Mwigulu Nchemba awachana wanaohoji deni la taifa

Mwigulu yupo sahihi Nape alikuwa anajikosha tu kwa wapinzani kiukweli kuna miradi mikubwa sana imefanyika sitaki kutaja sana mfano mmoja tu ni barabara, barabara zimejengwa kwa kiwango cha lami pamoja na madaraja makubwa mfano Morogoro mpaka mwanza hasa kupitia Bariadi Simuyu yaani barabara ilifumuliwa na kujengwa kisasa zaidi, makambako-Mbeya, Tabora to Nzega na Manyoni, barabara kuelekea kigoma ambako maendeleo yalidumaa kutokana na kotofikika kirahisi lakini saizi ni full mkeka kwa hiyo hao jamaa wa promo tuachane nao tu muda mwingine
Vipi value for money, maana Kuna kuongeza sifuri broo
 
Nape ni mnafiki na mjaa chuki ana hasira na jpm alimtumbuwa uwaziri
Mnafki sana huyo siamini kama ni yeye alienda kupiga magoti toka getini ikulu mpaka mbele ya JPM.
Leo marehemu hayupo ndio anaropokwa kwa nini hakusema wakati ule?
Aisee tumewajua wanafki wengi sana safari hii
 
Ndio, je, unaona ajabu? Pili tuliambiwa fedha zetu makusanyo ya ndani ndio anajenga miradi sasa kukopa na kujenga miradi nani anashindwa? Tulimuona jasili na shujaa kwa maelezo kuwa hakopi, sasa haya mambo gani hata mwanangu wa darasa la pili anaweza!
Kama huna uwezo wa kulipa mkopo utakopeshwa?
 
Waziri wa fedha Dk Mwigulu Nchemba amefunguka na kuwachana wanaohoji kukua kwa deni la taifa kuwa wasihoji kwa kukurupuka kama wamebambikwa mbali wahoji kwa kuangalia na miradi iliyotekelezwa kwenye kipindi hicho.
Nchemba amebaniinisha kuwa kuna maelfu ya miradi imetekelezwa nchini ikiwemo barabara za lami, umeme vijijini ,maji na Zahanati kila mahali kwa kutumia fedha hizo.

Huyu Mwigulu nae Ni MPOTOSHAJI mzuri Sana kwani anaogopa Nini ukaguzi kufanyika? Kwani Kama miradi imefanywa mingi si inajulikana na gharama zake kiasi cha pesa? Si aache mkaguzi apitie kila sehemu ndiyo aseme? Maana mtoa hoja mh Nape aliomba miradi ichunguzwe ifanyiwe ukaguzi na mkaguzi wa hesabu za serikali kujua Kama kiwango kilichokopwa kinalingana na matumizi yake? Kosa lipo wapi hapa mpaka mwigulu anakurupuka hivyo, anataka kuficha Nini kwa majibu hayo?
 
Nape ni nani zaidi ya kuwa msaka tonge!

Mwigulu kakwambia kwamba wanayo rekodi yote, sasa kwa nini asiiombe na aisome?

Nape ni muhuni na kwa hili amejiweka njiapanda ndani ya chama chake.

Aliyekuwa makamu wa rais wa awamu hiyo anayoituhumu Nape, ndiyo rais wa sasa.

Aliyekuwa waziri mkuu wa awamu hiyo anayoituhumu Nape, ndiye huyo huyo wa sasa.

Aliyekuwa waziri husika na fedha na mikopo yote awamu hiyo, sasa yupo ikulu.

Sasa huyo Nape wako anaposema awamu ya Tano ichunguzwe,je amejitathmini vizuri au ndiyo kukurupuka.?

Mdomo siku zote hukiponza kichwa.

Je tukiomba TAKUKURU ipitie ripoti ya kamati ya ukusanyaji na uhakiki wa mali za CCM huyo Nape wako atapona?

SI ndio hao walioomba kombe lifunikwe ili mwanaharamu apite?

Nani walihusika kuiza chanel Ten kwa wahindi kinyemela?

Na mitambo ya Tanzania Printpak iko wapi.
Tanzania Publshing House. Je?

Acheni kuropoka msiyo yajua!
Kwanini mkaguzi asioete kufanya ukaguzi kwani miaka yote madudu yanayoonekana serikalini anapopita mkaguzi kulikuwa hamna record zote? Acha kupotosha na kutetea ujinga mawazo ya nape Ni mazuri maana kwanza kwa awamu ya tano kumekuwa na sintofahamu nyingi Sana tumedanganywa serikali haikopi inatekeleza miradi kwa pesa za ndani huku Deni linakua CAG Alipojaribu kufumua madudu akapigwa chini kipuuzi kabisa Leo mnataka Nape apuuzwe Kuna Nini mnakilinda na mnapata Nini hasa ?
 
Waziri wa fedha Dk Mwigulu Nchemba amefunguka na kuwachana wanaohoji kukua kwa deni la taifa kuwa wasihoji kwa kukurupuka kama wamebambikwa mbali wahoji kwa kuangalia na miradi iliyotekelezwa kwenye kipindi hicho.
Nchemba amebaniinisha kuwa kuna maelfu ya miradi imetekelezwa nchini ikiwemo barabara za lami, umeme vijijini ,maji na Zahanati kila mahali kwa kutumia fedha hizo.

Si mwendazake alituambiwa hiyo miradi inatekelezwa kwa fedha za ndani?
 
ekani wanakopa na kujifichaficha na kudanganya kuwa hawakopi? Na je hiyo mikopo haipo wazi ama nayo ndio kama tufanyavyo sisi. Tena usitake kuleta uongo wako hapa juu ya Wamarekani wale jamaa ni wakweli sana linapokuja swala la miradi ya nchi.
Acheni propaganda ya mambo usiyoyajua... dunia kijiji. Kama hujui jambo nyamaza acha kusifiasifia tu mambo usiyoyajua... I must admit that, these people are on another level but still not all the time their staffs are wide open... do your research.

vijana tufanye kazi. Tuache uvivu, na ukizingatia jua kali now.
 
huyo mchora majabali apunguze jazba.

Uchunguzi wa deni la taifa ufanyike kwanza na matokeo yakishatoka ndiyo tutaona hiyo miradi imefanyika kwa kiasi gani.

MaCCM mengi ni matetezi ya ufisadi na yamepanic sana baada ya watu kuhoji kuhusu deni la taifa.
Mwigulu amemjibu Nape kisiasa sio kisomi. Kwa mfano, Mwigulu anasema sababu za deni la taifa kukua ni pamoja na umemem vijijini, lakini tunavyoelewa usambazaji wa umeme vijijini unatokana na levyy tunayolipa kwenye bill za umeme na grants nyingine, rural electrification haijawa funded na mikopo ya ndani au nje. Sasa haya ndio mambo yanahitaji ufafanuzi wa kitaalamu sio majibu mepesi mepesi ya kufokeana.
 
Mh
 
Waziri wa fedha Dk Mwigulu Nchemba amefunguka na kuwachana wanaohoji kukua kwa deni la taifa kuwa wasihoji kwa kukurupuka kama wamebambikwa mbali wahoji kwa kuangalia na miradi iliyotekelezwa kwenye kipindi hicho.
Nchemba amebaniinisha kuwa kuna maelfu ya miradi imetekelezwa nchini ikiwemo barabara za lami, umeme vijijini ,maji na Zahanati kila mahali kwa kutumia fedha hizo.

Afu wakisema jengo lile lina mazuzu wanachukia. Uchunguzi anaozungumzia nape ni kutaka kujua thamani ya miradi iliyofanyika na fedha iliyokopwa. Kama waziri kashafanya uchunguzi atujuze sio kutoa majibu ya juu juu tu
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom