Mwigulu Nchemba aomba radhi kufuatia Polisi kutumia nguvu kubwa kupambana na watu wenye ulemavu

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,305
2,000
Waziri wa Mambo ya ndani na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mkoani Singida, Mwigulu Nchemba leo bungeni amefunguka na kuomba radhi dhidi ya vitendo vya jeshi la polisi kutumia nguvu kubwa kupambana na watu wenye ulemavu.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba.


Mwigulu Nchemba amekiri kuwa jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa mno kwa watu hao na kusema serikali wamepokea jambo hilo na kuahidi kulifanyia kazi ili siku nyingine lisijirudie.

"Kwanza naomba niombe radhi kwa jambo hili na naomba salamu zangu ziwafikie watu wenye ulemavu, ni kweli kwamba kwa kuzingatia hali yao jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa, ila sisi kama serikali tumeshawasiliana na TAMISEMI na kuzungumza nao juu ya mambo yao, lakini pia tumepokea jambo hili na tunalifanyia kazi ili siku nyingine jambo hili lisijirudie" alisema Mwigulu Nchemba

Mnamo tarehe 16, Juni, 2017 jijini Dar es Salaam jeshi la polisi lilitumia nguvu kubwa ikiwepo kuwapiga na kuwadhalilisha watu wenye ulemavu ambao walikuwa wamejikusanya katika barabara ya Sokoine, Posta Jijini Dar es salaam ili kwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, kuwasilisha malalamiko dhidi ya askari wa usalama wa barabarani kuwakamata na kuwazuia kuingia katika jiji. Lakini pia walikuwa wakipigania haki yao ya kuwa na maeneo ya kuegesha vifaa vyao katikati ya jiji.

WAZIRI ANAOMBA RADHI KUFUATIA POLISI KUTOFAUTIANA NA WALEMAVU

Tii sheria bila shuruti.

 

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,305
2,000
Ni aibu pia Kwa Polisi kama ingekuja thread humu kuwa Polisi wameshindwa kuwaondoa Walemavu.
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
30,918
2,000
Dah ila nchii hii Bhana yaani mlemavu ambaye hata kukimbia hawezi ndio unampiga hivo kana kwamba amekataa kukamatwa??? Yaani wangetumia hasira hizi kuwasaka magaidi wa kibiti naona mauaji yangekuwa yameisha zamani sana
Mlemavu anapoamua kutumia njia za kiuwanaharakati kudai haki yake anategemea nini?
 

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
3,705
2,000
Ukiangalia video u hao polisi wakiwapiga hao walemavu, unapata shaka juu ya kile wanachojifunza pale ccp. Ni mfano wa uharamia usio na chembe ya utu. Kuna haja ya kupitia upya kile wanachofundishwa huko ccp
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,618
2,000
Ni aibu pia Kwa Polisi kama ingekuja thread humu kuwa Polisi wameshindwa kuwaondoa Walemavu.
We naye acha unafki siku ile wanapiga wafuasi wa CUF pale mtoni mtongani wwe mbona ulisifia kuwa watii sheria bila shuruti and all that!!!! Cku ile kina lembeli wakafurumushwa na virungu na mabomu kule kahama mbona hukutetea au kuumizwa?? Leo hii ndio unaona polisi inatia aibu ila akisema lema na lisu unawakejeli ila kwakuwa mwigulu kakiri kukosea wwe naye ndio unajifanya umeguswa???? Acha unafki mkuu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom