Mwigulu Nchemba, Gereza la Uyui Mkoani Tabora linahatarisha usalama wa Raia wema

Mpangawangu

JF-Expert Member
Mar 5, 2014
887
965
Heshima kwenu wakuu.
Naomba kwa yeyote mwenye mawasikiano ya karibu na waziri wa mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba amtaarifu yafuatayo.

Gereza la Uyui lililopo Tabora mjini linatiririsha Vinyesi vya wafungwa na familia za watumishi mita 30 kutoka lilipo soko la wakulima maarufu kama soko la Darajani.

Ukiwa sokoni ni harufu ya Mavi mabichi yanayomwagika kwenye Chemba ambayo ameziba na hatimae kusambaa.

Pamoja na Vinyesi hivyo kuwa kero kwa wananchi hasa wajasiliamali,pia ni kero kwa wakazi wa mitaa ya Mwanzo,Bomba Mzinga,Isevya na Maeneo ya Kidatu nguzo ya Kwanza na ya pili.

Chakula hakiliki kutokana na harufu kukithiri.

Kwa kifupi hali inatisha na sasa ni miezi mitatu watu wanapiga kelele warekebishe Chemba ili Kinyesi kiingie dampo.

Hata hivyo viongozi wa Magereza hawanyunyizi dawa ili kupunguza harufu kwenye makazi hayo ambayo kwa sasa imekuwa zaidi ya adhabu kwa wananchi.

Naombeni tafadhali wana Jamiiforums muufikishe huu ujumbe kwa Mwigulu Nchemba ili atoe agizo ili kuepusha na Magonjwa ya Mlipuko ambayo yanaweza kuangamiza wananchi wasio na hatia.

Shukran kwa Kutufikishia ujumbe huu kwa Mwigulu.
 
nemc, januar makamba, wizara ya afya.... wanasubiri hadi kipindupindu kifumuke.... au tume ya haki za binadamu wafungue kesi mahakamani....
 
Wape taarifa NEMC Gereza KEKO walikula Faini kwa masuala kama Hayo...
 
Bora wamesahihisha, uliandika kama vile yeye ndio ameyatamka hayo yako.

Naamini watashughulikia
 
Back
Top Bottom