Mwigulu Nchemba: Hakuna mwananchi atakayelipa mkopo, Serikali italipa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,176
103,656
"Hakuna siku Mtanzania mmojammoja atagongewa hodi mlangoni kwamba tunakudai Shillingi hizi kwasababu Nchi yako ilikopa, haipo Nchi hiyo, hivi ni vitu vya Kitaasisi na vinaangaliwa kutoka kwenye mapato ya Kiserikali"

"Hakuna siku Mtanzania atafuatwa aambiwe wewe una ng'ombe wengi sana toa mmoja tulipie deni la Taifa haipo siku hiyo, inalipiwa kwenye mapato ya Serikali"——— Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Mwigulu Nchemba mbele ya Rais Samia Ikulu,Dar es alaam leo.

My Take
Nchi yangu ina bahati mbaya kuwa na mawaziri "cheap" kiasi hiki. Hivi hizi kodi tunazolipa si ni zaidi ya hodi?
 
Pointeless !!! Hizo hela zinazotumika kulipia hayo madeni kupitia makato ya kodi/tozo/ushuru n.k. zinatoka wapi !!!??? Wananchi sio wajinga kama ambavyo baadhi ya watu wanavyofikiri au kujiaminisha.
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr Mwigulu Lameck Nchemba (PhD) leo amewaondoa wasiwasi wananchi wanaolia kwa sababu ya ukubwa wa deni la taifa (Trilion 70+) kwamba hakuna mtanzania hata mmoja atakayegongewa mlango au kutakiwa kutoa mali zake binafsi ili kulipia deni la taifa. Amesema deni hilo litalipwa na serikali yenyewe kwa fedha zake bila mwananchi yeyote kutakiwa kutoa hata senti moja ili kulipia deni. Msikilize wewe mwenyewe kwenye klipu hii hapo chini 👇 👇 👇 👇 👇​

Dr Mwigulu alisema hayo wakati Rais Samia alipokuwa akihutubia Baraza la Mawaziri ikulu Jijini Dodoma ili kuweka mambo sawa baada ya Spika wa Bunge kuwa mbogo kuhusiana na ukubwa wa deni la taifa ambapo Spika alisema kuwa serikali ya Samia isipokuwa makini kwenye ukopaji, ipo siku nchi hii itauzwa ili zipatikane fedha za kulipia madeni.

MAONI YANGU
Nawaomba wananchi tutulie, tuache kupapalika bila sababu kwa kuwa sasa tumehakikishiwa kwamba hatutahusika hata chembe kwenye ulipaji wa deni la taifa. Nawashangaa sana watu wanaowapotosha wananchi kwa makusudi kuwa watahusika kwenye ulipaji wa deni la taifa huku wakijua fika kwamba serikali itajilipia yenyewe deni lake. Tuache upotoshaji ndugu watanzania. Kuna makundi ya watu wabaya wanaotumiwa na watu wasioitakia mema nchi hii kuifarakanisha serikali na wananchi wake. Tuwe makini! ✍️​
 
Wadau naomba kufahamu kama Tozo ni jambo la Muungano.
Kwani nimemskia Waziri wa Fedha Bw. Mwigulu Nchemba akidai kuwa kwa Mwezi wa Dec 2021. Zanzibar imepelekewa Bil. 161Tshs ili hali Bara Tshs Bil 91. Ina kuweje Pesa za Walipa kodi wa Bara ziende Zanzabar? Zanzibar ina watu wake wa kulipa Tozo. Inakuweje hii? Je ina maana kila mwezi Pesa za Bara zina pelekwa Zanzibar? Au ndio kujipendekeza bila kujali Sheria, taratibu na misingi ya Muungano pamoja na Sera za Fedha?
 
ULisikia vyema yaani watu 1mil wapelekewe 161bil alafu watu 61mil wapewe 91bil?
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dr Mwigulu Lameck Nchemba (PhD) leo amewaondoa wasiwasi wananchi wanaolia kwa sababu ya ukubwa wa deni la taifa (Trilion 70+) kwamba hakuna mtanzania hata mmoja atakayegongewa mlango au kutakiwa kutoa mali zake binafsi ili kulipia deni la taifa. Amesema deni hilo litalipwa na serikali yenyewe kwa fedha zake bila mwananchi yeyote kutakiwa kutoa hata senti moja ili kulipia deni. Msikilize wewe mwenyewe kwenye klipu hii hapo chini 👇 👇 👇 👇 👇

Dr Mwigulu alisema hayo wakati Rais Samia alipokuwa akihutubia Baraza la Mawaziri ikulu Jijini Dodoma ili kuweka mambo sawa baada ya Spika wa Bunge kuwa mbogo kuhusiana na ukubwa wa deni la taifa ambapo Spika alisema kuwa serikali ya Samia isipokuwa makini kwenye ukopaji, ipo siku nchi hii itauzwa kwa sababu ya ukubwa wa madeni.

MAONI YANGU
Nawaomba wananchi tutulie, tuache kupapalika bila sababu kwa kuwa sasa tumehakikishiwa kwamba hatutahusika hata chembe kwenye ulipaji wa deni la taifa. Nawashangaa sana watu wanaowapotosha wananchi kwa makusudi kuwa watahusika kwenye ulipaji wa deni la taifa huku wakijua fika kwamba serikali itajilipia yenyewe deni lake. Tuache upotoshaji ndugu watanzania. Kuna makundi ya watu wabaya wanaotumia na watu wasioitakia mema nchi hii kuifarakanisha serikali na wananchi wake. Tuwe makini! ✍️
Dah DR inakuwaje tena uchumi wa wapi huu mlipa deni ni mwananchi kupitia kodi za kila siku.
Zinatumika zaidi ya 800bil toka kwenye kodi yetu kulipa madeni sasa unasemaje kuwa mwananchi hatawajibika kulipa deni.
Uchumi wa wapi huu jamani?
 
ULisikia vyema yaani watu 1mil wapelekewe 161bil alafu watu 61mil wapewe 91bil?
Kweli kabisa mkuu. Hata MwanaHalisi Online imeandika pia. Swali la Msingi. Tozo ni kodi mpya ya Simu. Wizara ya Fedha siyo ya Muungano. Watu mil1 wa Zenj watozwe zao. Na sisi mil 60 tutozwe kwa maendeleo yetu. Ratio ni ileile. Why pesa za Bara ziende Zanzibar?

Walikomaa Zanzibar ikope kama nchi. Wameruhusiwa tiyar. Ni kwa nn pesa za Tanganyika Ziende Zanzibar?
 
Kama ni kweli basi kuna upande mmoja wa Muungano ni .................au basi nsije tukana bure
HI ratio ya wapi hii wachache wapewe kingi alafu wengi wapewe kichache
 
Kama ni kweli basi kuna upande mmoja wa Muungano ni .................au basi nsije tukana bure
HI ratio ya wapi hii wachache wapewe kingi alafu wengi wapewe kichache
Haitakiwi kupewa hata shs1. Hii ni tozo. Ratio ni ileile. Zanzibar ina watu wake sijui mil 2. Bara ina watu wake Mil 60. Why pesa za tozo za simu za Bara ziende Zanzibar? Hii maana yake wao wana faidi mara 2.
 
Back
Top Bottom