Mwigulu Nchemba kwa anayofanya yupo sahihi, soma hapa

KUNAKITU ANAKITAJA KWENYE WARAKA WAKE ILA HAJUI KUWA NDICHO KINAKIUA CHAMA CHETU.
HOJA YA KWANZA MPAKA YA 4 ANAKIRI KUWA CCM NI CHAMA CHA MSIMU.

HOJA NYINGINE ANAJARIBU KUTUAMBIA KUWA CCM INASEMWA VIBAYA NA WAPINZANI KWA HIYO ITAFUTE WATU WA KUISEMEA VIZURI,HAPA NDIPO ANACHEKESHA,KAZI MLIYOPEWA NA WANANCHI WA TANZANIA INAONEKANA KWA MACHO NA INATATHMINIKA HATA KWA MTU ASIYE NA KISOMO,HATA AJE MALAIKA AKAE KATIKA HICHO KITENGO CHA PROPAGANDA ZA KUWAAMBIA

WATANZANIA KUWA MMEFANYA MAZURI TU HATA YEYE ATAHAMIA UPINZANI KWA HALI ILIYOPO SERIKALINI NA KWENYE CHAMA.
UKITAKA KUAMINI HILI NINALOSEMA ENDELEENI KWA MWENDO HUU NDANI YA CHAMA NA MUWAPELEKE VIJANA JKT MKAWABANE HUKO NA KUWAPA KADI ZA CHAMA KAMA ZAMANI,MZIDISHE PROPAGANDA VYUO VIKUU KWA MIAKA MIWILI HALAFU MUWAACHE MAFISADI WAENDE;LEE KUITAFUNA NCHI,MADINI MUENDELEE KUCHUKU 3 ASILIMIA,UFISADI UENDELEE KUSHAMIRI

TANESKO,UDA,BANDARI,UHAMIAJI,VIWANJA VYA NDEGE,MBUGANI,RELI,AFYA,POLISI,MADINIO,KAMPUNI ZA SIMU,MISITU,PEMBEJEO ZA KILIMO,MAZAO YA MASIKINI,BAHARINI,MISAMAHA YA KODI NK,HALAFU MUONE NI NINI KITATOKEA 2015.

hayo ni maoni yangu.
 
Kwanza, kwa mshangao mkubwa, si amini kama hii text inatoka kwa Mwigulu Nchemba (I give him a benefit of doubt in the first place.) Kama huu ujumbe unatoka kwake, basi, naomba kuhitimisha kuwa, Migulu atakuwa mtu mwenye upeo mdogo sana, na hiyo First class degree (acha tu ya uchumi, hata ingekuwa ya degree nyingine yeyote) imepotea njia na hii inadhihirisha fika kuwa Mfumo wetu wa Elimu una tatizo kubwa mahali fulani.

The content in your text is slimy, well bluffed and highly uncoordinated.

If Migulu is taken to be one of the key people to take the party to places, I take it to be a day-dream and unrealistic fantasy that will end up in a total failure.

Ujumbe wenyewe tayari umeshakiharibia chama (Kama ulikuwa hujui), na ninaamini hujagundua maana hata michango yako huwa hainyeshi kama ulisoma, achilia mbali kujitapa kuwa mchumi wa first class.

WEWE NA WENZAKO MNAPASWA KUJIPANGA SIO KUKURUPUKA NA UJUMBE WENYE KASORO KAMA UMEANDIKA WAKATI KICHWA KIMEAZIMWA, ULIKUWA UNATUMIA SHINGO PEKE YAKE.


NIMEJITAIDI NIWEKE KWENYE FILE LAKE ORIGINAL IKAGOMA BUT SOMA SASA (tafakari chukua hatua... ngeengeee .. haki ya elimu...)

CHAMA CHA MAPINDUZI
KUHUISHA MTANDAO WA WANA CCM KATIKA VYUO NA MASHINA YA WAKEREKETWA

Kumetokea na sura tofauti katika hali ya kisiasa nchini hivi karibunikufuatia propaganda za CHADEMA kutaka kujipatia umaarufu na kujitafutia uhalalikwa njia ya kuichonganisha serikali na wananchi na kupandikiza chuki dhidi yaChama cha Mapinduzi. Hali hii imedhihirishwa na juhudi za makusudi zilizofanywana chama hicho za kupotosha ukweli, kutokuona ukweli na kung'ang'ania uzushikuwa ndio mtaji wao wa kisiasa bila hata kujali masilahi ya Taifa na misingi yautu iliojengwa kwa wananchi wake. Kwa mfano kumekwepo na upotoshaji wa kuwahakuna uthubutu wa serikali ya awamu ya nne, ubunifu, kubeza mafanikio nawakati mwingine kuropoka kuwa hakuna mafanikio yaliofikiwa tangia uhuru.
 
Mwigulu kwisha habari yake.Kajimaliza mwenyewe kiulaini katurahisishia kazi ya kumwondoa kabisa Iramba.
 
Wananchi hawataki ahadi ambazo zimekuwa kama hadithi wanataka maji dawa na huduma nyinginezo hasa haki na utawala wa sheria ccm imetufikisha hapa .
ukiibiwa ukienda police mpaka utoe pesa ndio upate msaada ,mahakamani angalia wanaofungwa ni wasio na pesa ..kesi ya mauwaji ya chenge iliisha muda mfupi lakini kuna walioko magereza miaka 7 ,magereza kama unapesa utalala kwako asubuhi unarudi magereza ..hospitali kila mahali haki sasa inanunuliwa ....kila kinachotokea kuhusu wanachi halifanyiwi kazi angalia meli iliopinduka juzi kuanzia saa 8 serikali ya ccm haikufanya lolote hata spika alikataa mawaziri husika wakaendelea kupiga porojo bungeni mpaka opposition walipo waacha ndani pekee yao wakaona aibu
 
Kwanza, kwa mshangao mkubwa, si amini kama hii text inatoka kwa Mwigulu Nchemba (I give him a benefit of doubt in the first place.) Kama huu ujumbe unatoka kwake, basi, naomba kuhitimisha kuwa, Migulu atakuwa mtu mwenye upeo mdogo sana, na hiyo First class degree (acha tu ya uchumi, hata ingekuwa ya degree nyingine yeyote) imepotea njia na hii inadhihirisha fika kuwa Mfumo wetu wa Elimu una tatizo kubwa mahali fulani.

The content in your text is slimy, well bluffed and highly uncoordinated.

If Migulu is taken to be one of the key people to take the party to places, I take it to be a day-dream and unrealistic fantasy that will end up in a total failure.

Ujumbe wenyewe tayari umeshakiharibia chama (Kama ulikuwa hujui), na ninaamini hujagundua maana hata michango yako huwa hainyeshi kama ulisoma, achilia mbali kujitapa kuwa mchumi wa first class.

WEWE NA WENZAKO MNAPASWA KUJIPANGA SIO KUKURUPUKA NA UJUMBE WENYE KASORO KAMA UMEANDIKA WAKATI KICHWA KIMEAZIMWA, ULIKUWA UNATUMIA SHINGO PEKE YAKE.

Ujumbe huu unatoka kwake 100%.... na mambo mengi sana yake, nilimpenda sana hilakaanza kuniudhi...., akiendelea naanika yote.
 
[LIST said:
[*]Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi uwahusishe wananchi ili waone vinavyofanyika pamoja na wabunge kutumia fursa hiyo kuwaeleza kuwa kinachotekelezwa kilikuwepo kwenye ahadi. Kwa mfano vitabu visigawiwe kimyakimya kwa kuwatumia watendaji wa sekta ya elimu kuwakabidhi waratibu na waratibu kuvifikishia ofisini bali kuwe kunafanyika mikutano inayohusisha wanafunzi na wananchi ili wajue hatua zinazochukuliwa. Ifanyike hivyo kwa huduma za afya, kwa maabara, umeme n.k kwa kadri itakavyowezekana.
[/LIST]


Hivi ni kweli kuwa watanzania wanachodai ni maonyesho ya kazi za serikali? Mbona kazi zinaweza kijidhihirisha hata kama hakuna maonyesho? Ni mara ngapi wameuza sura kwenye vyombo vya habari halafu huduma hazimfikii mwananchi wa kawaida?
Na hizo gharama za kuonyesha show kuubwa kukabidhi vitu kama vile ni msaada kumbe ni wajibu wa serikali ni nani atalipa? Mwananchi?
Naona kama mawazo ya mwandishi wa proposal hii anajustify kuundiwa kitengo cha kula tu, hamna la maana. Vinginevyo angefanya utafiti wa kutosha angeweza kujua tatizo ni nini? na wafanye nini?
 
Hivi kweli huu waraka umeandikwa na Lameck Mkumbo Maleba aka Mwingulu Nchemba? No it is not possible, guy with the calibre of Mwigulu to write waraka kama huu achilia mbali contexts ya waraka lakini pia hata uandishi wa maneno ni mbovu, Just look para 1 ONLY.
Kabunikufuatia; NENO MOJA
Uzushikuwa: Neno moja
Kuwahakuna: Neno moja
Nawakati: neno moja
Piakumekwepo: neno moja na spelling zimekosewa
Kunzingatiachanzo: Neno moja
Kamavile: neno moja
nawengine; Neno moja
Yaushabikiaji: Neno moja
nahata; Neno moja
Matokeoyake: neno moja
maeneotofautitofauti: neno moja
kamailivyoelezwa: Neno moja

Halafu eti huyu ndiye alikuwa first class economist wa BoT? This is only possible in Tanzania
 
Bwana Nchemba,

Nianze kwa kukushukuru kwa uamuzi wako wa kutushirikisha mawazo yako. Binafsi napenda mijadala. Napenda Kukosolewa. Napenda kukosoa. Napenda maneno mengi. Napenda kusikiliza kila kitu kinachozungumzwa ili hatimaye niweze kung'amua lipi la kufuata au kuchukua.

Kwa sababu hoja yako imejengeka katika kuhuisha mtandao wa wana CCM katika vyuo napenda kusema yafuatayo:
  1. Turuhusu rasmi siasa vyuoni. Ikumbukwe wakati wewe unapendekeza kuwepo mtandao imara wa wana CCM wanafunzi watakaotumika kutoa taarifa za maendeleo na/au mafanikio ya chama pamoja na vikwazo vyake, Mawaziri wanaohusika na elimu ya juu wamekuwa wakitishia kuzima vuguvugu la siasa vyuoni. Nadhani pendekezo la kuimarisha siasa vyuoni linatakiwa liambatane na mabadiliko ya sera zetu za utumishi wa umma, pamoja na sera za elimu. Tunapoamua CCM ni ruksa kufanya siasa vyuoni tusitegemee matokeo chanya kwa CCM, kwani kila chama cha siasa kitatumia mwanya huo kujiimarisha, na kwangu mimi kufanya siasa inatakiwa iwe haki ya kikatiba kwa mtu yeyote mwenye UMRI WA MIAKA 18+.
  2. Tulifikirie Taifa letu. Bwana Nchemba wewe ni mchumi kitaaluma na unafahamu vigezo mbalimbali vinavyotumika kupima maendeleo ya nchi. Kwa umaskini wa taifa letu na watu wake, ni vizuri kuwa na mikakati isiyobagua kama tunataka kuendeleza taifa letu na watu wake. Kuwa na mikakati ya pro-CCM au kupinga CDM hakuna maana sana kama hakuleti maendeleo. Siasa safi ya Nyerere ililenga kuwaondolea Watanzania maadui ujinga, maradhi na umaskini. Tunataka vijana watumike kupambana na hao maadui kwa akili zao zote, kwa nguvu zao zote na kwa moyo wao wote. Vijana wa sasa tunawatumia vibaya kwa kuwapa sime na mapanga ili wachinjane. Hata hivyo ukweli ulio mchungu kabisa ni kwamba sime hizo hizo zitaturudia wenyewe. Tutapitaje kwenda nyumbani kwetu katikati ya njia iliyojaa vijana ambao ni maadui zetu kwa sababu tu wana itikadi tofauti na sisi?
  3. Serikali siyo chama cha siasa. Pendekezo la wizara za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya kazi zake kwa mtazamo wa chama tawala kwa kuainisha ni vijana wapi wanachama wa CCM siliafiki. Japo sina takwimu sahihi, lakini naelewa ni Watanzania wachache sana (kama 18%) ambao ni wanachama wa vyama vya siasa vilivyosajiliwa nchini Tanzania. Ikumbukwe kwamba hata pale mfumo wa chama kimoja ulipokuwa umetamalaki na ilikuwa ni mandatory kuwa mwanachama wa UVT unapokuwa shuleni (sekondari), bado kuna Watanzania ambao tulikataa kuwa na kadi za UVT (Umoja wa Vijana Tanzania). Kwangu mimi nilikataa kulipia kadi hiyo kwa sababu UVT lilikuwa ni kapu la wote, hata wale waliokuwa vinara wa kutesa fomu wani (FORM I) walikuwa ni wanachama wa UVT, ambayo ekichware ndiyo hii UVCCM ya sasa.
  4. Tujifunze kufanya siasa bila kutukana. Leo ninapokutana na vurugu na kampeni za matusi pamoja na bunge dhaifu sishangai kwa sababu walioshikilia usukani ni wale wnaoamini katika vurugu na kampeni za matusi (unaweza kurejea hotuba ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Ndg Lusinde aliyoitoa kwenye uchaguzi mdogo Jimbo la Arumeru Mashariki). Napenda kuisikiliza hotuba ya Lusinde, hata ninapopata mgeni huweka hotuba hiyo ili tujikumbushe juu ya aina ya viongozi tulionao kwenye taifa letu. Anajisifu kwa kutukana, na sijasikia kanyo lolote toka kwa viongozi waandamizi, kwa hiyo aliyoyatamka aidha walimtuma au alipanga kuyatamka na alipoyatoa kwenye hadhira ile ya Arumeru viongozi wote wa chama (Bw Nchemba sijakutaja) wakakubaliana nayo. Niaposema tuache kutukana namaanisha hata ndani ya CCM matusi yamekuwa mikakati ya ushindi (wenyewe mnaita KUCHAFUANA).
  5. Siasa si ngoma za chagulaga (BENI, PUBA). Mimi ni msukuma. Mojawapo ya ngoma zenye ushindani mkubwa sana katika jamii ya wasukuma ni ile inayoitwa beni. Ngoma hii hushirikisha vikundi vyenye itikadi tofauti kama vile Bagalu, Bagika, Bayeye. Baada ya ngoma kumalizika vijana hufukuzia wasichana kwa kuwakamata na kuanza kuwatongoza kwa zamu. Hivyo msichana hulazimika kuchagua kijana mmoja mmoja ambaye hutumia nafasi ile kujenga hoja kwa nini yeye anafaa 'kutoka' naye. Kwa upande wa uchezaji wa ngoma zenyewe uchawi hutumika kwa kiwango cha juu ili kujipatia ushindi. Lakini baada ya ngoma mashabiki hubaki salama wakiendelea kushirikiana katika kazi za maendeleo kama vile kutayarisha mashamba, kupanda, kupalilia, kuvuna, kupiga mtama au kutayarisha matobolwa, n.k. Najiuliza mbona kwenye siasa tunashindwa kuimarisha umoja wetu? Hivi hatuwezi kushindana bila kupigana? Tukifanya siasa za kistaarabu tutakosa kitu gani? Au kwa kufanya siasa za hovyo kama hizi tunapata nini?
  6. Kutembelea wanavyuo na wanafunzi wa sekondari. Zamani ofisi za serikali za wanavyuo na serikali za wanafunzi wa sekondari zilikuwa ndo ofisi za chama. Je, itawezekana kuwa na ofisi ya CCM ndani ya jengo la chuo kama ilivyo kwa ofisi ya serikali ya wanafunzi? Suppose hakuna, utaratibu wa kukutana na wanafunzi wa vyuo utafanyikaje? Wale wa sekondari je, walimu watakuwa 'FAIR' na kuruhusu kuahirisha vipindi ili wanafunzi wakutane na wanasiasa toka CCM au TLP? Sera zetu za Taifa zinasemaje?

Bw Nchemba niishie hapo kwa sababu naona kila hoja uliyotoa imeacha maswali mengi kuliko majibu.
 
hivi mavi ukiya pulizia pafyumu nini hutokea...ccm tumewachoka mmetuibia vya kutosha na hatuoni wa kuibadilisha mavi kuwa mandazi..

kwa kuwa wewe ni mavi hebu jipulizie pafyumu halafu utupe jibu,nini kitatokea.tupo hapa tunakusubiri we divi
 
Back
Top Bottom