Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
Ushauri kwa:-
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI Mh. Mwigulu. L. Chemba.
Pole na majukumu mengi ya kikazi, najua unafanya kazi wizara ngumu kidogo, pole.
Historia inatuonesha kuwa kwa muda mrefu kumekuwa na migogoro kati ya Wakulima na Wafugaji na hata kufikia wengine kuchinjana kama wanyama kisa mwingiliano. Japo Mimi Deogratius Kisandu bado niko vizuizini eti nitapindua nchi, OK, nimekubali kufa njaa. Lakini naomba nitoe ufumbuzi jinsi tunavyoweza kutatua mgogoro huu kwa amani, sasa nini kifanyike?:-
1. Nenda MKOA husika na team ya Wazee wenye Busara na vijana wenye hekima jumla yao iwe 10, angalia pia jenda.
2. Waagize Ma DCs wote wa MKOA husika wakusanye watu wafuatao: Watendaji wote WA kata wilaya nzima, mabwana shamba wote WA kata wilaya nzima, mabwana mifugo wote WA kata wilaya nzima, Maafisa ardhi na Maafisa mifugo wote WA wilaya. Na mkurugenzi.
3. Wawakilishi WA wakulima na wafugaji walau 6 kila wilaya, viongozi wa asasi za wafugaji au wakulima.
4. Tafta ukumbi mkubwa katikati ya mji utakao tosha idadi ya hao wajumbe wote.
5. Mkutano huo uwe katika mtindo wa mdahalo na uchukue siku nzima. Sikiliza hoja za kila upande na mapendekezo yake ya kumaliza mgogoro.
6. Ajenda yetu iwe " Nini kifanyike ili Mkulima na Mfugaji waishi kwa Amani?"
7. Wachangiaji wapewe Uhuru mkubwa na wala wasitishiwe. Na suluhisho watoe wao wenyewe. Wewe uje kutoa ya mwisho tu na team yako.
8. Angalia usiwekewe watu ambao ni marafiki wa Ma DC au wana CCM, Bali chukueni walengwa, msiweke uchama hata kidogo maana ni swala zito la kijamii.
9. Wakurugenzi wahusike na bajeti hiyo, kuanzia chakula na maji.
10. Issue nzima iwekwe kwenye video documents ili hata waziri mwingine anaweza kuapply mtindo huo kwenye mgogoro mwingine.
11. Nimechoka kukaa Detention kwa maslahi ya wapuuzi.
Deogratius Kisandu
2 Januari 2017.