Mwigulu Nchemba aumbuliwa na Waziri Nahodha Bungeni leo

its called tactical combat deployment
Ukimuuliza ni kwanini kambi ya Vifaru iko Kibaha si ajabu akakujibu kuwa ni kutokana na kuwa karibu na bandari hivyo gharama za usafiri ni rahisi zaidi, ukimuuliza swali la pili mbona mabomu ya vifaru hayapo Kibaha atakwambia yamepelekwa mbali na mjini.........Mchumi wetu bana duhh.....
 
Yalipolipuka mabomu mbagala akina Slaa na mbowe walikuwa wakwanza kuhoji kwanini kambi za kijeshi zinawekwa mjini wakaonekana majiniazi

Kahoji mwigulu the same thing anaonekana taahira.........,..what a double standard

Mapenzi ya vyama vyetu yasitupofushe upeo wetu wa fikra

Kwahiyo ulitaka KAMBI ya jeshi ya kulinda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tanzania ipelekwe IRAMBA?
 
hapo hajaumbuliwa ila ameelekezwa tu utaratibu unaotumika kuanzisha kambi na wala hapi hakuna tatizo tena swali alilouliza ni la msingi sana kambi zinatakiwa zihamishiwe mbali na makazi ya watu ilikisudi hata inapotokea milipuko isilete madhara kwa raia
 
Mwenye wivu naye nani Nahodha aliyemwambia kuanzisha kambi ya JWTZ sio sawa na kuanzisha shamba darasa au nani hasa? Maana kama Naibu katibu mkuu wa chama kinachotawala hajui maana ya kuanzisha kambi za jeshi kuwa ni suala la kimkakati huyu si ni mzigo hata kwa hicho chama na waliomteua?
Pia ukilitazama jibu la Nahonda kwa umakini utajua kuwa hamheshimu huyu jamaa hapa punje kwani angekuwa na punje ya heshima kwake walau angemjibu kuwa wazo halitekelezeki na kuishia hapo na sio kumpa vidonge kiasi kile

Kama naibu katibu mkuu wa ccm anaweza kuambiwa na waziri wa chama chake kauli kama hio, ni wazi hapewi heshima yake kama bosi wa chama.Hii kwa nje zaidi inaonyesha ndani ya ccm kuna wanaokerwa na mwenendo wake katika siasa.
 
Slaa na Mbowe waliuliza kwa nini kambi za jeshi zinawekwa mijini karibu na makazi ya watu?
Kwa nini isekwae mwabepande, pugu ambapo hakuna msongamano wa watu.
Inamaana wote hawajui kuwa kambi za JESHI zinaanzia mbali na makazi ya watu ila miji inapanuka na mwisho wa siku watu wanawafikia.kamwe JESHI halianzishi kambi zake mjini chunguza kambi ya gongo la mboto ilianza lini utapata jibu kuwa pale lilikuwa ni pori na hawaishi watu.
 
Kwahiyo ulitaka KAMBI ya jeshi ya kulinda uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tanzania ipelekwe IRAMBA?

Kwa mfano air defence system ya dar inalindwa na missile unit nne,, moja kaskazini, kusini, mashariki na magharibi.these units are squarely placed at fixed angle and distance kutegemea area coverage ya radar na missile range..., sasa ukihamisha hata unit moja tayari anga linakua na air gap.missile zinazolinda hapo dar ni petchora c 125 complex guided missile system.its russian, petchora means mshale.at all moments they are on launchers, utazihamishaje sasa
 
swali la kawaida sana hilo na limeshaulizwa mara kibao na wananchi wengi wala comred mwigulu lameck madelu nchemba, jembe la kiumeni sio wa kwanza kuliuliza. hongera mwigulu kwa kazi nzuri ya kupukutisha magaidi sasa hata ukienda kuoga yanakujadili
 
Katika kipindi cha maswali na majibu leo asubuhi lilikuwepo swali la MBunge Mariam Msabaha wa CHADEMA aliyetaka kujua hatma ya mgogoro wa wanajeshi na wananchi huko Znz kuhusu ardhi, likafuatia la nyongeza la Ester Bulaya aliyetaka kujua hatima ya mgogoro wa wananjeshi na wananchi Kunduchi , baada ya majibu ndipo Mhe. Mwigulu aliuliza

'Ni kwanini serikali isihamishe kambi zote za jeshi maeneo ya mijini na kuzipeleka vijijini ambako kuna maeneo makubwa na hivyo migogoro itakuwa imeisha ......na alitaja eneo moja huko kwao Iramba kuwa linafaa kuwekwa kambi ya JWTZ '

Nahodha katika majibu yake alimjibu kuwa kambi za jeshi huwa hazianzishwi tu bila utaratibu bali hufanyika utafiti wa kina na wa kimkakakti katika maswala ya ulinzi kabla ya kufanya uamuzi wa kambi iwekwe wapi na iwe ni ya aina gani akimaanisha ya Vifaru, Kikoso cha anga ama ardhii na majini,

Hii ilikuwa aibu kubwa sana kwa mchumi namba moja ambaye ametoka JKT juzi hajui kuwa masuala ya ulinzi sio sawa na kuanzisha shhamba darasa Iramba kuwa unaangalia eneo lililopo theni unaanzisha shamba darasa .

Nimeona aibu sana kwa naibu katibu mkuu wa CCM ambaye hajui kuwa kambi za jeshi ni suala la kimkakati na hakuna nchi duniani eti mijini hakuna wanajeshi kwenye kambi .......Hao ndio viongozi wa CCM ya leo tutarajie nini kama sio maafa kwa taifa....

Economist Last Class
 
Back
Top Bottom