Mwigulu Nchemba mbona yupo kimya bungeni siku hizi?

Usifanye mchezo na SCUD ya EPA mazee!
Mhe. Mnyika alifanya timing moja saafi sana.
Yaani Mwigulu karushiwa scud moja tu ya EPA chini kule miguu juu.Shhhhheenzziiiiiiiii kabisa!
 
Huyu hapa


MHE. AMINA ABDALLAH AMOUR: Mheshimiwa Mwenyekiti, siungi mkono hoja. (Makofi)
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa
nafasi hii ili nizungumze na Watanzania. Awali ya yote, Watanzania wanatakiwa wawe makini
sana na waigizaji. Ukimpata mwigizaji mzuri, unaweza ukalia, kumbe mwenzio anaigiza na hiki
ndicho ambacho kimetokea muda mfupi uliopita hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa...
MWENYEKITI: Mheshimiwa, nakuomba ufute neno uigizaji.
WABUNGE FULANI: Aaah!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafuta kama kuna waigizaji hapa.
MWENYEKITI: Naomba ufute neno uigizaji.


MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nafuta neno uigizaji kama kuna
waigizaji, lakini maana ya kusema hivi ilikuwa ni hii, tatizo linalojitokeza hapa ni kwamba, bajeti
imeandaliwa na wataalam, lakini watu badala ya kuuliza wajue undani wa bajeti, aliyesomea
Sheria za Mambo ya Kichawi na yeye anakuwa mchambuzi wa uchumi, mwenye uzoefu wa
kuendesha disko anakuwa mchambuzi wa uchumi, unawachanganya Watanzania. Sasa uhalisia
ndio huu, mimi ni Mchumi wa Daraja la Kwanza na Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, ngojeni
niwaambie uhalisia wa bajeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwenye Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano,
tunapoongelea 35%, tunajumuisha pamoja na uwekezaji kwenye sekta ya elimu lakini
tunapozungumzia bajeti hii ya leo, sekta ya elimu iko pembeni, fedha zake zimewekwa pembeni,
zile za maendeleo zimewekwa pembeni. Watanzania tuulizane, hivi kweli tunaposomesha
wanafunzi vyuo vikuu, hatuwekezi? Hivi kweli tunapojenga maabara, hatuwekezi? Hivi ni kweli
tunaposomesha vyuo, tunapoandaa Wataalam wa Ugani, tunapoandaa Madaktari, hatuwekezi?
Tulisoma wapi? Hiyo Sheria iliyokuwa inatenga investiment on human capital, ilikuwa ni ya miaka
ya 50 na 60 lakini ukisoma David Roma, ukasoma Waive, ukasoma Mankyu, miaka ya 90, Cop
Douglas Production Function, inatambua human capital kama investiment. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mpango wa Maendeleo huu tunaojadili, umejumuisha
investiment on human capital ndio ukapata 35%. Ukienda kwenye bajeti ya mwaka huu,
ukichukua investiment kwenye elimu, uwekezaji tuliouweka kwenye elimu, bajeti ya maendeleo
inaenda 39% kwenda 40%. Mmesoma wapi nyie? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la pili, ukiingalia kiutaalamu tu bajeti yenyewe, kiutaalamu
tu, dependency ratio, utegemezi bajeti imepungua. Ukiweka na ile mikopo kwa sababu mikopo
nayo ni fedha yetu tutalipa, ukiondoa na ile ya mikopo, utegemezi kwenye bajeti imebaki 6.5%.
Sifa nyingine ya bajeti, ukienda zile fedha zinazoenda kwenye kulipa mishahara, hamna hata senti
moja inayoenda kwenye mishahara, mishahara inalipwa na fedha za ndani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu muone sasa hili nililolisema ambalo mmesema nilifute, hebu
oneni sasa Bajeti ya Kivuli, wameandika kwamba, kima cha chini kitakuwa 315,000/= hawajui
wanaolipwa kima cha chini ni wangapi, zidisheni mpate hesabu, mimi nitawaambia mwishoni.
Halafu chukueni Walimu muwapandishie mishahara mara 50, chukua Madaktari uwapandishie
mara 50, chukua Manesi uwapandishie mara 50, tafuta jumla yake. Halafu chukua walewale,
makundi matatu haya, uwapandishie mara moja na nusu, bajeti ya matumizi inaenda zaidi ya hii
shilingi bilioni tisa waliyoandika wao. Hii waliyoandika kwenye matumizi ya kawaida inazidi,
ukijumlisha na ile wanayosema kwamba watalipa pensheni kwa wazee, hawajui idadi ya wazee,
ukijumlisha inakuwa zaidi ya shilingi trilioni 15, mmnatumia bajeti ya wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu wanasema...
MBUNGE FULANI: Silly thinking.
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi hili nitalirudia tu, halafu
wanasema kujenga, wanasema kupunguza mzigo wa matumizi ya magari. Mwaka jana
Mwenyekiti wao, Mheshimiwa Mbowe, alirudisha gari akisema kwamba, kupunguza matumizi,
akawahadaa Watanzania. Baada ya muda fulani, kumbe alilikataa lile gari kwa sababu
limechakaa, lilikuwa linatumiwa na Kiongozi aliyepita, baada ya muda fulani kachukua
kimyakimya gari lingine analitumia. Amelirudisha kimyakimya hajawaambia Watanzania kama
ameshalichukua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa watu wanatakiwa kwa kweli Wachamungu wote, mimi
tangia nizaliwe sijawahi kuona Kambi ya Upinzani yenye pepo mtaka vyeo kama hawa hapa.
(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanatakiwa waombewe, watalipeleka Taifa pabaya, mimi
nawaambia Watanzania mkiendelea kushabikia watu ambao haijulikani kama wako normal au
wanatakiwa wawe Mirembe mtapata kiongozi kama Iddi Amini hapa.


MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!
MBUNGE FULANI: Mwehu huyu!
MBUNGE FULANI: Mwongozo! Anatutukana huyu!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Nimesema niseme na Watanzania, ngojeni niwaambie,
jambo lingine ambalo wanalolikataa hapa, ngojeni mjue unafiki uko wapi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine wanalolikataa wanaongelea OC kama vile ni
dhambi kubwa kwelikweli, angalieni OC kuna nini, OC Serikali imetenga shilingi bilioni 140 kupeleka
vijana JKT, hivi kweli hiyo ni dhambi kupeleka vijana JKT. (Makofi)
MBUNGE FULANI: Waambie!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Serikali imetenga OC kwenda kwenye Tume ikakusanye
maoni ya Katiba Mpya, mnataka Katiba Mpya hamtaki tuweke bajeti, mnataka Katiba mpya kwa
kutumia fedha gani.
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Serikali imetenga fedha kwenye OC kwa ajili ya sensa,
mnataka sense, hamtaki tuweke bajeti. Serikali imetenga fedha kwenye OC kwa ajili ya fidia za
watu wanaondolewa kwenye maeneo kupisha miradi ya maendeleo, mnataka zisiwekwe, wale
watu mtawapatia hela gani mnapowaondoa pale? Serikali imetenga fedha kwenye OC kwa ajili
ya chakula, wanafunzi, wafungwa, wagonjwa mnataka ziondoke mtawapa nini? (Makofi)
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mimi sijawahi kuona Bajeti Kivuli ya aina hii, this is concisely
and precisely rubbish. (Makofi)
MWENYEKITI: Samahani kaa chini, Mheshimiwa naomba ukae.
MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
(Kicheko/Makofi/Vigelegele)
MWENYEKITI: Ngojea Mheshimiwa Mwigulu, order in the House, Mheshimiwa Mwigulu
naomba ufute neno pepo kwa sababu ni kinyume…
(Hapa baadhi ya Wabunge walizomea)
MWENYEKITI: Order in the House.
MBUNGE FULANI: Mbona walipotaja Mungu mpya hukusema?
MWENYEKITI: Order in the House.
MBUNGE FULANI: Afute.
MWENYEKITI: Order in the House, naomba ufute neno pepo halafu tuendelee.
MBUNGE FULANI: Mwongozo!
MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwigulu futa neno pepo tuendelee.
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika!


MHE. MWIGULU L. M. MADELU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa humu ndani nafuta lakini watu
wa aina hiyo wakaombewe, nafuta neno hilo. (Makofi)
MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.
MWENYEKITI: Naomba tuendelee.
MBUNGE FULANI: Kuhusu utaratibu!
MWENYEKITI: Naomba tuendelee, sasa namwita Mheshimiwa Ahmed Ally Salum na
Mheshimiwa Amina Clement ajiandae na atafuatia Mheshimiwa Komba. Yupo au hayupo?
MBUNGE FULANI: Yupo!
 
Mwigulu anajipanga kujibu tuhuma za EPA, anakusanya nondo, CHADEMA kuweni makini Mwigulu ni hatari.Ngoja niwaambie sifa moja ya wanyiramba, ni wabishi wa kuzaliwa na waliosoma ni welevu sana, yaani chadema hapo mmefika na amekabidhiwa mikopa na CCM kuhakikisha anawachanganya.Hongera mwigulu kwa sababu unapigania ugali wako.
 
Ametishiwa na watu wa jimboni kwakw hapa Singida kuwa asipokuwa makini na akiendelea na makelele watammwaga next term.

Kumbe!
Mi nilidhani alitumwa na wananchi wa jimbo lake kuishambulia chadema tu.
 
Wakuu toka juzi mheshimiwa John Mnyika amlipue mbunge wa Iramba Mashariki Mwigulu Nchemba kuwa ni mtuhumiwa wa wizi wa pesa za EPA,mbunge huyo amekuwa kimya na ameacha kuropoka ropoka ovyo maneno machafu.Ama kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni ile miongozo aliyokuwa akiomba Mwigulu Nchemba kila walipokuwa wakichangia wabunge wa CHADEMA imeishia wapi?

Kwanini Mwataka aongee Kiongozi asiyefaa wa Central Committee ya CCM, Kila kitu kwake ni Jazba hana HOJA
 
Chadema watafanya m4c jimboni kwake mara tu baada ya kikao cha bunge
ndipo atakapojua maana ya kuwa na "a'' wakati watu hawana maji, hospitali na mabilioni ya pesa yanaibiwa na kuhifadhiwa nje huku bot wakijua
 
Anapokuwa anaongea waweza sema anaongea ukweli kumbe ni mwongo, amefanikiwa kwa kiasi fulani kuwafool watu wanaomsikiliza bila kujiuliza nini anaongea, na bahati mbaya akitamka people wanaamini ndivyo kumbe sivyo, Mwigulu ni mjanja, amefanikiwa kuwa mwimbaji bora wa taarabu bungeni
 

Tangazo M4C Iramba Mangaribi - August 2012.


Chama cha CHADEMA kitafanya Ziara ya Mwezi Mzima katika Jimbo la Iramba Mangaribi ambalo ni Jimbo la Mh. Mwigulu Nchemba kwa ajili ya kuimarisha chama, Mada zitakazozungumziwa katika Ziara hiyo ni;

1. Utendaji wa BOT kati ya Mwaka 2006 - 2010
2. Wizi wa Fedha za EPA
3. Uhusika wa BOT na Taratibu za ufunguaji Akaunti nje ya nchi
4. Uhusika wa Wafanyakazi wa BoT na wizi wa pesa za EPA
5. Uhusika, usaidizi, ushauri wa kitaalamu wa wafanyakazi wa BOT uliosaidia kuibwa kwa Fedha za EPA
6. Ushauri Mbovu wa masuala ya Uchumi katika kipindi cha 2006 - 2010 ndani ya BoT
7. Ugumu wa maisha ya wananchi wa Iramba Mangaraibi, suluhisho la Matatizo yao.
8. Matatizo ya Elimu katika Jimbo la Iramba Magharibi,
9. Utendaji wa Kazi wa Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi,
10. Serekali kushindwa kushughulikia Mauaji ya Raia baada ya uchaguzi wa Igunga na Arumeru Mashariki.
11. Hali ya Uchumi ya Nchi.

Wazungumzaji Wakuu:

1. Freeman Mbowe
2. Mchungaji Msigwa - Kiongozi wa Ziara
3. Mh. John Mnyika - Katibu wa Ziara
4. Dr. Wilbrod Silaa
5. Godbless Lema
6. Halima Mdee
7. Joshua Nassari
8. Mh. Wenje

Wazungumzaji Huru.

1. Ma Profesa wawili wa Uchumi - Chuo Kikuu Dar - Es - Salaam
watatoa elimu kwa umma kuhusu Uchumi na utekelezaji wa Mipango ya Taifa - Majina yanahifadhiwa kwa sasa.

2. Wanaharakati Mashuhuri Wawili - Majina yanahifadhiwa kwa sasa
3. Uongozi wa TAMWA - Taifa
4. Aliyekuwa Mgombea wa Ubunge Igunga
5. Mume wa Mwanamke aliyefumaniwa na kiongozi wa Juu wa CCM Igunga
6. Baba mzazi wa Kijana aliyekutwa amekufa Igunga mara baada ya Kampeni
6. Wazazi na Mke wa Kiongozi wa Chadema aliyeuwawa Arumeru mara baada ya Uchaguzi
7. Wazazi wa Vijana Wanne waliouwawa kwa kuvunjwa Shingo na kutupwa Jimbo la Arumeru Mashariki
8. Viongozi wa Dini kuu mbili za Kiislam na Kikristo
9. RPC Mstaafu
10. Ungozi wa Kitaifa LHRC (Haki za Binadamu) Tanzania
11. UONGOZI WA KITAIFA - TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA (THBUB)
12. Kiongozi wa wazee wa Iramba.

KAZI HII ITAKUWA NI YA MWEZI MMOJA.

Hizi ni Namba za Mwigulu Nchema kama unataka kumpa Taarifa.
Office Location:Box 52 Kiomboi, Iramba
Office Phone: +255 878 513446/+255 757 946223
 
Ule ulikuwa ni utoto tu, sasa kakua.


Mwizi wa fedha ya UMMA huwa hakui maamuma,labda pale tu anapotoka jela kidooooooogo tunaweza hisi hisi ameanza kukua.Hivyo hao kina mwigulu nchemba,rada vijisenti,billionz uswizi,jairo nini sijui bado hawajakuwa.Pale tu watakapotoka jela ndo tunaweza kudhani vinginevyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom