Mwigulu Nchemba aomba radhi kufuatia Polisi kutumia nguvu kubwa kupambana na watu wenye ulemavu

Kwani hao walemavu walikuwa wanaandamana kudai nini???
Huna point mkuu kuandamana ni haki yao kikatiba na polisi kazi yao ni kuwalinda waandamanaji. Mapolisi wetu hawajui kabisa kazi yao wao wanadhani ni mahakimu. Nchi za wastarabu hana kama mtu kashikwa anaua kama hapingi kuwekwa chini ya ulinzi anashughulikiwa kistaarabu na chai anapewa maana kwa wakati ule siyo mhukumiwa anakua mtuhumiwa.
 
Mlemavu anapoamua kutumia njia za kiuwanaharakati kudai haki yake anategemea nini?
Sasa wana silaha?? Wamepigana na dola?? Wwe mtu hta silaha hana wala nguvu za kukimbia virungu vya nni?? Kwani mlishindwa kumkamata tu kistaarabu?? Dah nchi hii kwa wenzetu wangejiuzulu ila kwa linchi letu yasema TUMESHAONGEA KUTAFUTA SULUHU...... sasa walioumizwa watakuwa compensated vp!!! Waziri hasemi afu nyie mnashabikia

Mwiguli ur days are numbered kwenye equation umebaki wwe na january
 
Anaomba radhi wakati mkuu wa polisi anae kaimu kasema walemavu pia wanatakiwa kufuata sheria. Hivyo jeshi la polisi lilistahili kuchukua hatua dhidi yao.
Kama waliweza kuwapiga mabomu watoto wa shule ya msingi itakuwa walemavu???
 
Inafurahisha, wananchi mnafanyiwa vitendo vya kihuni, baadaye waliofanya uhuni wanakuja kuomba msamaha, ukurasa unafungwa. But they do not stop, they do the same in a different fashion, again after public outcry wanajifanya wanaomba msamaha wakati watu tayari wameumia.
Watanzania tuwe na kumbukumbu.
 
Yes,Mbase kuandamana ni haki iliyondani ya katiba,ila polisi wa nchi yetu wapo kama miungu watu,hakuna sharia inayowapa uhuru wa kupiga raia,inatia hasira mno eti waziri anaomba radhi na yanaishia pale,mbona haelezi hatua zitakazochukuliwa dhidi ya wale polisi?

Na hii ndio baada ya muda polisi wa Tanzania wataangaika mno kupata taarifa muhimu maana wanajenga ukuta baina yao na raia,polisi bila ya ushirikiano na raia utendaji wao utayumba ndio tunayoyaona sasa pale kibiti,hakuyna trust between civilians na polisi. Time will tell
 
Mlioshabikia vitendo hivyo sasa mnapiga u turn,"wafuasi wa ccm ni shida,mpaka viongozi wao waone na kufanya nao ndio wanabadili uelekeo"
Tulipiga juu ya jambo hili ila ccm wengi mliona ni sawa!
 
Ni aibu pia Kwa Polisi kama ingekuja thread humu kuwa Polisi wameshindwa kuwaondoa Walemavu.
Sio kwamba Polisi wafanye ili waonekane hawajashindwa, pale kazi isingeshindikana lakini wameshindwa kutekeleza kazi yao kulingana na watu wanaokabiliana nao.

Mlemavu hana miguu amekaa chini halafu unamshushia kirungu kwenye sehemu ya mwili ambayo pia haijakamilika(jinsi video inavyoonesha), wengine wanaburuzwa kama chini utadhani furushi la takataka. Hata kama wanatekeleza agizo la mamlaka husika kazi wanayoifanya ni ujinga mtupu kutotumia akili, maana hata macho hawajaona wanamuwajibisha mtu wa aina gani!

Wangetumia maneno kuwaamrisha bila kuwapiga zoezi lingefanikiwa, Najua polisi wetu kila jambo wanalolifanya wanajua kutumia nguvu ndio suluhu jambo ambalo ndio linawajengea sifa tunazoziona na chuki miongoni mwa jamii.

Kwa kitendo walichokifanya ni laana kubwa sana.
 
Polisi walipokamata waandishi wa Habari Arusha mliomba Radhi hivihvi lakini hakuna Hatua zilizochukuliwa..
 
Malipo ni hapa hapa duniani na niniyi wenye mamlaka na kujiona miungu watu hakika mtalipwa sawasawa na matendo yenu na bado adhabu ya ahera.

Huwezi kufanya makosa ya kipuuzi na kipumbavu yanayogharimu maisha ya watu so simple useme tena kwa kiingereza na unpolitely eti I apologize what???

Kulikuwa kuna sababu gani na ipi ya msingi hawa polisi kutumia nguvu kiasi kile au mnadhani Watz.wote ni wajinga????

Kwa nchi nyingine Kiongozi na wahusika au washirika wake lazima wawajibike tena kwa vitendo vikali not these blabla in Tz. that is happening.

Awamu hii pame kuwepo na matumizi makubwa na mabaya kwa vyombo vya dola,na sijui mnaandaa kizazi cha aina gani kama siyo chuki na visasi.

Surely for beyond very SILLY mistakes not unwillingness says I apologize without an intensive disciplinary measures has been taken to the all concerns????

The missuse of power to the dissabilities people and abilities people to this era is beyond huge.

Anyway Time will tell and every thing that has the source must has the end,the only issue is we don't know when and how it'll be.
 
Wamekuwa na tabia kuomba radhi baada ya kufanya kosa. Kwanini wasiwachukulie hatua askari hao?

Wa naomba radhi Lakini baadae wanaanza kujidai kuwa wamewaweza. Kuna Kiongozi nimemwambia japo hilo akasema halina tija katika ujenzi wa Uchumi, nikamwambia tunawasubili mkija kwetu kuomba KURA
 
Huna point mkuu kuandamana ni haki yao kikatiba na polisi kazi yao ni kuwalinda waandamanaji. Mapolisi wetu hawajui kabisa kazi yao wao wanadhani ni mahakimu. Nchi za wastarabu hana kama mtu kashikwa anaua kama hapingi kuwekwa chini ya ulinzi anashughulikiwa kistaarabu na chai anapewa maana kwa wakati ule siyo mhukumiwa anakua mtuhumiwa.
Hujamwelewa,anasupport kile polisi walichofanya!Kwamba ingekuwa aibu kwa polisi kutowapiga hivyo kushindwa kazi!
 
Ndio shida ya kupeleka waliofeli form four kwenye jeshi letu la polisi
 
Ameomba vp radhi wakati kaimu kamanda ameshasema walikuwa sahihi.....
 
Back
Top Bottom