Mwigulu Nchemba kiepuke kikombe hicho mapema vinginevyo jumba bovu linaenda kukuangukia wewe

jitombashisho

JF-Expert Member
Jun 11, 2020
667
2,242
Tanzania inaenda kushuhudia anguko kuu la makusanyo ya kodi ambalo limeruhusiwa kwa makusudi na kiongozi wa Nchi kisa eti kuwabembeleza wafanyabiashara.

Bila kuwa na maono mkuu wa Nchi amedai hata makusanyo yakipungua kwa miezi mitatu ama miwili halipo tatizo huku akitabiri makusanyo kupanda juu baada ya wakati huo wa mpito jambo ambalo kwa sera na uhalisia wa wafanyabiashara wetu ni vigumu kutimiza wajibu wao ki hiari.Na hapo ndipo anguko la Mwigulu Nchemba litapoanzia.

Ndugu yangu Mwigulu natambua wewe ni mtu wa fursa lakini kwa hilo anguko lijalo la makusanyo ya kodi litapelekea uangushiwe jumba BOVU huku ukilaumiwa umeshindwa kuisimamia mamlaka ya kukusanya kodi vyema na hapo utafutwa kazi.

Tafadhari,jiepushe na kikombe hicho mapema.
 
Mkuu jitombashisho awamu hii utajito...!

Threads zako zinaonesha umebanwa awamu hii, umeanza na mguu mbovu.





 
Katika wizara zote wizara yenye kazi ngumu ni wizara ya fedha na Mipango

Mwigulu kazi anayo sio siri

Ugumu wa nini? Kama ni ngumu mwambie Mwigulu atoke ili wanaoweza hiyo kazi wafanye, na mambo yatasonga tu.
 
Back
Top Bottom