Mwigulu Nchemba akiwaaga wanaTimu wa Kampeni ya CCM Arusha leo.

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
Huu ndiyo ujumbe wake,

Poleni sana wana Arusha kwa mlipuko wa bomu jana.

Mungu ibariki Arusha

Mungu ibariki Tanzania.

Habari zaidi pata kutoka TANURU LA FIKRA.

Ambatanisho la Picha kwenye kikao cha kuagana.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    133.9 KB · Views: 818
Mungu atamjibu udhalimu aliokuja kuufanya hapa arusha yeye na Nape Mmnauye. Amefanikisha jaribio lake la kwanza. Next time inawezekana ikawa ngumu sana
 
Tukiwa bado wenye huzuni na tunaomboleza tusisahau kutafuta majibu ya maswali magumu yaliyo mbele yetu ambayo vielelezo vinatuongoza na kutuonyesha njia ambayo tukiifuata kwa uangalifu na kwa msaada wa Mungu, hakuna pasi shaka tutafika kule ambako shetani amejificha.





Binadamu tumeumbwa na kupewa vitu viwili viwili. Macho mawili, mikono miwili, miguu miwili, pua mbili, masikio mawili na hata matendo yetu na muonekano uko mara mbili. Waingereza wanasema, Don't judge a book by its cover. Mungu ndiye atatuonyesha which cover is this?.


 
Last edited by a moderator:
Mbona anakimbia Arusha? Aende na hospital kwa majeruhi, muuwaji huyo. Siku zake zinahesabika
 
tukiwa bado wenye huzuni na tunaomboleza tusisahau kutafuta majibu ya maswali magumu yaliyo mbele yetu ambayo vielelezo vinatuongoza na kutuonyesha njia ambayo tukiifuata kwa uangalifu na kwa msaada wa mungu, hakuna pasi shaka tutafika kule ambako shetani amejificha.





binadamu tumeumbwa na kupewa vitu viwili viwili. Macho mawili, mikono miwili, miguu miwili, pua mbili, masikio mawili na hata matendo yetu na muonekano uko mara mbili. Waingereza wanasema, don't judge a book by its cover. Mungu ndiye atatuonyesha.



ila na wewe jamaa mbona unatoa harufu mdomoni.huwezi ukawa unawalinda wauaji halafu ukafikiri mungu hawezi kukuadhibu adhabu ipo amini usiamini. Ukweli mbona uko wazi kuwa ccm wanahusika hata mtoto mdogo wa chekechea analijua hili.
 
Last edited by a moderator:
Toka Mwigulu Nchemba apewe cheo CCM imekuwa si kile chama nilichokijua mwaka 1977 siku tunasherehekea kuzaliwa kwake.
 
Last edited by a moderator:
Toka Mwigulu Nchemba apewe cheo CCM imekuwa si kile chama nilichokijua mwaka 1977 siku tunasherehekea kuzaliwa kwake.
Huo ni mtazamo wako na una heshimiwa.

Hata wahenga walisema, mzoea vya kunyonga, vikibadilika na kuwa vya kuchinja, lazima anakuja na sababu kwa sababu haviwezi.

Je, hawa watu walikuwa kwenye kikao wanafikiriaje kauli yako au wewe unawafikiriaje ukiwa pekee na kauli yako hii wakati tunamuona Mwigulu Nchemba ana wana kampeni wake wengi.
 
yaani anajiona yeye ni kipanga kweli,anafikiri atawafool watu wote muda wote?ipo siku atakuja aibika
 
Watu hawa wapo,kwa makusudi maalum.

1.inawezekana upeo wao wa kuchambua mambo hapo ndipo ulipifikia.
2. Wengi wanaweza kuwa ni wale wanaotegemea fadhila,wa njia ya masomo,biashara.......
3.baba zao wako kwenye mkondo uleule.

4.sura nyingi si za wakazi wa Arusha.chunguzeni hilo mtakuja kutupa habari.

Pamoja na yote,tunayoyafanya Mungu wetu yupo anatutazama.
 
Jina la Mwenyezi Mungu halitajwi tajwi bure na hata yeye aliwakanya wale wanao mtaja taja.

Binadamu wana sura mbili. Usiwaone wanaomtaja taja Mwenyezi Mungu ukafikiria ni wacha Mungu. Jaribu kuwaangalia upande wa pili.

Wanaweza wakatamba sana hapa duniani kwa kulitaja jina la Mungu wakisema walianza na Mungu na watamaliza na Mungu lakini mwisho wake Mwenyezi Mungu atawaambia hivi,

Matthew 7:21-23
"Not everyone who says to me, 'Lord, Lord,' will enter into the kingdom of heaven - only the one who does the will of my Father in heaven.
On that day, many will say to me, 'Lord, Lord, didn't we prophesy in your name, and in your name cast out demons and do many powerful deeds?'
Then I will declare to them, 'I never knew you. Go away from me, you lawbreakers!'

Surah Ibrahim
21. And they all shall appear before Allâh (on the Day of Resurrection) then the weak will say to those who were arrogant (chiefs): "Verily, we were following you; can you avail us anything against Allâh's Torment?" They will say: "Had Allâh guided us, we would have guided you. It makes no difference to us (now) whether we rage, or bear (these torments) with patience, there is no place of refuge for us."
 
Tukiwa bado wenye huzuni na tunaomboleza tusisahau kutafuta majibu ya maswali magumu yaliyo mbele yetu ambayo vielelezo vinatuongoza na kutuonyesha njia ambayo tukiifuata kwa uangalifu na kwa msaada wa Mungu, hakuna pasi shaka tutafika kule ambako shetani amejificha.





Binadamu tumeumbwa na kupewa vitu viwili viwili. Macho mawili, mikono miwili, miguu miwili, pua mbili, masikio mawili na hata matendo yetu na muonekano uko mara mbili. Waingereza wanasema, Don't judge a book by its cover. Mungu ndiye atatuonyesha which cover is this?.





Upuuzi wa ku "spin" unafika mahali kuwa kituko kila wakati ukweli unapojitenga
 
Last edited by a moderator:
anamjua MUNGU huyu? mnafiki mkubwa!!!!hujiulizi kwa nini mahali uendapo damu lazima imwagike?TAFAKARI SANA
 
Watu hawa wapo,kwa makusudi maalum.
Kama wako kwa makusudi maalum hata wewe uko hapo ulipo kwa makusudi yako maalum kama wao.

1.inawezekana upeo wao wa kuchambua mambo hapo ndipo ulipifikia.
Kila binadamu ana upeo alijaliwa katika kuchambua mambo lakini haina maama upeo wako unawazidi wanadamu wote. Hata wewe inawezekana una upeo kiduchu wa kuchambua mambo.
2. Wengi wanaweza kuwa ni wale wanaotegemea fadhila,wa njia ya masomo,biashara.......
Huwezi kuleta dhana ya WANAWEZA na kuifanya kuwa ni hoja. By the way, kwani watu wanaojiunga na CHADEMA hawategemei chochote katika maisha yako kutoka CHADEMA. Haya ndiyo mawazo ya kidikteta kuwaona watu walioko kwenye vyama vingine kama ni wajinga na uwezo wa kuchambua mambo ni mdogo zaidi yenu. Who are you to judge human. Hii ndiyo demokrasia, wanasema ukitaka unaacha. Watu wana maamuzi na maisha yao kama ulivyo na maisha yako.
3.baba zao wako kwenye mkondo uleule.
Kwanza umejuaje kama wana baba?. Kwa hiyo wewe uko CHADEMA kwa vile baba yako yuko huko?. Hizi ni fikra mufilisi kabisa.

4.sura nyingi si za wakazi wa Arusha.chunguzeni hilo mtakuja kutupa habari.
Kwani kuna muhuri wa watu wa maeneo fulani. Haya mawazo yenu ya kimajimbo jimbo ndiyo yanaleta hizi mentality za PROFILING. Hao ni Watanzania.
Pamoja na yote,tunayoyafanya Mungu wetu yupo anatutazama.

You seem to be desperate and frustrated?. Vile vile kumbuka Usilitaje bure jina la Mwenyezi Mungu.

Hizi ndizo siasa. Wanasema, usipopenda, unaacha.
 
Kulia na kucheka zote kelele...............asanteni kwa yote mliyoyafanya hapo arusha na Mungu awajalie afya njema na pia awape nguvu za ziada za kuendeleza yale yote mmiliyokusudia kuyafanya siku za mbeleni.....amina
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom