Mwigulu Nchemba hongera lakini Kuwa Polisi haitaleta mabadiliko ya Kilimo nchini

meddie

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
434
125
Kilimo bado ni uti wa mgongo kiuchumi hapa nchini lakini bado kunauduni kifikra, kiutendaji na kiusimamizi wa shughuli za kilimo nchini! Nasema haya kwa ufupi, kwa sababu hii kuu; bado kuna-gap kubwa kati ya Wizara ya kilimo na sera zake na mkulima na shughuli zake kule kijijini. Ndugu waziri na wizara yako na serikali hii ya Magufuli nakushaurini ku-review system mzima ya usimamizi na uendeshaji shughuli za kilimo nchini na kuondoa gap katiya wizara ya kilimo na mkulima. Kwa sasa bado mkulima anajiendeshea shughuli zake bila muongozo na msaada mkubwa kutoka katika wizara husika au msaada kutoka taasisi za utafiti chini ya wizara. Mabwana shamba ni kama wametupwa tu huko vijijini kuchukua dhamana ya wizara wakati wao hawana mshikamano wowote na wizara ya kilimo bali wapo chini ya Tamisemi . Mabwana shamba wengi hawana update ya new innovations zinazojili. Unakuta Bwana shamba ana miaka mitano, kumi au zaidi toka ametoka/amemaliza chuo cha kilimo na hapo ndio unakuwa mwisho wa mshikamano kati yake na wizara ya kilimo! Sasa anakuwa chini ya Mkurugenzi wa Tamisemi! Hili ni tatizo na bado kunamatatizo mengi yanayohitaji umakini katika kupatiwa ufumbuzi ilikuweza kuleta mabadiliko tarajiwa ya kilimo nchini.

Mweshimiwa waziri nakupa hongera kwa namna ya utendaji wako katika kipindi hiki kifupi, utendaji wa kipolisi! Ila napenda kushauri pamoja na huo upolisi kuna haja ya kubadili mambo…siyo kubaki na business as usual! Kunahaja ya ku-review usimamizi na utekelezaji wa sera za kilimo. Kipimo kikuu cha mafanikio yako na wizara ya kilimo kiwe idadi ya vijana wanaojiajili katika kilimo na ongezeko katika uzalizaji! Hii inawezekana kufikiwa kama kilimo kitaonekana kuwa na tija na kuwepo urahisi wa kupata msaada!
 
Back
Top Bottom