Mwigulu Nchemba, Mnalofanya Serikali ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za kodi na mnadhani Watanzania hawaelewi

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,585
2,000
Mwigulu Nchemba, ambaye siku zote ametueleza kwamba yeye ni mchumi mbobezi aliefaulu degree yake ya uchumi pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa daraja la kwanza, anakuja kutufafanulia Watanzania kwamba serikali imefanya ufikirio saa katika suala la kodi ya laini ya simu ili isiwaumize Watanzania. Kimsingi huo si ukweli.

Kama Mwigulu alifanya vizuri kama anavyodai katika degree yake ya uchumi, basi atakumbuka kwamba kanuni moja ya msingi katika kodi ni kwamba huwezi kumtoza kodi mnunuzi mara mbili kwa huduma au bidhaa ileile. Huo ni unyanyasaji au wizi wa kiserikali.

Sasa Mwigulu na serikali kwa makusudi kabisa, wameamua kututoza watanzania kodi ya kununua airtime au data katika huduma za simu mara mbili, halafu wanaona ni sawa. Kumbuka kwamba kila unaponunua airtime, lazima ulipe VAT - ambayo ni kodi. Na sasa juu ya hii VAT, Mwigulu na serikali wanakuja na kodi nyingine, kati ya Shs 10 hadi shs10,000. Hii ni kodi, na wamekiri hivyo.

Ili kuepuka labda serikali kufunguliwa mashitaka ya kikatiba juu ya suala la kutoza kodi mara mbili kwa huduma ileile, wakadhani ni akili sana kuiita hii kodi ya pili "Kodi ya Laini ya Simu". Lakini hii si kweli, hii sio kodi ya laini za simu. Ingekuwa hivyo ingepaswa kukatwa pale unaponunua line ya simu. Huko ni kutumia technicalities kupotosha ukweli. Hii kodi ni juu ya kitu kile kile ambacho kinatozwa kodi kama VAT - kununua airtime au data, in essence doubl taxation, na ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za kodi. Na kama ingekuwa ni "line service charge" isingepaswa kubadilika kutegemea kiasi cha airtime au data unachonunua, ingebaki palepale, fixed amount.

Najua huenda walifikiria kuiita hii kodi "levy" badala ya "kodi". Lakini sasa, Mwigulu na serikali walijua wazi kwamba ikiwa wangeiita levy, basi matumizi ya mapato ya hiyo levy yangepaswa kuwa ndani ya sekta ya mawasiliano - yaani ring-fenced. Kanuni za levy zinataka ukitoza levy basi mapato yake yaende kuboresha huduma ndani ya sekta hiyo levy inapokatwa. Mfano, huwezi kukata levy ya road maintanance kwenye mafuta, halafu uchukue fedha kuzipeleka kulipa mishahara ya serikali ya bara na visiwani.

Na kama ingekuwa "line service charge" serikali ilijua wazi basi ingepaswa kunufaisha pia kampuni za simu, sio kwenda serikalini. Hilo serikali iliona kabisa haiwezekani.

Na sijui kwa nini waliona aibu kusema ni levy badala ya kodi ya laini ya simu, kwa kuwa serikali haijawahi kuwa na aibu ya kutumia makato ya levy kwa kitu kisichokusudiwa. Angalia kwa kila lita ya petroli na dizeli kuan levy ya road mainatance, mabilioni ya shilingi kila siku, lakini serikali bila aibu inachukua hizo fedha na kuzipeleka kwenye matumizi yasiyohusika kabisa na barabara, na kutojali kwamba barabarani kuna mashimo ambayo yanasababisha ajali zinazoharibu magari na hata kuleta vifo. Hawajali. Mashimo yanabaki barabarani hata mwaka mzima, wakati fedha za angalau kuyafukia tumeshalipa!

Kuna levy pia kwenye vitu kama bill za umeme, kwa ajili ya kuwapa REA kusambaza umeme vijijini. Lakini mtu akikuambia hiyo levy imetumika kwenye gharama za uchaguzi wala usishangae.

Kwa hiyo Mwiguli Nchemba, tunawaambia wazi. Mnachofanya ni ukiukwaji wa taratibu za kodi na msidhani kwamba hatuoni. Mnaiita kodi ya laini ya simu lakini ni kodi inayokatwa kwa kununua airtime au data ambazo tayari zina kodi - VAT. Na tunajua kwa nini mmeogopa kuiita levy, kwa kuwa kama ni levy basi haipaswi kutumika kulipia mishahara na posho nyingi za wabunge, na mlishindwa kabisa kuuelewa kama mkiita levy mtasema ni levy kwa ajili ya nini na ingewabana kikatiba kuingiza hizo fedha kwenye matuizi yenu yasiyo na tija na suala la mawasiliano.

You can fool some people sometimes, but not all the people all the times.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
8,449
2,000
Nasubiri kuona kama hizi tozo zao zitadumu mpaka 2025! Kwa aina hizi za tozo, ni wazi serikali yetu imeishiwa vyanzo vipya na rafiki vya kukusanya mapato.

Kinachokera ni kwa upande wao kuto onesha kabisa dalili za kupunguza matumizi yao ya kila siku! Wabunge bado wanajilipa mabilioni ya shilingi kila mwezi kama posho na mishahara, serikali bado inachezea tu fedha za walipa kodi kwa kulipia vyeo visivyo na tija kama vile vya Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Ma Ras, Ma Das, nk! Ma V8 bado yanaendelea kununuliwa kila siku!
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,585
2,000
1624006493598.png
 
Rogojin The Idiot

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
1,712
2,000
Zamani kidogo, wafanya biashara walipokuwa wanalalamika kodi zinaongezwa mara mbili mbili walioekana wazushi, Kwa mfano, unanunua gari. Hela ya kununua inajulikana. Ila ukifika dar kodi inakuwa uplifted. Unaanza kushangaa kulikoni.

Kama Watanzania wote tukianza kuona maumivu ya kodi na kuhoji matumizi yake, nafikiri tutakuwa tumeanza kukua. Mzogo wako kodi ubebwe na watanzania wote. Sio asilimia 3 tu ya Watanzania mil 60. That is not sustainable
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,585
2,000
Nasubiri kuona kama hizi tozo zao zitadumu mpaka 2025! Kwa aina hizi za tozo, ni wazi serikali yetu imeishiwa vyanzo vipya na rafiki vya kukusanya mapato.

Kinachokera ni kwa upande wao kuto onesha kabisa dalili za kupunguza matumizi yao ya kila siku! Wabunge bado wanajilipa mabilioni ya shilingi kila mwezi kama posho na mishahara, serikali bado inachezea tu fedha za walipa kodi kwa kulipia vyeo visivyo na tija kama vile vya Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Ma Ras, Ma Das, nk! Ma V8 bado yanaendelea kununuliwa kila siku!
Mkuu yaani wala huko usiende, maana inatia hasira tu. Kuna siku haya mambo yatafikia critical mass then serikali itagundua Watanzania sio wapole kama wanavyofikiria
 
Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
17,184
2,000
Nasubiri kuona kama hizi tozo zao zitadumu mpaka 2025! Kwa aina hizi za tozo, ni wazi serikali yetu imeishiwa vyanzo vipya na rafiki vya kukusanya mapato.

Kinachokera ni kwa upande wao kuto onesha kabisa dalili za kupunguza matumizi yao ya kila siku! Wabunge bado wanajilipa mabilioni ya shilingi kila mwezi kama posho na mishahara, serikali bado inachezea tu fedha za walipa kodi kwa kulipia vyeo visivyo na tija kama vile vya Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Ma Ras, Ma Das, nk! Ma V8 bado yanaendelea kununuliwa kila siku!
Hizo kodi ziongezwe mara 20 ili kuwakomoa mataga
 
mfianchi

JF-Expert Member
Jul 1, 2009
10,489
2,000
Mkuu sijui tukupen
Mwigulu Nchemba, ambaye siku zote ametueleza kwamba yeye ni mchumi mbobezi aliefaulu degree yake ya uchumi pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa daraja la kwanza, anakuja kutufafanulia Watanzania kwamba serikali imefanya ufikirio saa katika suala la kodi ya laini ya simu ili isiwaumize Watanzania. Kimsingi huo si ukweli.

Kama Mwigulu alifanya vizuri kama anavyodai katika degree yake ya uchumi, basi atakumbuka kwamba kanuni moja ya msingi katika kodi ni kwamba huwezi kumtoza kodi mnunuzi mara mbili kwa huduma au bidhaa ileile. Huo ni unyanyasaji au wizi wa kiserikali.

Sasa Mwigulu na serikali kwa makusudi kabisa, wameamua kututoza watanzania kodi ya kununua airtime au data katika huduma za simu mara mbili, halafu wanaona ni sawa. Kumbuka kwamba kila unaponunua airtime, lazima ulipe VAT - ambayo ni kodi. Na sasa juu ya hii VAT, Mwigulu na serikali wanakuja na kodi nyingine, kati ya Shs 10 hadi shs10,000. Hii ni kodi, na wamekiri hivyo.

Ili kuepuka labda serikali kufunguliwa mashitaka ya kikatiba juu ya suala la kutoza kodi mara mbili kwa huduma ileile, wakadhani ni akili sana kuiita hii kodi ya pili "Kodi ya Laini ya Simu". Lakini hii si kweli, hii sio kodi ya laini za simu. Ingekuwa hivyo ingepaswa kukatwa pale unaponunua line ya simu. Huko ni kutumia technicalities kupotosha ukweli. Hii kodi ni juu ya kitu kile kile ambacho kinatozwa kodi kama VAT - kununua airtime au data, in essence doubl taxation, na ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za kodi. Na kama ingekuwa ni "line service charge" isingepaswa kubadilika kutegemea kiasi cha airtime au data unachonunua, ingebaki palepale, fixed amount.

Najua huenda walifikiria kuiita hii kodi "levy" badala ya "kodi". Lakini sasa, Mwigulu na serikali walijua wazi kwamba ikiwa wangeiita levy, basi matumizi ya mapato ya hiyo levy yangepaswa kuwa ndani ya sekta ya mawasiliano - yaani ring-fenced. Kanuni za levy zinataka ukitoza levy basi mapato yake yaende kuboresha huduma ndani ya sekta hiyo levy inapokatwa. Mfano, huwezi kukata levy ya road maintanance kwenye mafuta, halafu uchukue fedha kuzipeleka kulipa mishahara ya serikali ya bara na visiwani.

Na kama ingekuwa "line service charge" serikali ilijua wazi basi ingepaswa kunufaisha pia kampuni za simu, sio kwenda serikalini. Hilo serikali iliona kabisa haiwezekani.

Na sijui kwa nini waliona aibu kusema ni levy badala ya kodi ya laini ya simu, kwa kuwa serikali haijawahi kuwa na aibu ya kutumia makato ya levy kwa kitu kisichokusudiwa. Angalia kwa kila lita ya petroli na dizeli kuan levy ya road mainatance, mabilioni ya shilingi kila siku, lakini serikali bila aibu inachukua hizo fedha na kuzipeleka kwenye matumizi yasiyohusika kabisa na barabara, na kutojali kwamba barabarani kuna mashimo ambayo yanasababisha ajali zinazoharibu magari na hata kuleta vifo. Hawajali. Mashimo yanabaki barabarani hata mwaka mzima, wakati fedha za angalau kuyafukia tumeshalipa!

Kuna levy pia kwenye vitu kama bill za umeme, kwa ajili ya kuwapa REA kusambaza umeme vijijini. Lakini mtu akikuambia hiyo levy imetumika kwenye gharama za uchaguzi wala usishangae.

Kwa hiyo Mwiguli Nchemba, tunawaambia wazi. Mnachofanya ni ukiukwaji wa taratibu za kodi na msidhani kwamba hatuoni. Mnaiita kodi ya laini ya simu lakini ni kodi inayokatwa kwa kununua airtime au data ambazo tayari zina kodi - VAT. Na tunajua kwa nini mmeogopa kuiita levy, kwa kuwa kama ni levy basi haipaswi kutumika kulipia mishahara na posho nyingi za wabunge, na mlishindwa kabisa kuuelewa kama mkiita levy mtasema ni levy kwa ajili ya nini na ingewabana kikatiba kuingiza hizo fedha kwenye matuizi yenu yasiyo na tija na suala la mawasiliano.

You can fool some people sometimes, but not all the people all the times.
Mkuu sijui Mungu akupe nini kwa kutufungua macho sisi vihiyo, nadhani hii wizara angepewa mtu kama Kimei lakini shida kubwa mkuu ni tatizo la utashi kwa viongozi wetu akiwemo na raisi mwenyewe ama raisi amedanganywa na wanaojipendekeza kwake au raisi hajui hayo madhara ya hizo''levy'' au nae ndio kaamua kututupa chini ya basi. Pia wabunge wetu wamekaa kimya kama kwamba hilo jambo ni jambo la kawaida, kwa hili inatakiwa sote tuseme HAPANA kwa sauti KUBWA!
 
Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
9,585
2,000
Moderators:

Ni sawa kama mmeamua kurekebisha kichwa cha thread, lakini basi, rekebisheni hiyo typo mliyofanya kwenye neno serikali, linapaswa kuwa serikalini

Mwigulu Nchemba, Mnalofanya Serikali ni ukiukwaji mkubwa wa kanuni za kodi na mnadhani Watanzania hawaelewi​

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom