inatoka Taasisi za Fedha za Kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia ambayo riba yake ni ndogo (chini ya asilimia 1), na kipindi cha kulipa kinaanza baada ya muda mrefu.

“Kipindi cha neema (grace period) kabla hatujaanza kulipa ni kirefu ambacho ni kati ya miaka 30 hadi 40 tofauti na masharti ya mikopo ya kibiashara ambayo inalipwa ndani ya miaka miwili hadi 10 na riba yake ni kubwa”

Dkt. Nchemba amesema mikopo inayokopwa na Serikali inawekezwa kwenye maeneo ya miradi inayoweza kuchochea uchumi wa nchi haraka na pia ndiyo maana Tanzania inauchumi ulio imara na vigezo vyake kuhusu deni la Taifa ni himilivu.

AYO TV
 
Back
Top Bottom