Mwigulu Nchemba anafuatilia changamoto za Jimbo lake kwa ukaribu mkubwa

KHALFANI 86

Member
May 16, 2020
14
24
Kifupi nimejaribu kuangalia kwa nini bado Ndugu MWIGULU LAMECK NCHEMBA ana mvuto kwenye jimbo la Iramba Magharibi tangu kuwapo mwaka 2010 hadi leo.

Mheshimiwa MWIGULU anafuatilia changamoto za jimbo lake kwa ukaribu mkubwa kuliko wabunge wa majimbo mengine, ni Mbunge ambae anatambua yupo Bungeni kwa ajili ya wana IRAMBA kwanza na mengine yanamkutia huko.

Amebahatika kuwa kwenye wizara mbali mbali lakini hiyo haimsahaulishi kuhusu ufuatiliaji wa miradi ya jimboni kwake.

Na mheshimiwa Waziri MWIGULU anajua yupo Bungeni kwa udhamini wa chama gani hivyo humpelekea kuwa karibu na Viongozi wa chama chake katika kushiriki kujenga chama kuanzia shina ,tawi,kata,Wilaya,mkoa na Taifa.

Kwa namna hiyo ya namna ambavyo anatambua waajiri wake ndio maana linapotokea swala la kuomba ridhaa huwa anashinda wapinzani wake kwa ushindi uliomkubwa zaidi.

Mnamo mwaka 2015 alishinda ushindi wa asilimia kubwa mno mbele ya mpinzani wake KILIMBA aliyepata kura 92 na mwenzake JAIRO aliyepata kura 51 wakati huo MWIGULU aliwashinda kwa kujikusanyia kura 1,826 .

Ushindi huo ulikuwa mkubwa mno ambapo leo tena 2020 haiwi maajabu kuona anashinda kwa ushindi ule ule wa kujinyakulia kura 617 ambapo mwenzake alijizolea kura 14 tu.

Hayo ni majibu ya ukaribu na waajiri wake ambao ndio wapiga kura wake. Kwa aina hii ya namna anavyolihudumia jimbo la Iramba Magharibi atakaa hadi aombe kupumzika mwenyewe.
 
Nikishika karatasi ya kupigia kura nikakuta picha za Mwigulu na Kishoa , nitaenda moja kwa moja kumpigia kura Kishoa.

Mwigulu nitampangia kazi nyingine malishoni.
 
Mwigulu Nchemba ni majina ya Kisukuma, Iramba Magharibi wanakaa Wanyiramba. Wezi wa majina, watoa rushwa, wakatili, wambea, wakurupukaji, washamba, limbukeni...wote mwisho Oktoba mwaka huu kwa wale ving'ang'anizi ambao bado watakuwepo. Oktoba njoo, Tanzania mpya njoo, Watanzania waweze kuishi kwa uhuru, haki, amani na furaha chini ya viongozi wenye busara na hekima wanaoheshimu na kuitetea Katiba watakayoapa kuilinda.
 
Haujaeleweka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwigulu Nchemba ni majina ya Kisukuma, Iramba Magharibi wanakaa Wanyiramba. Wezi wa majina, watoa rushwa, wakatili, wambea, wakurupukaji, washamba, limbukeni...wote mwisho Oktoba mwaka huu kwa wale ving'ang'anizi ambao bado watakuwepo. Oktoba njoo, Tanzania mpya njoo, Watanzania waweze kuishi kwa uhuru, haki, amani na furaha chini ya viongozi wenye busara na hekima wanaoheshimu na kuitetea Katiba watakayoapa kuilinda.
Umepanic brother
 
Back
Top Bottom