Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,735
- 6,291
Waziri wa Fedha na Mipango mnachokifanya hivi sasa ni kama vile mna shida sana ya pesa na mmeishiwa ubunifu na sasa mnataka kutuvika Mizigo ya madeni na matatizo ya Serikali kwa gharama yeyote ile.
1. Mmetuongezea kodi ya katika mawasiliano ya simu kwa vocha na vifurushi wakati tunalipa VAT. Uliposemwa semwa unadai mikopo ya SGR na Bwawa la Nyerere ni mikubwa itatuumiza so mnataka mzibezibe humo.
2. Mkatuongezea kodi nyingine ktk mafuta mkidai mnataka kumalizia barabara zilizoaki.
3. Sasa mnakuja tena na kodi ya Majengo kulipiwa kwenye Luku, Yaani unampunguzia Mpangaji idadi ya Token zake ili amlipie mwenye nyumba kodi ya Majengo. Hapo ameshalipa Maji, Kodi ya pango, bado ana maisha yake pia.
Hilo mmeona halitoshi mumpunguzie na Unit alipe kodi ya Jengo yeye halafu aende akamdai mwenye nyumba ambaye hata nyinyi Serikali kulipana naye hiyo kodi ya Jengo ni mpaka kizaazaa na vitisho vingi. Siyo bomu hili mnaenda kupika la kesi za madai na dhuluma?
Mahakama gani inayomaliza kesi ya madai ndani ya mwezi mmoja?
NARUDIA TENA, BWANA MWIGULU NCHEMBA UNATAKA KUTUCHONGANISHA NA MAMA YETU NA UNATURUDISHA UNYONGENI. MBONA SHUJAA MMEANZA KUMZIDI SHUJAA KATIKA KUTUBANA?