Mwigulu Nchemba kuongoza Wizara ya fedha ni pigo kubwa kwa Wafanyabiashara na Walipa kodi

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,377
217,438
Wakuu naomba kutangaza kwamba ninayo maslahi kwenye suala hili maana mimi ni mfanyabiashara wa ndani na nje ya nchi , ni mlipa kodi

Kwa takribani miaka sita sasa Sisi wafanyabiashara wa nchi hii tunahenya , makadirio ya kodi kubwa , vitendea kazi tunavyoagiza kutoka nje ya nchi zikiwemo matirio za kutengenzea bidhaa kodi tunayotwangwa kwenye bandari ya Dar es Salaam haina urafiki wowote ule , kwa ujumla Wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo ambao ndio walipa kodi wa kutegemewa kwenye nchi hii Wamegeuzwa kuwa maadui , hakuna asiyeelewa hiki ninachoandika hapa , hela zetu zimeng'olewa kwenye akaunti za benki bila hata maelezo yoyote .

Kwa mtu katiri na mwenye mihemko na visasi kama Mwigulu kupewa Wizara hii ni pigo kubwa kwa wafanyabiashara , wenye viwanda , wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa nchini , kuna hatari ya vyuma kukaza zaidi .

Wizara hii muhimu ilihitaji Waziri msikivu asiyejikweza kwa kiburi cha madaraka , inahitaji waziri atakayekaa na wafanyabiashara na anayeamini katika majadiliano , ingekuwa vema Waziri wa fedha atokane na Walipa kodi wanaofahamu ugumu na umuhimu wa kulipa kodi , huyu Mwigulu hajui lolote kuhusu mambo haya , ataleta shida zaidi .

Itaendelea ........
 
Back
Top Bottom