Mwigulu Nchemba aumbuliwa na Waziri Nahodha Bungeni leo

Haki sawa

JF-Expert Member
Oct 3, 2007
4,780
3,208
Katika kipindi cha maswali na majibu leo asubuhi lilikuwepo swali la MBunge Mariam Msabaha wa CHADEMA aliyetaka kujua hatma ya mgogoro wa wanajeshi na wananchi huko Znz kuhusu ardhi, likafuatia la nyongeza la Ester Bulaya aliyetaka kujua hatima ya mgogoro wa wananjeshi na wananchi Kunduchi, baada ya majibu ndipo Mhe. Mwigulu aliuliza

'Ni kwanini serikali isihamishe kambi zote za jeshi maeneo ya mijini na kuzipeleka vijijini ambako kuna maeneo makubwa na hivyo migogoro itakuwa imeisha ......na alitaja eneo moja huko kwao Iramba kuwa linafaa kuwekwa kambi ya JWTZ '

Nahodha katika majibu yake alimjibu kuwa kambi za jeshi huwa hazianzishwi tu bila utaratibu bali hufanyika utafiti wa kina na wa kimkakakti katika maswala ya ulinzi kabla ya kufanya uamuzi wa kambi iwekwe wapi na iwe ni ya aina gani akimaanisha ya Vifaru, Kikosi cha anga ama ardhi na majini.

Hii ilikuwa aibu kubwa sana kwa mchumi namba moja ambaye ametoka JKT juzi hajui kuwa masuala ya ulinzi sio sawa na kuanzisha shhamba darasa Iramba kuwa unaangalia eneo lililopo theni unaanzisha shamba darasa .

Nimeona aibu sana kwa naibu katibu mkuu wa CCM ambaye hajui kuwa kambi za jeshi ni suala la kimkakati na hakuna nchi duniani eti mijini hakuna wanajeshi kwenye kambi .......Hao ndio viongozi wa CCM ya leo tutarajie nini kama sio maafa kwa taifa....
 
Mh mimi ningekuwa ni yeye, ningekaa kimya tu! Every eye on you! Hivi mtu unavyotajwatajwa na vyombo vya habari kwa muda mrefu kwa kuhusishwa na kashfa mbalimbali, hivi hata ukiwa nyumbani kwako utathubutu kuangalia TV sebuleni na familia yako? Kweli kwa hali kama hii, yataka sana moyo....
 
Yani kwenda jeshini wiki tatu tu ndiyo anaona tayari ameshalijua jeshi.
 
Mna wivu na mwigulu tuu.
Mwenye wivu naye nani Nahodha aliyemwambia kuanzisha kambi ya JWTZ sio sawa na kuanzisha shamba darasa au nani hasa? Maana kama Naibu katibu mkuu wa chama kinachotawala hajui maana ya kuanzisha kambi za jeshi kuwa ni suala la kimkakati huyu si ni mzigo hata kwa hicho chama na waliomteua?
Pia ukilitazama jibu la Nahonda kwa umakini utajua kuwa hamheshimu huyu jamaa hapa punje kwani angekuwa na punje ya heshima kwake walau angemjibu kuwa wazo halitekelezeki na kuishia hapo na sio kumpa vidonge kiasi kile
 
Wivu wa nini na mjinga bana unakuwa na wivu kwa mtu mwenye akili sas mwigulu duuuuu unamatatizo makubwa sana ndugu. We wa lumumba nini khaaaaaaaaaaaaa pole lakini
 
Kaibukia bungeni tena?
Vp ya kule Arush ina maana hajaenda hata kutoa pole kwa wapiga kura wa chama chake.
Ama kweli laana ya mauaji itammaliza huyu pimbi na ile midevu yake kaa stili waya.
 
Yalipolipuka mabomu mbagala akina Slaa na mbowe walikuwa wakwanza kuhoji kwanini kambi za kijeshi zinawekwa mjini wakaonekana majiniazi

Kahoji mwigulu the same thing anaonekana taahira.........,..what a double standard

Mapenzi ya vyama vyetu yasitupofushe upeo wetu wa fikra
 
Mwenzenu alitaka kambi kama ile ya Mbeya au ile ya kwao ndago ya wakati wa uchaguzi wa Igunga kwa ajili ya Green guard
 
sasa hapo kaumbuliwa vipi?
Yeye alitaka kambi zote za jeshi mijini ziondolewe na baadhi zipelekwe Iramba , sasa kajibiwa kuwa kuanzisha kambi sio sawa na kuanzisha shamba darasa huoni huko ni kuumbuliwa ? Katoka JKT juzi huyu hakujifunza hata mkakati wa kumpiga adui ?
 
Mwenzenu alitaka kambi kama ile ya Mbeya au ile ya kwao ndago ya wakati wa uchaguzi wa Igunga kwa ajili ya Green guard
Ohhh...kumbe alifikiri kambi za jeshi zinautaratibu kama za kwake kuwa unaangali popote ....pole zake na chama chake.
 
Yalipolipuka mabomu mbagala akina Slaa na mbowe walikuwa wakwanza kuhoji kwanini kambi za kijeshi zinawekwa mjini wakaonekana majiniazi

Kahoji mwigulu the same thing anaonekana taahira.........,..what a double standard

Mapenzi ya vyama vyetu yasitupofushe upeo wetu wa fikra

Slaa na Mbowe waliuliza kwa nini kambi za jeshi zinawekwa mijini karibu na makazi ya watu?
Kwa nini isekwae mwabepande, pugu ambapo hakuna msongamano wa watu.
 
Hii ilikuwa aibu kubwa sana kwa mchumi namba moja ambaye ametoka JKT juzi hajui kuwa masuala ya ulinzi sio sawa na [COLOR=#ff0000 said:
kuanzisha shhamba darasa [/COLOR]Iramba kuwa unaangalia eneo lililopo theni unaanzisha shamba darasa .

Nimeona aibu sana kwa naibu katibu mkuu wa CCM ambaye hajui kuwa kambi za jeshi ni suala la kimkakati na hakuna nchi duniani eti mijini hakuna wanajeshi kwenye kambi .......Hao ndio viongozi wa CCM ya leo tutarajie nini kama sio maafa kwa taifa....

...hahahhahaaaaaaa...mbavu zangu... mkuu Ritz njoo umuone kiongozi wako huku anazani jeshi ni kama kuanzisha bustani ya mchicha....
 
Last edited by a moderator:
Slaa na Mbowe waliuliza kwa nini kambi za jeshi zinawekwa mijini karibu na makazi ya watu?
Kwa nini isekwae mwabepande, pugu ambapo hakuna msongamano wa watu.

Nadhani suala hapa sio Dr. Slaa, mbowe wala vyama, jambo la msingi ni mikakati ya Kijeshi ya kuanzisha kambi za kijeshi ambayo ni lazima izingatiwe kulinga na mahitaji, sio kama huyu bwana anavyowaza kama vile unaweza kuamka na kuanza kuhamisha vifaru.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom